Sera ya ushuru sifuri ya China yapiga jeki mnyororo wa thamani wa maparachichi nchini Kenya

Sera ya ushuru sifuri ya China yapiga jeki mnyororo wa thamani wa maparachichi nchini Kenya

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,276
Reaction score
1,241
VCG111638516359.jpg


Katika eneo la mashambani lililotanda rangi ya kijani katika Kaunti ya Murang'a katikati mwa Kenya, Jeff Ngigi Mburu alifurahia sana miparachichi yake aina ya Hass, huku akistarehe kwa upepo mwanana wa alasiri.

Mkulima huyo kijana alifurahia kuzungumza na wafanyakazi kadhaa kutoka vijiji jirani ambao alikuwa amewakodi kuchuma maparachichi yaliyokomaa kwa ajili ya kupelekwa kwenye kituo cha ukusanyaji na baadaye kwenye kiwanda cha kusindika mafuta ya parachichi kinachomilikiwa na Wachina kilichopo nje kidogo ya Nairobi.

"Tulikuwa tukipitia changamoto kadhaa huko nyuma, lakini wasindikaji wa mafuta ya parachichi wametusaidia, wakitupa soko la uhakika kwa matunda yetu na bei nzuri zaidi," Mburu aliambia Xinhua wakati yupo kwenye shamba lake.

Yeye ni miongoni mwa mamia ya wakulima wadogo wa maparachichi ya Kenya ambao huuza mazao yao moja kwa moja kwa kampuni ya Sanmark Limited, ambayo ni ya kusindika mafuta ya parachichi inayomilikiwa na Wachina iliyoko katika Eneo la Usindikaji wa bidhaa za kusafirisha Nje la Mto Athi, kitovu cha viwanda cha kusini mashariki mwa Nairobi.

Katikati ya shughuli nyingi katika kiwanda cha Sanmark Ltd., Mohamed Khan, meneja uendeshaji, alichukua muda kusimamia upakiaji wa maparachichi laini ambayo yalikuwa yametolewa kwa ajili ya kusagwa na kuwa mafuta ghafi.

"Matunda yanapofika kiwandani, tunayahifadhi hadi yatakapoiva vizuri. Kisha timu ya upangaji huyaleta kwenye mashine ya kusagwa ili kutenganisha vitu vikavu na majimaji," Khan alisema.

"Mchakato unaofuata ni kutenganisha maji na matunda, baada ya hapo huingia katika hatua ya mwisho ya kufungasha mafuta ya parachichi," aliongeza.

Kampuni ya Sanmark Ltd. ina mashine za kisasa za kusindika na kupima mafuta ya parachichi ili kuhakikisha yanafikia viwango vinavyohitajika vya kusafirisha kwenda China na masoko mengine ya nje kama vile Ulaya na Marekani.

Khan alielezea ongezeko la mahitaji ya mafuta ya parachichi nchini Kenya na nje ya nchi, akitaja faida zake za lishe na kiafya, ambazo zimeleta faida kubwa kwa wakulima wa ndani.

Sera ya ushuru sifuri ya China, ambayo imeanza kutekelezwa Mei 1, inaahidi nyakati bora kwa wadau wote walio katika mnyororo wa thamani wa parachichi, wakiwemo wakulima, wakusanyaji, wasindikaji, na wauzaji nje.

"Tayari tunafurahia ushuru sifuri. Unawahimiza wawekezaji wa China kuja kwa wingi kuanzisha vituo vya TEHAMA kwa ajili ya kuwafunza wakulima wenyeji," Khan alisema.

"Kabla ya ushuru sifuri, tulikuwa na rasilimali chache katika suala la ufadhili ambao tungeweza kuwapa wakulima, lakini ushuru huo ukiwa haupo tena, kuna ufadhili wa ziada uliobaki kwa mwekezaji, ambao unaweza kupelekwa kwa mkulima. Unamwezesha mkulima," aliongeza.

Khan alisema kituo hicho kinalenga kukusanya hadi tani 100 za maparachichi kwa wiki na kuziba pengo la mwingiliano kati ya kiwanda cha usindikaji na wakulima.

Kiwanda cha usindikaji mafuta ya parachichi pia kimetoa ajira yenye faida kwa vijana wenyeji wenye ujuzi kama Ann Mwende, meneja wa udhibiti wa ubora katika kampuni ya Sanmark Ltd., ambaye alisomea kemia ya uchambuzi katika chuo kikuu cha umma.

Mwende tayari amevuka kizuizi kwa kujitosa katika shamba ambalo hapo awali lilikuwa na wanaume wengi, na kazi yake kwa siku inahusisha kuchambua unyevu na vitu vikavu katika maparachichi yanayopelekwa kiwandani kwa ajili ya kusagwa na kutengeneza mafuta.

Alibainisha kuwa usindikaji wa mafuta ya parachichi umetoa mapato ya uhakika kwa wafanyakazi wa kiwanda na wakulima, huku kiwanda cha kusafishia mafuta kinachotarajiwa kuanzishwa na Sanmark kitaleta ajira mpya kwa wafanyakazi waliofunzwa.

"Kiwanda cha kusafishia mafuta kitakuwa na matokeo mazuri. Sasa tuko watu wawili katika maabara, lakini tutakuwa na wengine zaidi. Hapo ina maana fursa zaidi za kazi. Tutakuwa tukifanya kile tunachojifunza na kuwafundisha watu wengi zaidi," Mwende alisema.

Virginia Mbatha, afisa mkuu mtendaji wa Virginia Orchards, ambaye ni mkusanyaji, alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikiipatia Sanmark aina tofauti za maparachichi kwa ajili ya kusindika na kutengeneza mafuta.

Akiwa na wakulima karibu 10,000 katika mtandao wake, Mbatha alisema wanapata faida kubwa kutokana na soko lililopo ambalo limetolewa na msindikaji wa mafuta ya parachichi wa China.

Alisifu msamaha wa kodi wa China kwa maparachichi na mazao ya kilimo yanayoagizwa kutoka Kenya, akisema umepanua soko la wakulima wa ndani, wakusanyaji, na wauzaji nje.

"Tunaishukuru China kwa kutupa fursa hii ya ushuru sifuri. Tutaweza kuzalisha maparachichi zaidi, na wakulima watafurahia faida kubwa zaidi. Sasa tunaona faida zikimfikia mkulima," Mbatha alisema.
 
Tz huku wachina wanawakwepa maana bei zao wanalalia sana

Ova
 
Back
Top Bottom