Wadau wasisitiza umuhimu wa kukuza huduma ya msaada wa kisheria nchini

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Kufuatia changamoto ya huduma ya msaada wa kisheria kwenye maeneo mbalimbali nchini baadhi ya wadau wamedai kuwa kuna athari ambazo zinaweza kuwa zinatokea kwenye jamii kutokana na huduma hiyo kukosekana hivyo wamesisisitiza umuhimu wa wadau pamoja na Serikali kuendeleza jitihada za kuwezesha wananchi kufikiwa na usaidizi wa kisheria.

Dk.Veronica Bachumi ambaye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM- Shule ya Sheria), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Msaada wa Kisheria chuoni hapo, amesema kuna baadhi ya maeneo nchini hususani vijiji ambayo hayajafikiwa huduma ya msaada wa kisheria hali ambayo amedai kuwa inaweza kuwa sababu ya baadhi ya haki kukiukwa.

"Watanzania wengi hawana uwezo kumudu gharama za mawakili hasa kwa maeneo ambayo yako mbali na vijijini, ambapo hata kama wakati mwingine mtu anaweza kuwa na hiyo hela lakini unakuta hakuna mawakili au watu wa kuweza kutoa huduma hizi"amesema Dk. Veronica Bachumi

Kwa upande wa Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema kuwa amesema kuwa huduma za msaada wa kisheria zinaitajika zaidi ili kuwafikia wananchi wa maeneo yote nchini, amedai kuwa elimu hiyo isipofika kwenye jamii za chini kuna uwezekano wa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa baadhi wananchi hawana uwezo wa kulipa mawakili ili wapate huduma.

"Ni watanzania wengi ambao hawawezi kuajiri mawakili kwanza kuna maeneo ya vijijini ambayo hayana huduma za mawakili au wanaotoa msaada wa kisheria ni kwamba watanzania wengi watakosa kupata msaada wa kisheria mahakamani, watanzania wengi haki zao zitakiukwa, na ukiukwaji wa haki za binadamu utakuwa mkubwa na hali ya watu kutofuata sheria kwenye jamii itakuwa kubwa."amesema Olengurumwa.

Wadau hao wameyasema hayo leo Augosti 7, 2023 kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyondaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki Binadamu Afrika Mashariki (EAHRI) pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa baadhi wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria katika Mkoa wa Dar es salaam, Pwani na Tanga. Ambao mada mbalimbali zinawasilishwa na kutoa fursa kwa washiriki kuchangia huku mada hizo zikiwa zinalenga kuchochea utoaji huduma kwa ubora zaidi.

Mafunzo Maalum ya umahiri kwa wasaidizi wa Kisheria ni miongoni mwa malengo ya sheria yetu ya msaada wa Kisheria, kulikuwa na takwa lazima wapewe mafunzo na tumeanza na mafunzo ngazi ya chetu na baada ya muda tutaanza diploma mpaka tupate ithibati.

Aidha Naibu Mkuu wa Shule ya Sheria akizungumzia mafunzo hayo amesema kuwa wameazisha kozi ya kitaalama inayolenga kuwezesha watoaji wa huduma hiyo kubobea zaidi ili kukuza utoaji wa huduma, amesema kozi hiyo kwa sasa imeanza kutolewa ngazi ya cheti (certificate) na kuwa mbeleni wataindeleza mpaga ngazi za juu zaidi hivyo amewataka wadau kutumia fursa hiyo kujieleza kupata ujuzi zaidi.

"Wale wasaidizi ambao hawajapata masomo Maalum mnaweza kutumika fursa hiyo dirisha la usajili limeshafunguliwa. Haya ni mafunzo muhimu sababu yanamuandaa mwanafunzi kwenda kutoa huduma bora" amesema Dk. Clement Mashamba.
 
Back
Top Bottom