Mkuu naomba nikushauli kwamba kilimo kina faida nyingi sana lkn niwachache sana wanakuwa wanufaika na izo faida kwasabubu ya kuzingatia vitu vifuatavyo
1) Mpangilio (Calendar) ya shughuli za shamba ; mkulima kabla ya kuingia shambani inabida ajuwe analima nn na kwa muda gani na atatumia jitiada gani kufanikisha iyo mipango yake kwa mfano inabidi ajuwe taharifa sahihi kuhusiana na zao lake analotaka kulima maana itamsaidia kupanga ratiba sahihi ya kuhudumia shamba lake kama vile maandalizi ya shamba, kupanda, kuweka mbolea, kupalilia na kuvuna pia ! Nakumbuka mwaka jana nililima Tikiti kila kitu kilienda sawa lkn nilikosea muda wa kuvuna yani nilichelewa kwaiyo kila ukipata mteja anakupangia bei ya chini kwasababu anajua auna namna ya kujitetea pia ilinighalimu kukubaliana na bei yake kwa sababu mzigo ungenidodea kwaiyo inabid mkulima uwe makini kwenye calendar apo utaweza kuepuka hasara za kujitakia
2) Masoko ! Apa niwe mkweli tuu akuna watu wenye roho ngumu na ambaya ambazo azielezeki kama madalali
maana mazao mengi kama vile matikiti, vitunguu na achungwa na nk uwezi kupeleka sokoni eti ukauze aisee yan nibola umuite dalali mmalizane mapema kuliko upeleke sokoni maana wafanya biashara awana mamlaka ya kununua mazao kwa wakulima moja kwa moja bila dalali kwaiyo dalali anapanga bei anayo itaka yeye lkn ili uweze kushindana na dalali jitaidi kulima mazao yenye ubora zaid au nenda kinyume na wakulima wenzio yani unaenda kinyume na msimu kwaiyo unajikuta pekeyako ndo unamzigo apo kidogo unaweza kutaja bei unayo itaka ww lkn ili uende kinyume na msimu inabidi ulime ndani ya protective environment condition yan Green house apo ndo utaweza kufanikiwa
3) Nidhamu ! Kilimo ni kazi kama kazi nyingine kwaiyo inabid mkulima awe na nidhamu ya kutosha kama vile kufuata ratiba aliyo jiwekea na kufuatilia shamba lake endapo ameweka kibarua kwa mfano kilimo cha matikiti kinaitaji nidhumu ya juu Sana yan ikipita siku tatu ujaenda shambani apo ujuwe kuna gharama utaingia ili kufix ule muda ambao ukwenda shambani yani Time is money
Vipo vingi vya kuzingatia lkn ivyo ni moja wapo