Kilimo gani kina asilimia kubwa ya kufanikiwa?

Biashara ya kilimo nadhani sio biashara ya cash wakulima wengi hawaelewi hilo. Kuna mazao ni wanted hayo unaweza uza kwa cash, ila mazao kama hizo nyanya asee kwa mkulima nadhani ingekua vyema ukiwa unavuna unaandaa wafanyabiashara wako wa uhakika Unawakopesha.

Hamna ataekataa kukopa..unawapelekea hadi walipo kwa gharama zako then hela yako unaipitia after a month ila tatizo wa wakulima wa Tanzania mitaji yao huishia kupanda mpk kwenye Kuvuna, akishavuna pale hana hata hela ya Kusafirisha yale mazao kuyaleta MJINI (MASOKONI) anakaa anatafuta mteja angali mazao yapo shambani.

Mwisho wa siku mazao yanaendelea kuoza na kuharibika ila naamini wakulima wakijipanga kwenye kilimo akaingia na Hela ya Mbegu, Kilimo, Mavuno, usafiri mpaka kwa mlaji kisha akakopesha. Uhakika wa kutolia ukosekanaji wa SOKO ni mdogo sana sana.
Kwa waTz, ukikopesha andaa kabisa gharama za kesi za madai
 
Perimeter,
Yaani wewe ni mweupe sana, ila kwa suala la jana nilishindwa kushangaa. Hivi mkulima gani smart unalima nyanya uvune miez hii jamani? Sijui ugeni au nini?

Hapa napoishi naishi karibu na mto so majirani wote wanalimaga nyanya, yaani toka nimefika kila siku naletewa minyanya masado na masado manyanya yamedoda nakula salads hadi nimekinai!
Limeni kwa misimu jamani, nyanya ivune December kuelekea January au ivune April hivi
Hapo ni kilimo cha umwagiliaji au 'green house' ndo unaeza kupanga muda wa kuvuna.. ila kwa kusubiri mvua, lzm utoe offer ya mavuno buree
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30.

Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Tatizo inakuwa ni mtaji ila kama utaweza kupata mtaji kwenye kilimo na ukaanza kununua nafaka kama mahindi utapiga hela na stress hazitakuwepo kabisa
Ni kweli kitu kinachitufanya kulima au kufanya biashara katika scale ndogo ni MTAJI. mtu mwenye taji mdogo ni vizuri kulima, pia ukiwa na muda. ukiwa na mtaji mkubwa na usimamizi thabiti pamoja na ushauri wa kitaalamu kilimo hakikutupi.
 
Mimi nauliza!

Ivi kwanini serikali ya Tanzania huwa inawapiga vita sana wakulima wanapotaka kujikwamua?

Maana kila wanapoelekea kupata unafuu serikali lazima iingilie kati na kuwafanyia figisu

Same to mahindi,korosho, pamba, kahawa (hii wamehakikisha mpaka soko wameliua kabsa) kunde n.k
Kuongeza dependency chain na kuwa na kundi kubwa la wenye uhitaji wa mambo basic kwenye maisha. Feeding an hungry man with just little food ili asife, lakini asifanye kazi ya maana. otherwise haieleweki karibu miaka 60 ya uhuru tunaimba wimbo uleule.
 
Mkuu naomba nikushauli kwamba kilimo kina faida nyingi sana lkn niwachache sana wanakuwa wanufaika na izo faida kwasabubu ya kuzingatia vitu vifuatavyo

1) Mpangilio (Calendar) ya shughuli za shamba ; mkulima kabla ya kuingia shambani inabida ajuwe analima nn na kwa muda gani na atatumia jitiada gani kufanikisha iyo mipango yake kwa mfano inabidi ajuwe taharifa sahihi kuhusiana na zao lake analotaka kulima maana itamsaidia kupanga ratiba sahihi ya kuhudumia shamba lake kama vile maandalizi ya shamba, kupanda, kuweka mbolea, kupalilia na kuvuna pia ! Nakumbuka mwaka jana nililima Tikiti kila kitu kilienda sawa lkn nilikosea muda wa kuvuna yani nilichelewa kwaiyo kila ukipata mteja anakupangia bei ya chini kwasababu anajua auna namna ya kujitetea pia ilinighalimu kukubaliana na bei yake kwa sababu mzigo ungenidodea kwaiyo inabid mkulima uwe makini kwenye calendar apo utaweza kuepuka hasara za kujitakia

2) Masoko ! Apa niwe mkweli tuu akuna watu wenye roho ngumu na ambaya ambazo azielezeki kama madalali maana mazao mengi kama vile matikiti, vitunguu na achungwa na nk uwezi kupeleka sokoni eti ukauze aisee yan nibola umuite dalali mmalizane mapema kuliko upeleke sokoni maana wafanya biashara awana mamlaka ya kununua mazao kwa wakulima moja kwa moja bila dalali kwaiyo dalali anapanga bei anayo itaka yeye lkn ili uweze kushindana na dalali jitaidi kulima mazao yenye ubora zaid au nenda kinyume na wakulima wenzio yani unaenda kinyume na msimu kwaiyo unajikuta pekeyako ndo unamzigo apo kidogo unaweza kutaja bei unayo itaka ww lkn ili uende kinyume na msimu inabidi ulime ndani ya protective environment condition yan Green house apo ndo utaweza kufanikiwa

3) Nidhamu ! Kilimo ni kazi kama kazi nyingine kwaiyo inabid mkulima awe na nidhamu ya kutosha kama vile kufuata ratiba aliyo jiwekea na kufuatilia shamba lake endapo ameweka kibarua kwa mfano kilimo cha matikiti kinaitaji nidhumu ya juu Sana yan ikipita siku tatu ujaenda shambani apo ujuwe kuna gharama utaingia ili kufix ule muda ambao ukwenda shambani yani Time is money

Vipo vingi vya kuzingatia lkn ivyo ni moja wapo
Well said.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom