Kilimo chenye viashiria vya faida kubwa

mwagito25

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
633
350
Habarini wana jamvi, ninapenda kuwashirikisha jambo ambalo nililiona huko mkoani Iringa, wilaya ya Mufindi.

Mwezi march mwaka huu 2021, nilienda kijijini kwetu huko mufindi, nikabahatika kumtembelea ndugu mmoja shambani kwake.

Shamba lake la parachichi lenye ukubwa wa ekari 15, lakin sehemu ambayo tayari kaanza kuvuna ni ekari tano.

Jambo la kuvutia kuliko yote ni kwamba kwa sasa soko bado lipo imara saana endapo umepanda mbegu inayofaa kuuza nje ya nchi. Mbegu hii ina maganda imara na inachelewa kuharibika.

Lakini pia kilichonishangaza ni kwamba matunda ameanza kuvuna baada ya muda wa miaka miwili na nusu tangu alipopandikiza miche.

Nilipoona hayo ilibidi niendelee kuhoji kuhusu maeneo ambayo matunda hayo hustawi, na jibu lilikuwa ni kaskazini mwa nchi na nyanda za juu kusini ingawaje kwa kaskini kikwazo ni bei ya ardhi kwa kuwa hupaswi kukodi kwani ni zao la kudumu.

Lakini pamoja na mazuri hakusita kunijuza changamoto za kilimo hiki ambazo ni kama ifuatavyo:-
  • Upatikanaji wa mbolea ya samadi.
  • Kumwagilia miche wakati wa kupandikiza kwani hupaswi kuipanda msimu wa mvua, hivo kama shamba halipo karibu na mto utapaswa kuwa na vifaa vya kuhifadhia maji ili uweze kumwagilia miche hadi mvua itapokuja.
  • Kuweka fenzi ya wire ili kuilinda miche ya mifugo kama mbuzi nk.
Pamoja na changamoto hizo lakini bado kwa utashi wangu si chochote ukilinganisha na faida zake kwani nimeahuhudia akilipwa zaidi ya 6M kwa mavuno ya awali kabisa. Hii ni kusema kwamba msimu unaofuata atapata zaidi kwa sababu miche bado inakua hivyo matunda yataongezeka.

Kwa wapenzi wa kilimo endeleeni kufuatilia kwa undani kama utavutiwa na maelezo hayo.

NB: Fuatilia kwa umakini kwa faida yako, usikatishwe tamaa wala usivutiwe tu bila kujiridhisha na uhalisia.

Asanteni
 
Kusini hii wanaiita green gold inalipa sana.
In 2 to 3 years unavuna mpka miaka 50 na kuendelea.
Mbolea wengi huenda kuifuata kanda ya kati uko mavi ya ngombe mengi tuu
Asante kwa rejea
 
Pale kijijini kwetu moshi Nina hela zaidi ya 28 japo Ni za urithi lakini hii mada imenifikirisha kidogo maana naona Kama huku mjini napoteza muda kwa kuwatumikia wengine wakati frusa za kuweza kuendelea Zipo!
 
Parachichi za kisasa zinahitaji uangalizi wa hali ya juu, kama huna muda na fedha ya kuhudumia usijaribu hiki kilimo
Nilimsikiliza jamaa mwny Co. Ya Malembo farm kwny kipindi cha kina masudi kipanya pale clouds+ cha saa 2 usiku.

Akasema sa hivi kinacho trend huko mitandaoni/mashambani ni kilimo cha parachichi(HASS) anasema wakulima wanalima sana na wote ukiwauliza mtauzia wapi wanakwambia Ulaya,ukiwauliza Ulaya nchi ipi maana sio nchi zote tunafanya nao biashara hawana majibu,ukiwauliza mnajua ni standards gani hizo nchi za ulaya zinataka ili kununua hayo matunda wao hawana majibu ila wanakwambia tu cha msingi iwe ni aina ya HASS.

Yajayo yanafurahisha,Parachichi inaenda kua kama kilimo cha Tikitimaji.
 
Back
Top Bottom