Kilimo cha Tufaa (Apple)

Nilikuwa na watch Youtube kuhusu mkulima wa Apple Nchini Kenya anaitwa Wambugu (Wambugu Apple) nimekuwa inspired aisee, ingia Youtube andika Lynn Ngugi Wambugu apple utaiona, na anatoa darasa free of charge, kuna mtu yoyote ni mkulima wa Apple atupe dondoo la soko hapa Tanzania?
Hakuna mchongo wa maana ukazagaa mtandaoni kamwe ukiona kitu free kina gharama kubwa
 
Imani yangu itastawi na kuota matunda, hapo kuna miche aina mbili inayohitaji au kukua kwenye mazingira ya baridi sana na Ile ya wastani.

Ndiyo maana kama umenisoma vyema nimechukua Miche 4 ambayo ndani ya mwaka utanipa majibu ya ukuaji wake na nitafanya tathimini lya uzalishaji kisha nitaamua kupanda mingi au laa. Ngoja tuone mwaka siyo mkubwa nitajua mbovu na mbichi.
✅👏👏👏🙏
 
Mche wa Apple ni buku 3
Maybe ulipigwa
Mkuu, ni wapi wanakouza sh 3,000/=?

Wakenya wenyewe wanauza Ksh 500/= kwa mche mmoja, ukiibadilisha kwa hela ya Tanzania si chini ya Tsh 8,000/=.

Mimi nafikiri kama miche aliyouziwa ni "mizuri", hata kwa Tsh 10,000/= bado ni bei nzuri
 
Mkuu, ni wapi wanakouza sh 3,000/=?

Wakenya wenyewe wanauza Ksh 500/= kwa mche mmoja, ukiibadilisha kwa hela ya Tanzania si chini ya Tsh 8,000/=.

Mimi nafikiri kama miche aliyouziwa ni "mizuri", hata kwa Tsh 10,000/= bado ni bei nzuri
Miche ya apple ya Wambugu ni ghari sana na ile ndio miche ya uhakika, hii ya Iringa siijui hata ni aina gani ya apple. Wambugu apple ni nzuri sana
 
Mkuu, ni wapi wanakouza sh 3,000/=?

Wakenya wenyewe wanauza Ksh 500/= kwa mche mmoja, ukiibadilisha kwa hela ya Tanzania si chini ya Tsh 8,000/=.

Mimi nafikiri kama miche aliyouziwa ni "mizuri", hata kwa Tsh 10,000/= bado ni bei nzuri
Usipoteze muda kumuelewesha mtu asiyejua, nimeridhia mie kununua Sh 10,000/ au Sh 8,000/ yeye anasema Sh 3,000/ hawa ndiyo wanaishiaga kuvunja moyo wenzao.

Hata kama ningenunua Sh 20,000/ najua ulikuwa na kukomaa faida yake hivyo kwangu bei ilikuwa sawa.
 
Miche ya apple ya Wambugu ni ghari sana na ile ndio miche ya uhakika, hii ya Iringa siijui hata ni aina gani ya apple. Wambugu apple ni nzuri sana
Iringa wanazo aina tofautitifauti, na wanayo catalogue yao inafafania kila aina, binafsi niliagiza aina ijulikanayo kama Anna pamoja na Dorsett Golden zinazostawi maeneo yasiyo na baridi sana. Ipo na aina zingine zinastawi kwenye baridi kali.
 
Miche mmoja nilinunua Sh 10,000/ sasa wanauza Sh 8,500/ ila kuanzia Miche 12 nimeona wakitangaza hivyo.
Kuhusu kukua, najua itakuwa hapa nangoja kujua ufanisi wake.
Hata kama itakubali kukua vizuri...kabla ya kufanya large scale shamba ni muhimu kwanza ufanye trials huko shamba...miche 30 au 50....

Miti ya kupanda home huwa inapata special care ambayo ni ngumu ku maintain kwa shamba...ikiwa shamba itakubali with standard care, then utasema jaribio limefaulu....!
 
Unauliza soko usha zalisha? Hivi nani anawaambia kwamba u apaswa kwanza kupewa soko then ndio ukazalishe? Sikiliza unatafuta soko ukiwa na products, Kuna Wamisir huwa wanakuja hadi Tanzania na matunda yao ya sample kutafuta soko.

Hakuna mtu anaweza kukupatia soko kama huna mzigo, mtu anataka aone sample kwanza ndio muongeee biashara.

Zalisha then tafuta soko. by the way Apple si zinaliwa? ni chakula kile so zinaliwa

Kaka labda umesoma hukunielewa ujumbe wangu na pia kuuliza Soko si mbaya kwasababu kuna watu maybe washafanya na kuelewa hili zao vizuri ndio maana unatakiwa kufanya research kwa jambo lolote ambalo ujalianza kujua undani wake na sio kila kinacholiwa kinapendwa na wengi.
 
USha wahi lima hata mchicha? Unajuaje kuna faida kwenye ku export? unaweza ebda shindana na nchi kama Poland na wengineo ambao wana hecta na hecta za Apple?

Siku zote soko la ndani ndio soko la uhakika, internatiina Market isikie tu story zake, sio rahisi kama unavyo dhania

Sijawahi Kaka nasijasema soko la nje ni rahisi na mimi nipo nje naona watu wanavyopambana kuleta mazao huku na kupata faida kila kitu kinawezekana ni kupambana tuu usiwatishe watu ndugu
 
Kustawi itastawi je kuzaa? Hata Dar unaweza panda apple na ikastwai ila kutoa matunda ndio mziki
Mimi nimeotesha apple DSM,, kupata matunda nilishapata ila simshauri mtu aoteshe aple dar..mikoa kama kagera..Arusha iringa Njombe sawa ila DSm ni changamoto saana..kipindi cha joto zinashambuliwa sana, nina mbegu ya wambugu kutoka kenya na nyingine nilinunua kuffel creek nadhani hata tamu tamu wananunua kwao
 
Back
Top Bottom