Tangantika
JF-Expert Member
- Aug 12, 2018
- 4,941
- 6,192
Sio kweli, Mbeya, Njombe wananunuzi wanakuja nyumbani kwako kununua hata kama una mti mmoja.kampuni ya Rungwe wao ndio kidogo wanamasharti hasa ya usafi, mti usiwe karibu na jalala au choo. Hata hivyo soko la ndani ni kubwa sana maana hatuna mahekta ya parachichi panda tu parachichi isitoshe wakenya ndio huja nyanda za juu kununua hivyo Arusha ni karibu kabisa na wakenya unaweza tafuta connection.Hili zao kweli ni deal ila mpaka uliuze ni mziki na wengi hawajui hili.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakenya wenzetu wana export to UK. Jambo lingine ni kwamba Parachichi za Tanzania zinaenda msimu tofauti na ulaya hata tulime ardhi ya mikoa yote inayostawi parachichi hatutoshelezi soko la dunia. Mikoa inayastawi parachichi ni Mbeya, Njombe, Arusha Kilimanjaro, Kgera na Kigoma. Kila sehemu inayostawi kahawa na chai parachichi itakubali.