Bhakusyobhile
Member
- Aug 1, 2018
- 47
- 126
Mkuu kama unataka kulima parachichi nenda MBEYA au NJOMBE, wanalima sana hiyo aina HASS,tena zipo aina tofauti tofauti kama vile GWEN HASS, CALFONIA HASS na LAMB HASS ila kwa sabab unataka kwa ajili ya export nakushauri ulime lamb hass mana ni kubwa halaf lina peke dogooo, pia kuna zile mbegu za burundi kama penkerton na chorquatte zote zina stawi tu. Hata hivyo kama hautapenda ku-export waweza kuwauzia wawekezaji (1kg 2500/3000 pia inalipa sana), wanapatikana hukohuko MBEYA na sasa wako mbioni kufungua plantation zingine NJOMBE.
Na kama unataka kufanya biashara ya kupeleka dar/dom, usiende MOSHI kama mdau flani hapo juu alivyosema nenda RUNGWE ndiko kwenye uhakika wa parachichi iliyobora na yenye faida kutokana na maoni ya walaji,hasa parachi ya x-ikul.ambayo ni kubwa na ina ngozi ngumu, inapatikana kwa wingi sana maeneo hayo na ai haribiki haraka.lakini pia waweza kwenda hata moshi kuangalia aina za kule ili kujiridhisha. Mimi niliyagundua haya yote mana nilikuwa kwenye industry kwa muda wa kama 5yrs hivi.