Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,281
Tumezoea kupanda miche ya ndizi, unaweza kuinunua au kuomba kwa jirani. Lakini ndizi iliyokomaa na kuiva inaweza kukupa mbegu naipanda ndizi kwenye karai bovu lenye matobo ili maji yasituame, weka udongo wenye mbolea kwenye karai na uwe unamwagilia maji kila siku. Baada wiki mbili au tatu utaona majani ya ndizi yanaanza kuota. Miche ikifika urefu wa inch 6 inaweza kuihamishia kwenye kitalu ambacho ni tuta. Hakikisha unaipanda kwa nafasi ya futi mbili kati ya mche na mche.
Miche ikifika urefu wa futi 2-3 unaweza kuihamishia shambani. Katika shamba chimba shimo la futi moja, weka mbolea na udongo, kama viganja viwili kwanza, weka mche wa ndizi funika kwa kwa mbolea na undongo, kabla hukafika juu weka chupa ya litre mbili za maji iliyokatwa kitako. Kitako kiangalie juu. Chupa hii itakusaidia wakati wa kumwagilia.
Maji ni muhimu sana katika kilimo cha ndizi. Unaweza kumwagilia maji kwa mifereji, kwa njia hii huhitaji chupa. Chupa ni muhimu kama unamwagilia kwa ndoo au kwa mpira. Wengi wanachimba kisima na kupump maji kwenye sim tank. Ukiwa na mpira mrefu wa maji unarahisiha kazi.
Wengi tunatumia ndizi kama chakula, kwa kilimo hiki unaweza kuwa na uhakika wa ndizi ya kula kila wiki katika eneo nusu ekari. Zikiwa nyingi huwa ninamenya na kuweka katika mifuko ya plastic na kuhifadhi kwenye freezer. Nyingine huwa ninapeleka sokoni na pia ninavumbika hasa ndizi mzuzu.
Ndizi mzuzu unakweza kuzichemsha na zikiiva unaponda kwenye kinu, zinatoa ugali mtamu sana, ugali huu unawafaa sana wenye kisukari.