Wapenzi wa ndizi: Namna nyingine ya kupika ndizi tamu za kukaanga na nyama ya kuku/ng'ombe

Aaliyyah

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
15,804
37,773
Nafikiri mkopoa kabisa
Naomba ku share na nyie recipe nzuri ya kupika ndizi mzuzu Kwa wale wasiopenda rost na wengine wanaopenda kula chakula Cha tofauti na hakichukui mda kuandaa
Mahitaji
Ndizi zilizokaangwa ambazo umekata shape ndogo size uipendayo na nyama iliyokaangwa unaweza tumia hata mishikski,
nyanya 2 kubwa zikate au zisage
karoti na hoho kata size uipendayo ,mafuta ya kupikia navitunguu(saumu kilichopondwa) na kitunguu maji,pilipili hoho,karoti na chumvi

Hatua ya kwanza
Bandika sufuria Yako jikoni weka mafuta ya kula kijiko kimoja Kisha kaanga vitunguu maji kikianza kulegea weka kitunguu swaumu

Hatua ya pili
Kisha weka nyanya pamoja na chumvi ziache ziive zikiiva weka hoho pamoja na karot acha Kwa dakika 3 zilainike

Hatua ya Tatu
Weka nyama zilizokaangwa au mishikaki Yako Kisha weka ndizi zilizokaangwa geuza na zichanganye vizuri had zichanganyike vizuri acha Kwa dakika moja Changanya Tena hapo zitakuwa tayar Kwa kuliwa

Unaweza kushushia na juis hata soda pia
Kama unaswali unaweza kuuliza pia km nitakuwa sijaeleweka mniwie radhi

IMG_20230929_110531.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom