Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

Habari wakuu!
Hongereni sana kwa harakati na mikakati madhubuti mfanyazo katika kuziteka fursa adhimu kupitia kilimo kwa mstakabari wa future ya familia zenu!

Binafsi nimekuwa nikinufaika na michango yenu katika huu uzi kimyakimya na wengi wenu hapa mmekua mkinihitaji kwajili ya huduma ya miche ya mitiki na wote tumemalizana kimyakimya tena kwa uaminifu uliotukuka!

Nawapa hongera sana nyote mlio thubutu kufanya uamzi wa kuwekeza kwenye upandaji miti-ni uamzi nyeti kwa watu makini na hakika hamtajuta, mbele yenu ni ya neema tele make miti haidanganyi ikishafikia umri wa mavuno basi hesabu pesa pesa pesa!!
Ushuhuda wa hili ninao mwenyewe. Nimezaliwa na kukulia kwa wapanda miti na nimeshuhudia unufaikaji wa mradi huu kwa miaka na miaka ningali mdogo.

Nawasihi msikate tamaa na muendeleze mapambano.
Kwa yeyote atakae hitaji miche ya miti hii asisite kunitafta; Mninga, mkomba/mkola/mkongo, mitiki, syprus carribeae, misila n.k tafadhari weka order nikuhudumie.
Napatikana JF muda wote ukinihitaji.
Karibuni sana...
 
Nilitokanazo mbegu ifakara nikaziotesha ktk kitalu hapa ukerewe lakini hazikuota,na kuna miti ya mitiki kanisa LA roman nansio lakini hutopata mitiki iliyojiotea hapo chini.
 
Hivi Mikaratusi nayo inalipa!? Nimepanda Mikaratusi Ila nataka nipande mitiki msimu wa mwaka huu
Hongera mkuu! hakuna mti usiolipa. Upatapo wasaa panda miti kadri ya uwezo wako. Miti ni mali asikwambie mtu.
Kwa hitaji la miche ya mitiki au punje zake nicheki muda wowote.
Njia nzuri ni kupanda stumps kwenye viriba kama nursery stage ili upate muda mzuri wa kufuatilia ukuaji wa mche na umwagiliaji wa maji kabla hujahamishia shambani kipindi cha mvua za mwaka.
Karibu sana!
 
Mkuu nahitaji hii elimu ya stumps kwenye mitiki
 
Stumps ndio njia rahisi sana kuliko kununua miche au mbegu.
Stumps kuna jamaa moja anaitwa kisima mtafute humu utampata.
Muagizie akuletee stumps nene na nzuri atakuletea.
Mimi stumps 5000 aliniuzia kwa milioni moja.
Akikuletea hesabu kabla ya kummalizia pesa.
Chukua udongo wenye rutuba au inaweza changanya na mbolea ya ngombe .
Kisha mchanganyo huo changanya na fungicides then pakia kwenye viroba.
Wakati wa kupanda stumps
Stumps huwa ni ndefu zikate kwa chini kidogo.kisha zichomeke kwenye vifuko.
Zichomeke hadi ziwe na usawa sawa na udongo ukiojaza kwenye mfuko.
Hapo ni kumwagia tu ndani ya miezi miwili unapori la miti kwenye kitalu chako.
Jitahidi kuilinda na wadudu kwa kumwagia insectcides.
 
Mkuu nahitaji hii elimu ya stumps kwenye mitiki
IMG-20170118-WA0051.jpg
IMG-20161212-WA0029.jpg
IMG-20161212-WA0028.jpg
IMG-20170101-WA0014.jpg
 
Picha hizo zinaonyesha stumps.
Vifuko ambavyo nimejaza udongo na kupanda.
Jinsi zilivyoota na kustawi
 
Mimi natafuta mbao za ujenzi. Ofcourse Kama ningeweza ningetamani nipate mbao za mitiki. Sasa kuna mwenye uzoefu na mbao za mitiki? Kuna Hawa wazungu WA Kilombero Valley Teakwood. Nimetembelea website Yao na kuongea na one of their managers inaonekana focus Yao in export. Anybody anayewajua? Atupie neno hapa. Vile vile Kama kuna mtu anayejua sehemu nyingine wanauza teakwood mbao in large quantity humu humu Tz.

Asanteni in advance.
 
Karibu sana kiongozi. I am caple of preparing for you any amount.
Naomba tuwasiliane tujadili kwa pamoja namna ambavyo tunaweza kukamilisha hitaji lako kwa wakati bila tatizo lolote.
Karibu sana mkuu.
 
Mkuu Bitabo bila shaka umeyasoma waelekezo ya mkuu cumins hapo juu kuhusu stumps...
Kwa kuongezea tuu ni kwamba stumps ni ile miche ya mitiki iliyo dumu kwenye kitalu kwa muda usiopungua miezi 12 tangu kusia.
Miche hii hung'olewa na kukatwa kwa urefu wa angalau nchi4 kuanzia kwenye mzizi mkuu hadi mwanzo wa shina iwe 3" na 1" iwe kuanzia kwenye shina kuja sehemu ya juu ya mche.
Kawaida mizizi midogo hukatwa kwa ustadi na pia mzizi mkuu nao hukatwa na kuondolewa baada ya kile kipimo cha 3"
Stumps hizi hupandwa kila mmoja kwenye kiriba cha nylon chenye urefu angalau 5ft kwa kuweka mchanganyiko wa udongo na mbolea.

Baada ya hapo utakuwa unamwagilia maji ila yawe ya wastani mpaka pale mche utakapoanza kuchipua na kuwa na majani lau matatu, baada ya hapo unaweza kuongeza unyweshaji wa maji kwenye mche wako.

Njia hii ya kuweka miche kwenye viriba ni nzuri make itakurahisishia utunzaji wake na uhakika wa uchipuaji
na hatimae utapunguza gharama za kurudia zoezi la upandaji.

Karibu tena mkuu kwa hitaji jingine.
 
Mimi natafuta mbao za ujenzi. Ofcourse Kama ningeweza ningetamani nipate mbao za mitiki. Sasa kuna mwenye uzoefu na mbao za mitiki? Kuna Hawa wazungu WA Kilombero Valley Teakwood. Nimetembelea website Yao na kuongea na one of their managers inaonekana focus Yao in export. Anybody anayewajua? Atupie neno hapa. Vile vile Kama kuna mtu anayejua sehemu nyingine wanauza teakwood mbao in large quantity humu humu Tz.

Asanteni in advance.
Mtafute mtu anaitwa planie aliposti kwenye huu Uzi kuwa ana mitiki iko tanga.
 
Mimi nilipanda mitiki miche 6000 mwaka 2010 ilikua kama najaribu tu na sina utaalamu sana sasa miti imekua mirefu sana ( kwa kudaria urefu ni zaidi ya jengo la gorofa mbili ) nataka mwenye ujuzi anifahamishe maana nimeambiwa ni muda muafaka kupunguzwa, je hiyo inayopunguzwa naweza pata soko wapi? Maana inayopunguzwa ni zaidi ya miti 2000
 
waone mohammed entreprises
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom