Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by nat867, May 3, 2010.

 1. n

  nat867 Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nafuatilia threads zinazohusu kilimo na kuvutiwa na jinsi mnavyochangia-mfano Elnino na Malila na members wengine. naomba kuuliza kama nitaamua kulima MITIKI (teak wood). Sasa naomba mwenye utaalamu anisaidie kunielewesha yafuatayo:

  1. Je unapotaka kupanda mitiki je mbegu zinauzwa wapi?
  2. Je mbegu unazipanda kwenye vimfuko vidogovidogo na udongo wake (i.e kitalu). je mche unapotolewa kwenye kitalu unaupanda moja kwa moja shambani au kuna process nyingine?- i.e. yaani namaanisha hatua (steps) za kutoa kwenye kitalu kwenda shambani
  3. Je unatakiwa kuweka umbali gani kati ya mtiki/mche mmoja na mwingine kama unataka ikue kwa ajili ya mbao.. na je spacing ni kiasi gani kama unataka ikue na uvune kama milingoti
  4. Je kwenye ekari moja unaweza kupanda miche mingapi?
  5. Je KIWASTANI inachukua miaka mingapi mpaka uvune kupata mbao na pili kupata milingoti
  6. Je kuna paper au website ninayoweza kupata maelezo zaidi?
  nitashukuru sana kwa mwenye kufahamu kunipa maelezo!

   
 2. D

  Dafia Member

  #2
  May 4, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 35
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mbegu za mitiki zinapatikana Tanzania Tree Seed Agency wako Msamvu Morogoro.Kilo moja ya mbegu za mitiki inatosha kuotesha kwenye shamba la hekta moja, ambayo ni wastani wa miti 1500

  Matayarisho:

  • Ganda la nje la mbengu ya mtiki ni gumu sana na lina sumu mbaya.Unatakiwa uloweke mbegu ya mitiki kwa masaa 72, na kila baada ya masaa 12 unatakiwa ubadilishe maji kwa kumwaga maji ya zamani na kuweka maji mapya.
  • Baada ya masaa 72 anika mbegu zako juani kwa masaa 12.
  • Tengeneza kitalu, weka mbolea ya wanyama au mboji, kisha panda mbegu zako kwenye kitalu.
  • Mwangilia maji kila siku asubuhi na jioni, mbegu zitaanza kuota baada ya siku 10 hadi 20.
  • Miche ikifikia urefu wa futi moja, unaweza sasa kuiotesha kwenye shamba lako ulilotayarisha kwa ajili ya kuotesha miti.
  • Kabla ya kungÂ’oa miche hakikisha unamwaga maji mengi, ili mizizi isikatike sana, kisha chukua kisu chenye makali ya kutosha na kata ncha ya juu ya mti na ondoa majani, hii inasaidia mti kuchipuka upya hasa eneo ambalo halina maji mengi.
  • Otesha miti futi 6x6 mitiki inaposongamana, hurefuka haraka ikikimbilia jua angani, hivyo kwa vipimo hivyo miti yako itakuwa mirefu sana na iliyonyooka, baadaye unaweza kuipunguza na kuuza fito za kujengea.
  • Ili upate mbao bora hakikisha unaondoa matawi yanayochipuka pembeni hadi mti ufike zaidi ya futi 10 kwani ndiyo yanafanya mbao kuwa na mabaka (vidonda)
   
 4. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  wakuu hii imekaa vizuri - swali langu nifahamisheni kwa mfano nimepanda eneo la hekari 1000 - na Miti yangu ipo tayari kwa uvunaji baada ya miaka kadhaa jee nitahitajika kupata kibali chochote cha serikali kabila ya uvunaji?

  Wasiwasi wangu wakuu unaweza kupanda heka 1000, miti ikawa tayari serikali wakakwambia huwezi kuvuna bila kuwa na kibali cha idara ya misitu - n.k

  nifahamisheni maana si mnajua ardhi ni mali ya serikali na unapopanda miti ni zao la muda mrefu. je unatakiwa kuwa na lease kabla ya kupanda?
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hakuna kibali, labda kama unapeleka nje ya nchi.

  Biashara ya miti imeshamiri sana Njombe, nguzo za umeme za Tanesco na TTCL zinatoka Njombe

  Nilitembelea wakulima wa miti wa Lupembe, Njombe. Miti imewakomboa sana, wanachofanya wanatafuta wafanyabiasha wa mbao mkulima anawaonyesha eneo la kuvuna miti, tajiri akiridhika na aina ya miti wanaandikiana mkataba wa kuvuna ekari moja au nusu ekari. Mara nyingi wakulima hawataki pesa taslimu, mnakuja Dar kuchangua lori mara nyingi wanataka scania au fuso idadi ya magari inategemea ukubwa wa shamba la miti.

  Ukianza kuvuna magari yake ndiyo yanabeba mbao zako na kuleta sokoni dar
   
 6. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu hata ukipanda mchicha kwa ukubwa wa shamba hilo hekta 1,000 lazima upate kibali. Maana ingine ya kibali ni kodi mkuu sio jambo geni.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  This is a very good thread, lakini naangalia pia je ni wapi mitiki inakua na ni wapi haistawi ndani ya tanzania?
   
 8. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sehemu nyingi inastawi.......ila zaidi kwenye mvua za kutosha, joto la wastani na udongo wenye kina kirefu. Mashamba makubwa ya Teak yapo Tanga (Longuza), Morogoro (Turiani, Ifakara etc). Kazi kwako.....ukipata kijitabu cha mbegu cha Tanzania Tree Seed Agency kimeorodhesha maeneo kwa ufasaha zaidi.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tanzania Tree Seed Agency watashiriki maonyesho ya sabasaba mwaka huu na watapatikana kwenye banda la Maliasili na utalii watakuja na aina mbali mbali za mbegu za miti kwa kuuza. Ni kipindi kizuri basi kuwaona na kupata taarifa za kina kuhusu aina mbalimbali za miti, zinastawi wapi, bei zake na masoko.

  Wataalamu wa kilimo wa chuo kikuu cha SUA, Morogoro nao watashiriki, wanakuwa na taarifa nyingi nzuri kupita maelezo kuhusu kilimo, ufugaji, uvuvi, masoko n.k. Kwa wale walioko Dar na mikoa ya jirani na umedhamiria kulima, hakikisha unakutana na hao wataalamu wetu.
   
 10. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  aha, basi wakati wa sabasaba itakuwa ni kuwatafuta hiyo Tree agency ili kupata maeelezo. lakini pia nimejaribu kupitia kwenye website yao naona wana maelezo mazuri ingawa yapo outdated (ni vema wakaboresha).
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Kama unataka kujishughulisha na misitu ni jambo jema, nakushauri nenda bonde la kilombero,huko kuna kila kitu yaani ardhi ya kutosha ambayo ni muafaka kwa mitiki,kuna kampuni kubwa sana iliyowekeza ktk mitiki, na siku za karibuni wataanza ujenzi wa kiwanda chao. Mimi nimefika huko kwa nia ya kujifunza. Unaweza kupata zaidi ukienda huko,kwa sababu utapata nadharia na vitendo. kama utapanda 3m x m3 basi utakuwa na miche kama 576 hivi kwa eka moja.

  Watu wengi husahau kufanya root pruning kabla ya kupanda miche shambani,hatua hii ni muhimu sana ili miche ipone kwa asilimia kubwa.Ni vizuri kutumia polythene tubes ktk kitalu chako. Ifakara na Ikwiriri unaweza kupata mbegu za kuokota ktk misitu ya watu.

  Unaweza kupata boriti nzuri baada ya miaka kumi na unaweza kupata mbao safi baada ya miaka 20 hivi.
  Soko la mitiki kwa sasa ni nje zaidi sio ndani,kwa hiyo ni vizuri kupanda kitaalamu ili usipate hasara wakati wa mavuno. Wakala wa serikali wa Mbegu si wakuaminika sana kwa sasa. Wameshindwa kutosheleza mahitaji ya soko. Mimi ni mdau wao.lakini nimekosa mbegu leo hii ninapoandika meseji hii.
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Jamaa wamelala mno,tangu wale jamaa toka Ulaya wajitoe kuhudumia vituo vya mbegu,hakuna kitu tena,hata umeme wanashindwa kulipia. Ni aibu kweli.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Unahitaji kibali kama miti ni ya asili,mitiki ni miti ya kigeni hapa kwetu. Taratibu za ushuru zipo lakini sio kibali cha kuvuna.
   
 14. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  hopefully wakala wa mbegu watashiriki maonyesho ya nane nane morogoro na dodoma....
  any data?
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Wanaweza,ila jamaa wamechoka vibaya,sijui nao wako ktk uchaguzi!!!!!. Hivi ninapoandika hata mbegu za pines hawana,eucalyptus saligna hawana kabisa, wakati ambapo hizo ndizo mbegu zinazoongoza kwa soko kwa sasa. Cyprus pia hawana,sasa hiyo hela ya kuandaa maonyesho watapata wapi wakati product ya kuuza hawana? Jamaa walivyo wa ajabu watakwenda ku-promoti mbegu ya Zimbabwe ile ya miaka nane na kugawa vipeperushi.

  Taarifa wanazo nyingi sana za kutoa,lakini vitendo haba na watakwambia wanasubiri budget. Mungu iokoe Tz.
   
 16. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu Morogoro mbegu wanauza kwa Kg kiasi gani?

  Nahitaji kama kila 45 ningependa kujua zitanigharimu kiasi gani.

   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Mimi nitakupa bei kwa kilo. Kg moja ya mtiki ni Tsh 6000/,sijui kama watakuwa wame-update,ila inatoa miche kati ya 1000 mpaka 1500. Miche ya mitiki inasumbua sana uotaji wake,unaweza ukawatika kilo nzima ukapata miche mia. Sasa inabidi ufuate maelekezo ya kitalaam sana.

  Siwezi kukuhakikishia kama utapata au utakosa,ila pines/mlingoti nina hakika hakuna kabisa. Pine iliyopo ni ile ya kutoka Zimbabwe ambayo huuzwa Tsh 500,000/ kwa kilo kwa sababu huvunwa baada ya miaka nane.

  Ukishindwa Morogoro,jaribu Lushoto na Kilombero. Kule kilombero ni private firm unaweza kupata kiasi hicho bila taabu.

  Nimekupa yale ninayofahamu,akiwepo mwenye taarifa zaidi atupe.
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ahsante Mkuu Malila,

  Nimekutumia e-mail kwenye e-mail yako ya yahoo kukuomba namba ya simu.

  Tutaongea zaidi.
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Tayari nimekujibu na nimekupa.
   
 20. M

  Malila JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Samahani wana jamvi, mbegu ya mitiki iko pale Morogoro kwa wakala wa serikali,nimeongea na ofisa wao kanihakikishia kuwa ipo ya kutosha. Kwa sasa bei ni Tsh 6500/ kwa kilo moja.

  Kwa wanaohitaji,kazi kwetu.
   
Loading...