Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Messages
284
Points
1,000
A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2016
284 1,000
Kila siku naona makala na thread zikizungumzia kilimo cha mitiki na jinsi inavyohitajika sana. Ila sijawahi kuona mtu akitoa kuhusu bei hasa ya mitiki ikishakuwa mikubwa iwe ni kwa mti mmoja mmoja au kwa eka ili kutuhamasisha kulima na pia kutufanya kufanya cost-profit analysis kabla ya kulima. Pia sionagi mtu akieleza ni wapi hasa soko la mitiki lipo au ni kampuni zipi hasa zinanunua mitiki.

Sio kwamba napinga kulima mitiki, ila inakuwa kama hakuna mtu mwenye uhakika hasa wa ni faida kiasi gani (hata kwa makadirio ya wastani, maana bei ni maelewano) mtu anaweza kupata baada yabkuwekeza kwa hiyo miaka 15-20.

Kama yupo mtu wa namna hii naomba atusaidie kutuelewesha zaid. Asante

Hate me at your own risk
Kaina, mawazo yako ni kama yangu.

Kuna jamaa yangu amelima mitiki heka 50 na. Nilimuuliza hayo maswali na alishindwa kujibu.

Sipingi kulima mitiki, ila nadhani ulimaji wake umekuwa exagorrated. Ni kama ukuzaji wa sungura. Poleni kusema haya.

Cut point niliyoiona, ni kwamba mitiki inakomaa baada ya miaka 25 na.... Kwa maana hiyo, hii investment sio yako tena, ni ya wanao.

Kwa maana hiyo, kulima mitiki ni excess wakati una mambo mengine ya kufanya. Maana yake hutategemea mitiki kuishi.
Haya mnataka bei za mtiki ni hizi hapa
Kuhusu soko: Nenda Turiani morogoro kuna Viwanda vitano vinauza nje hii miti. Pia nilisikia kilombero kipo kimoja

Nenda pia NMB wanakupa mkopo mzuri ukiwa na shamba la miti. Hapa ndio wajanja wengi wanatokea, wananunua kwa bei rahisi halafu wanachukulia mkopo mkubwa.

Ukitaka kuamini zaidi tembele wakala wa miti ofis zao zipo Morogoro njia ya kwenda Dodoma , nenda wakakupe ushuhuda.

Ushuhuda: kuna mtu kakataa 60M kwa ekari mbili zenye miti isiyozidi 800 ya mitiki ya miaka 8. Yupo morogoro sehemu inaitwa mngazi. Mwingine Turiani alitakataa 40M kwa nusu ekari ya mitiki. Hizi sio stori bali nimejionea

Taarifa mnazo sasa kimbieni shamba haraka msichelewe

NB: mitiki inaweza kuuzwa ukiwa na miaka 8, kwahiyo ondoeni fikira za kwamba watafaidi watoto.
 
From Sir With Love

From Sir With Love

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2010
Messages
1,782
Points
2,000
From Sir With Love

From Sir With Love

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2010
1,782 2,000
Haya mnataka bei za mtiki ni hizi hapa
Kuhusu soko: Nenda Turiani morogoro kuna Viwanda vitano vinauza nje hii miti. Pia nilisikia kilombero kipo kimoja

Nenda pia NMB wanakupa mkopo mzuri ukiwa na shamba la miti.

Ukitaka kuamini zaidi tembele wakala wa miti ofis zao zipo Morogoro njia ya kwenda Dodoma , nenda wakakupe ushuhuda.

Taarifa mnazo sasa kimbieni shamba

NB: mitiki inaweza kuuzwa ukiwa na miaka 8, kwahiyo ondoeni fikira za kwamba watafaidi watoto.
A2G, tunashukuru kwa taarifa. Japo mkali kama umelima mitiki lakini faida yake bado hujaiona.

Uliyosema ni yetu kuchunguza na kutafiti.
 
A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Messages
284
Points
1,000
A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2016
284 1,000
A2G, tunashukuru kwa taarifa. Japo mkali kama umelima mitiki lakini faida yake bado hujaiona.

Uliyosema ni yetu kuchunguza na kutafiti.
Mimi sijapanda ila Nipo kwenye maandalizi ya kupanda. Concern zenu zipo sahihi kuna stori nyingi kuhusu mitiki ambazo hazipo verified Ila Mimi stori zangu nilizo wapa nina uhakika nazo sababu kabla sijafanya maamuzi ya kupanda nilizunguka kwa watu walionayo.

Ukitaka kujua thamani ya mtiki nenda Turiani Morogoro, ukifika muulize dereva bodaboda yoyote hivi mitiki inalipa? Halafu ujue hapa uniambie. ndio utajua kuwa mjini watu tunapoteza muda.
 
From Sir With Love

From Sir With Love

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2010
Messages
1,782
Points
2,000
From Sir With Love

From Sir With Love

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2010
1,782 2,000
Mimi sijapansa ila Nipo kwenye maandalizi ya kupanda. Concern zenu zipo sahihi kuna stori nyingi kuhusu mitiki ambazo hazipo verified Ila Mimi stori zangu nilizo wapa nina uhakika nazo sababu kabla sijafanya maamuzi ya kupanda nilizunguka kwa watu walionayo.

Ukitaka kujua thamani ya mtiki nenda Turiani Morogoro, ukifika muulize dereva bodaboda yoyote hivi mitiki inalipa? Halafu ujue hapa uniambie. ndio utajua kuwa mjini watu tunapoteza muda.
A2G, asante kwa taarifa zaidi.

Jamaa yangu niliyemwelezea ambaye amelima mitiki, aliniambia faida kubwa ya mitiki aliyopanda ni kuhifadhi ardhi. Alisema in case serikali imeamua kuchukua ardhi yake kwa vyovyote vile, faida yake ni mitiki aliyopanda kama fidia.

Asante A2G.
 
A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Messages
284
Points
1,000
A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2016
284 1,000
A2G, asante kwa taarifa zaidi.

Jamaa yangu niliyemwelezea ambaye amelima mitiki, aliniambia faida kubwa ya mitiki aliyopanda ni kuhifadhi ardhi. Alisema in case serikali imeamua kuchukua ardhi yake kwa vyovyote vile, faida yake ni mitiki aliyopanda kama fidia.

Asante A2G.
Mpe pole na hongera sababu alikuwa hajui kuwa anapanda dhahabu bila kujua thamani. Huyo Jamaa ni tajiri mtarajiwa, kaa naye karibu .

Mwambie thamani ya mtiki ni kubwa kuliko hizo fikira zake
 
From Sir With Love

From Sir With Love

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2010
Messages
1,782
Points
2,000
From Sir With Love

From Sir With Love

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2010
1,782 2,000
Mpe pole na hongera sababu alikuwa hajui kuwa anapanda dhahabu bila kujua thamani. Huyo Jamaa ni tajiri mtarajiwa, kaa naye karibu .

Mwambie thamani ya mtiki ni kubwa kuliko hizo fikira zake
Sawa A2G, nitamwambia japo amepanda miti yake kibiti
 
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
3,757
Points
2,000
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
3,757 2,000
Nipo hapa kuwajibu wadau Kaina na From Sir With Love kuhusu kubeza upandaji wa mitiki na uhalisia wa thamani ya hii miti kwa sasa na baadae.

Binafsi ni mdau katika upandaji wa miti, nishanufaika nayo na ntaendelea kupanda kadri nafasi inapo ruhusu.

Upandaji wa miti ni utajiri na ni uwekezaji wa uhakika.

Licha ya kuipanda mitiki, najihusisha pia na uchakataji wa mbao na magogo ya mitiki kutoka kwa watu binafsi.
Huku Turiani mtaani tunanunua mti wa mtiki wenye miaka7-9wenye round kuanzia cm80-120(katikati ya mti) na urefu wa ft16-18,kwa sh30000.
Ukipeleka kiwandani miti ya ukubwa huu yenye kutoa magogo mawili ya ft8 kila mmoja, ikiwa mitano wanagrade kama cbm1 ambayo thamani yake ni sh400,000/=

Kwenye ekari1 ya mitiki kuna miti640.
Hivyo kama uta opt kuuza mitiki yako ya umri huu kiwandani utapata 640/5*400,000=51,200,000
Hii ni pesa ambayo angepata leo hii mtu aliyepanda ekari moja ya mitiki miaka7 iliyopita.

Kwenye ununuaji wa mitiki, kinacho angaliwa na outer round sio kukomaa kwa mti.
 
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
3,757
Points
2,000
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
3,757 2,000
Ndugu zangu kinacho tuongopesha kupanda mitiki ni ukosefu wa taarifa sahihi. Watu wanahofia kupanda miti kisa vitisho vya umri wa kukomaa.

Panda mitiki yako lau ekari10 sasa, ihudumie vizuri kwa miaka10. Weka samadi ya kutosha kwenye kila shina ili inenepe haraka make unene ndiyo soko lenyewe! dhibiti uvamizi wa mifugo shambani ili ardhi iwe laini mizizi iweze kupenya kwa wepesi kuusaidia mti upate chakula chake kwa wingi. Fanya prunning na thinning kitaalam na kwa muda muafaka.

Kadri unavyo hudumia vizuri ndivyo miti itakimbia katika ukuaji wake.

Ndani ya mtibwa teak, ipo mitiki mirefu na minene yenye kutoa cbm2. Hii inamaanisha kwamba mti moja una thamani ya sh800,000+ ndani ya Tanzania.
Soko kuu la teak wood lipo barani Asia ndiyo maana wanunuzi wakubwa ni wahindi.
Mtaani hapa Turiani, piece moja ya ubao wa mtiki yenye vipimo vya ft7ur*1'unene*10'upana ni sh10,000/=
Fikiria thamani ya mtiki miaka10 ijayo itakuwaje?
Nakusihi kapande miti kwa ustawi wa kesho yako. 10-15yrs ni michache sana kwa mtafutaji
 
A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Messages
284
Points
1,000
A2G

A2G

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2016
284 1,000
Nipo hapa kuwajibu wadau Kaina na From Sir With Love kuhusu kubeza upandaji wa mitiki na uhalisia wa thamani ya hii miti kwa sasa na baadae.

Binafsi ni mdau katika upandaji wa miti, nishanufaika nayo na ntaendelea kupanda kadri nafasi inapo ruhusu.

Upandaji wa miti ni utajiri na ni uwekezaji wa uhakika.

Licha ya kuipanda mitiki, najihusisha pia na uchakataji wa mbao na magogo ya mitiki kutoka kwa watu binafsi.
Huku Turiani mtaani tunanunua mti wa mtiki wenye miaka7-9wenye round kuanzia cm80-120(katikati ya mti) na urefu wa ft16-18,kwa sh30000.
Ukipeleka kiwandani miti ya ukubwa huu yenye kutoa magogo mawili ya ft8 kila mmoja, ikiwa mitano wanagrade kama cbm1 ambayo thamani yake ni sh400,000/=

Kwenye ekari1 ya mitiki kuna miti640.
Hivyo kama uta opt kuuza mitiki yako ya umri huu kiwandani utapata 640/5*400,000=51,200,000
Hii ni pesa ambayo angepata leo hii mtu aliyepanda ekari moja ya mitiki miaka7 iliyopita.

Kwenye ununuaji wa mitiki, kinacho angaliwa na outer round sio kukomaa kwa mti.
1. Miti 640 kwa ekari mbona Kama michache mkuu? Kuna Mdau aliniambia ekari unaweza kupanda mpaka miti 1200 ili Kama kuna ambayo itakufa utaishia na miti 800 mpaka 1000. Kwa uzoefu wako hili likoje?

2. Nilishauriwa kupanda mitiki kwa kuchanganya na mazao Kama mahindi au arizeti inasemakana inasaidia kuufanya mti ukue fasta sababu utakuwa unashindania mwanga na hayo mazao. Embu tia neno kwenye hili pia
 
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
3,757
Points
2,000
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
3,757 2,000
Mkuu A2G taarifa ulizo nazo si sahihi.
Required spacing ya upandaji mitiki ni 2.5m*2.5m. Ekari moja ina sqm4000, hii inamaanisha kwamba content ya ekari moja ni miti 640.
Na hii idadi utatakiwa kuipunguza(thinning) kadri umri na unene wa miti utakavyo kuwa unaongezeka.

Pia haishauriwi kuchanganya mitiki na alizeti kwenye eneo moja. Mimea yote hii ni heavy feeder, inatumia maji mengi sana na mbaya zaidi alizeti inapandwa mwishoni mwa msimu wa mvua wakati huo tayari mitiki itakuwa imepandwa, kitakacho tokea ni scrumble ya chakula na kwakua mtiki una tabia ya kufyonza na kuhifadhi maji mengi, matokeo yake atakae umia hapo ni mtiki make maji yote aliyojikusanyia kujihami na kiangazi, yatatumiwa na alizeti ambaye life span yake ni fupi.
Katika mnyukano huo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mavuno mabovu kwenye alizeti na pia ukaishia kuathiri mitiki make yenyewe itaendelea kuishi mpaka msimu mwingine wa kilimo.

Unaweza kuchanganya na mahindi sio mbaya sana japo mimi siafiki hilo kwa usalama wa miti kwenye palizi.
 
Nimekusoma mkuu.

Kuna athari gani kama utapanda zaidi ya miti 640 kwenye ekari? Mfano Mimi nilipanga kuweka spacing ya 2m * 2m ili nipande miche 1200 kwenye ekari ambayo najua hata nikija kuipunguza itabaki si chini ya miti 800.

Kuna athari zozote hapo?
 
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
3,757
Points
2,000
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
3,757 2,000
Spacing hiyo italeta idadi hii 4000/(2*2)=1000

Ukipanda hivi, miti itakimbizana kuutafuta mwanga wa jua. Itarefuka haraka sana ktk hali ya udhoofu hivyo haishauriwi kuiprun haraka haraka vinginevyo baadhi itapinda(hasa ile ya katikati) na itakubidi uipunguze mapema kuliko muda unao takiwa make itakuwa imebanana sana kiasi cha kuzuia kunenepa.

Suala la thinning kwenye miti ni mhimu na lazima vinginevyo utajikuta unasubiri miaka 40 ili inenepe ktk ubora wenye faida.

Kitaalam zaidi ikiwa miti itadumu hadi miaka zaidi ya 20 kwenye ekari moja inatakiwa ipungue mpaka miti300 tu, hapo itanenepa zaidi na kuna uwezekano wa miti kuwa bora zaidi na thamani yake kwenye soko itakuwa juu vibaya mno! usishangae mwanao akaja kuuza mti mmoja kwa thamani ya sh 2000,000/=

Huko bara Asia kuna mtiki mmoja uliuzwa zaidi ya $5,000/=

Pandeni miti, jifanye kama hujui, pambana na ustawi wa kesho yako mkuu!!
Kuna jamaa yangu huko njombe anaitwa Mbilinyi alipanda mamia ya maekari ya miti huko mkoani njombe, leo ana miaka15 yupo CA
 
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
3,757
Points
2,000
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
3,757 2,000

2 years old teak tree

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeona kazi nzuri mkuu, hongera sana kwa uthubutu na utendaji wako kwenye uwekezaji huu!

Kwa hapo ulipo mtiki hauwezi kufa tena. Endelea kuuhudumia kwa jicho angavu, panapohitajika kuweka mbolea weka ili ikimbie kukua. Itengenezee fire lanes kuzuia majanga ya moto.
Uzuri ni kwamba huko ukanda wenu, hakuna changamoto kubwa kutoka kwa wafugaji holela na raia wasio na uelewa wa thamani ya miti kama jinsi ilivyo huku kwetu. Halafu pia upandaji wa thamani ya ardhi huko chanika, haina mfanano na huku maporini.

Pambana katika matunzo, unamiriki utajiri mkubwa kuliko wengi wadhaniavyo.
 
V

viking

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
1,462
Points
1,500
V

viking

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
1,462 1,500
Mkuu mbegu ninazo mimi. Weka oda yako nikuandalie mzigo ambao utaupata kwa haraka na wepesi kulingana na shehena utakayo.
Karibu sana mkuu!
Nina shida na mbegu za mitiki,tafadhali tuwasiliane
 
Powder

Powder

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2016
Messages
3,593
Points
2,000
Powder

Powder

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2016
3,593 2,000
Kuna kipindi nilisikia Serikali ilizuia kuuza Magogo ya huu Mti kwa watu walokua wanauza nje!
Je! Kwa sasa imeruhusu?
 
de pedezyee

de pedezyee

Member
Joined
Jun 21, 2015
Messages
81
Points
225
de pedezyee

de pedezyee

Member
Joined Jun 21, 2015
81 225
Kama unahitaji miche wasiliana nasi sasa.
Gharama za miche ni shilingi 400@
Tunapatikana Boko -Timiza Kibaha.
Usafiri ni bure hadi mkoa husika ukichukua kuanzia miche 500.
Call/text/WhatsApp
0766006128
0655715184
0783579456

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,336,206
Members 512,562
Posts 32,530,544
Top