Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Jamani bado hatujapata ufafanuzi mzuri wa kilimo cha mihogo.hatujajua kwa heka Moja unaweza kupanda kwa kiasi gani na mavuno yake yanakuaje.anayejua basi atusaidie ili tuanze maandalizi

Pitia post zote, kuna moja imegusia kidogo kiasi unachoweza vuna kwa ekali kutokana na aina ya mbegu
 
KILIMO BORA CHA MIHOGO

Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

TEKNOLOJIA ZILIZOPO
Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
Naliendele
Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

Kiroba
Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

Mbinu bora za kilimo cha muhogo
Uandaaji wa shamba
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
  • Kufyeka shamba
  • Kung’a na kuchoma visiki
  • Kulima na kutengeneza matuta
· Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.
· Upanadaji
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
  • Kulaza ardhini (Horizontal)
  • Kusimamisha wima (Vertcal)
  • Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.

· Palizi:
  • Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
  • Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
  • Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
  • Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

· Uvunaji:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

· Usindikaji bora
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
  • Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
  • Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
  • Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

Njia bora za usindikaji
- Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
  • Kwa kutumia mashine aina ya chipper
  • Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

Matumizi ya Muhogo
  • Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
  • Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
  • Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.
 
Wakuu,

Kutokana na uhitaji wa kuwepo mjadala endelevu na wa tija kwa wajasiriamali, tumeona ni vema tukaweka hii thread kwa maslahi ya wengi.

Tunashauri Mjadala huu ujikitae kwenye maeneo yafuatayo:

1. Aina za mihogo na maeneo inakostawi vizuri
2. Misimu ambayo mihogo inapandwa ni miezi ipi? Inaweza kupandwa misimu yote ya mwaka?
3. Mihogo inashambuliwa na magonjwa yapi? Zipi mbinu za kukabiliana na maradhi hayo?
4. Mihogo inachukua muda gani tangu kupandwa hadi kuvunwa?
5. Hekari moja inaweza kutoa magunia mangapi ya mihogo?
6. Masoko ya mihogo na bidhaa zake ndani na nje ya nchi yapoje?

Asante
nahitaji mbegu za mpapai nitapata wapi zinakouzwa?
 
ZAO LA MUHOGO

Utangulizi
Mihogo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kigoma, Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuna, Tanga, Morogoro, Mbeya, na Shinyanga. Muhogo una kiwango kikubwa cha wanga ukilinganisha na nafaka (zaidi ya asilimia 40 kuliko mchele, na zaidi ya asilimia 25 kuliko mahindi). Majani yake hutumika kama mboga na yana virutubishi muhimu hususan vitamini B na protini.
Uzalishaji wake ni wastani wa tani 1,292,000 kwa mwaka. Ili kupata mazao mengi na bora ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora cha mihogo hasa zifuatazo:

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Uzalishaji
Kuchagua aina ya mbegu

  • Chagua mbegu kufuatana na mahitaji ya soko, zilizo safi zinazostahimili magonjwa, wadudu waharibifu na zenye uwezo wa kutoa mazao mengi na bora.
Palizi
  • Palilia ili kupunguza ushindani wa virutubishi kati ya mmea na magugu.
  • Palilia na kupandishia udongo kwenye mashina.
  • Palizi ifanyike mara kwa mara mpaka mihogo inapokomaa.
Kudhibiti magonjwa na wadudu
Muhogo hushambuliwa na wadudu waharibifu kama vidung’ata, vidugamba, mchwa na magonjwa kama batobato na ugonjwa wa michirizi ya kikahawia. Visumbufu hawa wanaweza kusababisha upotevu wa mazao kwa zaidi ya asilimia 90. Hivyo ni muhimu kukagua shamba mara kwa mara ili kuona kama kuna mashambulizi na kuchukua tahadhari mapema.

Maandalizi kabla ya kuvuna
Kukagua shamba

  • Kagua shamba ili kuhakikisha kama muhogo umekomaa. Kwa kawaida muhogo hukomaa katika kipindi cha miezi 9 hadi 24 tangu kupanda kutegemea aina na hali ya hewa. Wakati huo muhogo huwa na unyevu wa asilimia 60 na wanga asilimia 35.
Dalili za muhogo uliokomaa
  • Udongo unaozunguka shina hupasuka.
  • Mti wa muhogo huonekana kupevuka.
  • Muhogo uliokomaa ni mnene na ukiutafuna utahisi wanga mwingi na maji kidogo.
Kuandaa vifaa vya kuvunia, kubeba, vyombo vya usafiri, na vifungashio

Vifaa vya kuvunia na kubeba

  • Jembe, Panga, Vikapu, Matenga, na Magunia
Vifaa vya kufungashia
  • Maboksi ya mbao/plastiki, viroba, Matenga
Vyombo vya usafiri
  • Baiskeli, Matoroli, Mikokoteni, Magari na matela ya matrekta.
Kuvuna
Ni muhimu kuvuna mapema ili kupunguza uharibifu unaoweza kusababishwa na mashambulizi ya magonjwa na wadudu waharibifu. Kabla ya kuvuna matawi yote yakatwe ili kurahisisha uvunaji.

Njia ya kuvuna muhogo
Chimbua shina la muhogo kwa kutumia jembe na ng’oa muhogo wote kutoka ardhini. Tenganisha muhogo na shina kwa kutumia panga kali.

Utayarishaji, Hifadhi na Usindikaji wa Mazao ya Mizizi baada ya Kuvuna

Tahadhari

Epuka kukata muhogo wakati wa kuvuna kwani mihogo iliyokatwa au kuwa na majeraha huharibika mapema, kutokana na kuingiwa kwa urahisi na vimelea vya magonjwa.

Kuchambua Na Kusafisha

Kuchambua

Lengo la kuchambua ni kuondoa mihogo isiyofaa, iliyooza na iliyokatwa vibaya na kuharibika.
  • Mihogo iliyooza isitumike kwa chakula bali ifukiwe.
  • Mihogo iliyokatwa au yenye michubuko itumike kwa chakula mapema iwezekanavyo au ioshwe vizuri na isindikwe mara moja.
  • Mihogo iliyodumaa itumike kwa chakula cha mifugo.
Kusafisha na kuimarisha maganda

Kusafisha

Mihogo iliyovunwa huoshwa mara tu baada ya kuvuna ili kuondoa udongo na uchafu mwingine. Mihogo ambayo haikuoshwa vizuri hupunguza ubora wakati wa kukausha na kusindika. Mihogo huoshwa kwa maji na kurudiwa hadi maji yanapokuwa safi na kuona kuwa mihogo imetakata.

Kwa maelezo au mazao mengine unaweza tembelea
 
Nijuavyo Muhongo ni heavy feeder sasa unaporuka kipengele cha mbolea naamini watu watapotoshwa. Mbolea ipi inafaa, kwa kiwango gani na wakati gani?
 
Chacha nami naomba kujuzwa zaidi na sanasana ni utafiti uliofanywa Italy na pia kama kunamtu anajua matumizi ya Starch itokanayo na mihogo.
Japo mimi sio Chacha, tuna mradi pale Rufiji kwenye zao la Muhogo uko chini ofisi ya waziri mkuu, tunawajengea wakulima uwezo katika uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko jina la mradi kwa kizungu wanaita Marketing Infrastructure Value Addition and Rural Finance Program (MIVARF).

Kuna kata tatu tunafanya nazo kazi ambazo ni Bungu, Dimani na Ruaruke. Pale Bungu kuna viwanda viwili. Kikubwa kinajihusisha na utengenezaji wa starch kwa matumizi ya hospitali kwa ubia na watu wa Marekani na kidogo ni kuandaa bidhaa za chakula hasa unga. Katika tani 60 za muhogo mbichi mchakataji anaweza kupata wastani wa tani 16 za starch. Matumizi ya Muhogo kwasasa ni Kuzalisha kachori, unga, chips, kuni, mboga, maandazi na mikate. Kwa upande wa kiwanda wanatengeneza starch pia maganda ya muhogo unaochakatwa yanatarajiwa kutengeneza umeme kwa matumizi ya kiwanda na mwingine kuuza Tanesco.

Masoko moja ni Bungu na Kibiti kwa wakulima wadogo maarufu chini ya muembe pia kwenye viwanda tajwa. Lakini kuna masoko ya Dar es Salaam viwandani kwa Mama Mwaipopo food products na Power Food kawe. Mahitaji ya muhogo mbichi pia yapo masoko ya Kariakoo, Tandika na Kawe ambapo wakulima kwa vikundi wamesaini mikataba na wanunuzi mwaka huu 2016.

Huduma za mikopo kwa wakulima wa muhogo kwa kiasi kidogo hasa za uongezaji thamani zinapatikana benki ya wananchi wa Dar es Salaam (DCB) kwa mikopo ya vikundi. Juhudi zinafanyika wapate mikopo pia kupitia PASS. Usafiri ni rahisi kutoa muhogo ukanda huo kutokana na magari mengi yanayotoka Mtwara na Lindi kupeleka mizigo kutokuwa na mizigo yakupeleka Dar. Nikutakie kila la kheri.
 
KAMPUNI YA FJS AFRICAN STARCH DEVELOPMENT CO. LTD imeishaanzisha kiwanda kikubwa cha kusindika mihogo katika wilaya ya Rufiji.

Kampuni hii kwa kutumia mkopo kutoka TIB, iliamua kuwasaidia wakulima wa Rufiji kwa kuanzisha kiwanda cha kuchakata na kusindika mihogo katika viwangi vya juu, kwa ajili ya kuongeza thamani zao la mihogo na hivyo kuliwezesha kupata soko zuri hapa nchini na ziadia kuuza katika soko la nje.

Kampuni hii imeeleza mipango yake ya kuwa, wanakusudia kuwasaidia wakulima wote wa wilaya hiyo. Shukrani kwako aliyeweka maada hii ya mihogo hapa. Joseph Sekiku 0754605682
 
Hii Thread ni ya toka 2011, ila nmeipenda sana, nmepata vingi, maana na mimi nafikiria kuanzisha shamba hilo hilo mitaa ya mkuranga, sehem baada ya Chanika. kichanga ni kizuri, ila sina uhakika kuhus Mvua. Shukrani wote kwa huu uzi.
 
Japo mimi sio Chacha, tuna mradi pale Rufiji kwenye zao la Muhogo uko chini ofisi ya waziri mkuu, tunawajengea wakulima uwezo katika uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko jina la mradi kwa kizungu wanaita Marketing Infrastructure Value Addition and Rural Finance Program (MIVARF).

Kuna kata tatu tunafanya nazo kazi ambazo ni Bungu, Dimani na Ruaruke. Pale Bungu kuna viwanda viwili. Kikubwa kinajihusisha na utengenezaji wa starch kwa matumizi ya hospitali kwa ubia na watu wa Marekani na kidogo ni kuandaa bidhaa za chakula hasa unga. Katika tani 60 za muhogo mbichi mchakataji anaweza kupata wastani wa tani 16 za starch. Matumizi ya Muhogo kwasasa ni Kuzalisha kachori, unga, chips, kuni, mboga, maandazi na mikate. Kwa upande wa kiwanda wanatengeneza starch pia maganda ya muhogo unaochakatwa yanatarajiwa kutengeneza umeme kwa matumizi ya kiwanda na mwingine kuuza Tanesco.

Masoko moja ni Bungu na Kibiti kwa wakulima wadogo maarufu chini ya muembe pia kwenye viwanda tajwa. Lakini kuna masoko ya Dar es Salaam viwandani kwa Mama Mwaipopo food products na Power Food kawe. Mahitaji ya muhogo mbichi pia yapo masoko ya Kariakoo, Tandika na Kawe ambapo wakulima kwa vikundi wamesaini mikataba na wanunuzi mwaka huu 2016.

Huduma za mikopo kwa wakulima wa muhogo kwa kiasi kidogo hasa za uongezaji thamani zinapatikana benki ya wananchi wa Dar es Salaam (DCB) kwa mikopo ya vikundi. Juhudi zinafanyika wapate mikopo pia kupitia PASS. Usafiri ni rahisi kutoa muhogo ukanda huo kutokana na magari mengi yanayotoka Mtwara na Lindi kupeleka mizigo kutokuwa na mizigo yakupeleka Dar. Nikutakie kila la kheri.
Mkuu naomba uchungulie PM yako
 
Nimekujibu whatsapp

Sorry jamaa yangu, huu mradi wa muhogo umebase huko Rufiji tuu au hata mimi nikiamua kulima huko Newala kwa kufuata aina (ya muhogo mnaohitaji) na ulimaji/ubora mnaouhitaji mnanunua?
 
Sorry jamaa yangu, huu mradi wa muhogo umebase huko Rufiji tuu au hata mimi nikiamua kulima huko Newala kwa kufuata aina (ya muhogo mnaohitaji) na ulimaji/ubora mnaouhitaji mnanunua??
Huu mradi uko nchi zima halmashauri zilishindanishwa kwakuandika maandiko tofauti tofauti. Kwa mkoa wa Mtwara zilishinda wilaya mbili za Tandahimba na Nanyumbu kwenye zao la Korosho.

Hivyo mradi unatekelezwa kwa zao hilo. Muhogo ni kwa Mkuranga na Rufiji ambapo sisi tulipewa jukumu lakuwajengea uwezo wakulima wa Rufiji na tunaona mafanikio makubwa. Kimsingi kuna mabadiliko na wakulima sasa wamehamasika tofauti na awali walikuwa wanatugomea kutokana na kuwa na picha mbaya ya miradi ya maendeleo.
 
Huu mradi uko nchi zima halmashauri zilishindanishwa kwakuandika maandiko tofauti tofauti. Kwa mkoa wa Mtwara zilishinda wilaya mbili za Tandahimba na Nanyumbu kwenye zao la Korosho. Hivyo mradi unatekelezwa kwa zao hilo. Muhogo ni kwa Mkuranga na Rufiji ambapo sisi tulipewa jukumu lakuwajengea uwezo wakulima wa Rufiji na tunaona mafanikio makubwa. Kimsingi kuna mabadiliko na wakulima sasa wamehamasika tofauti na awali walikuwa wanatugomea kutokana na kuwa na picha mbaya ya miradi ya maendeleo.
Ningependa nijifunze kuhusu huu muhogo na soko lake, nitakutafuta PM ndugu. Nashangaa ndugu zangu mihogo wanalima miaka miwili halafu inawadodea hata soko haina.
 
Ninaona kuna haja ya kufanya "stakeholders mapping "kwenye zao hili la Muhongo ili kuweza kuboresha value chain ya zao hili na kuwezesha stakeholders kupunguza vikwazo wanavyokabiliana navyo wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.
 
Tembelea library SNAL na ofisi za MIVARF Arusha utapata majibu, unless uwe unataka kurudia.
 
Tembelea library SNAL na ofisi za MIVARF Arusha utapata majibu, unless uwe unataka kurudia.
Asante kwa taarifa...! Ila nadhani review ya hii kitu ni muhimu maama wadau wanabadilika kutokana na mazingira na nyakati.
 
Back
Top Bottom