Kilimo cha matikiti ni anguko la wengi mwaka huu

Kilimo cha matikiti ni anguko la wengi mwaka huu

Kimeshaanza kusikika mkuu kilio cha ufugaji sasa hivi Tray ya mayai 5000, tokea 8000
Na bado hayana soko

Kweli kabisa kwa sasa mayai bei ni tatizo tuna kuku wa mayai zaidi ya 10,000 mayai yapo ya kutosha wateja sasa nitatizo
 
Mkuu kwani kuiga kitu kizuri ni vibaya? Wakati mwingine tunaiga kwa kuwa pia mazingira tunayotokea zao hilo tuliloiga ndio linakubali zaidi. Ama unataka watu waige ujambazi maana hata wenye unalipa.
Nina uhakika hujaelewa nachokiongeaa..
 
kwa sie wafuga nguruwe neema tunanunua nyanya tunawapa nguruwe, lakini inasikitisha sana.
 
ni muda sasa wa kuanza kufikiri kuhusu viwanda vya usindikaji na masoko nje ya nchi ya bidhaa zetu...
nimelima matikiti natoa mwezi huu mwishoni,ila siwazi tena kulima matikiti..nawaza kulima zao litakalokuwa adimu sokoni ili nilime...!!!
Uko Wapi?
 
Kweli kabisa kwa sasa mayai bei ni tatizo tuna kuku wa mayai zaidi ya 10,000 mayai yapo ya kutosha wateja sasa nitatizo
Mie,nilikuwa natafuta wateja ktk benki na taasisi za umma zenye kaharufu ka pesa!mathalani nilikuwa nauza ktk benki za nmb na crdb!pia waweza ongea na watu binafsi wenye uwezo uwauzie!
 
Mie matunda mpaka niandikiwe na daktari... Kuwafuta machozi wakulima, leo nikale tikiti ili tuyapunguze huku sokoni.
 
Kimeshaanza kusikika mkuu kilio cha ufugaji sasa hivi Tray ya mayai 5000, tokea 8000
Na bado hayana soko
Wewe unaongea ukweli. Kwamba bidhaa zimeshuka. Inabidi kuangalia na upande wa pili nao washushe bei ya malighafi
 
Naomba ushauri wadau Nina shamba la heka 5 maeneo ya MKATA naomba ushauri kwa wataalam wa kilimo na ufugaji nifanye nini Asante sana
 
hii sera ya viwanda itatuua ,jamaa uongozi unamshinda,tz tunanuka umaskini wa kutisha halafu unahubiri viwanda badala ya kuboresha kilimo kwa kututafutia masoko nje ya nchi ,haya manyanya tuyapeleka wapi sasa
 
Wanabody nimekuja kutoa rai yangu wale wenzangu waliojitokeza kulima matikiti mwaka huu.

Hali ilivyo mpaka sasa si shwari kwa kuwa soko linatatiza sana kwa maana watu walioingia kwenye kilimo hiki ni wengi sana na matokeo yake kupelekea matikiti kuwa mengi sana sokoni na mitaani na mazao mengine kuadimika.

Hii inaleta kilio hapo badae kwani kwa sasa hata madalali ndio wameongeza ukali wa manunuzi.

Wananunua tikiti kubwa kwa 1500, au 1000.

Naomba nitoe rai ya kuwa makini na watu wengine ambao bado hawajalima wajaribu kufanya simple research kwenye kilimo kwamba ni nini kinahitajika.
Haha mimi ni mmojawao ntapokea tu matokeo
 
Hii kitu its all about timing and target.
Mfano
Mwaka huu hasa mwez huu n muda mzur sana wa kulima nyanya na matikit sabb wakulima wengi hawatarud shamba kwa kukosa mtaji au kukata tamaa na watashift kwenye mahind na maharagwe ambayo saiv sikon n machache.
Wakirud hapa watalia the same.
Wew utakuja na kile wakichokiacha ukiwa sokon mpo wachache
 
Mdololo wa uchumi umeadhiria kiac fulan
Maana mimi mwaka uu nimenunua ufuta sijapAta faida sokoni
Nikanunua mbaazi kwa 1000
Alafu nikakuta bei ya soko ni900
So kuna wingi zto kiac
Pole sana mdau,ajabu mwaka huu mavuno hafifu ya ufuta halaf bei iko chini,ila si tumeambiwa India ma Japan wamahitaj hayo mazao hebu tembelea wizara ya Biashara ukaulizie procedures
 
Hii kitu its all about timing and target.
Mfano
Mwaka huu hasa mwez huu n muda mzur sana wa kulima nyanya na matikit sabb wakulima wengi hawatarud shamba kwa kukosa mtaji au kukata tamaa na watashift kwenye mahind na maharagwe ambayo saiv sikon n machache.
Wakirud hapa watalia the same.
Wew utakuja na kile wakichokiacha ukiwa sokon mpo wachache
Upo sahihi ndugu, ila changamoto ya huu msimu ni upatikanaji wa maji tofauti na msimu uliopita wengi walitegemea mvua. Kwa wanye uwezo wa kulima kilimo cha umwagiliaji huu msimu watapiga hela ya kutosha.
 
Exactly.
Na siku zote kilimo cha kutegemea mvua ni cha kupata chakula na sio cha biashara
 
Back
Top Bottom