Kilimo cha matikiti ni anguko la wengi mwaka huu

Kilimo cha matikiti ni anguko la wengi mwaka huu

popo1986

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2014
Posts
1,120
Reaction score
373
Wanabody nimekuja kutoa rai yangu wale wenzangu waliojitokeza kulima matikiti mwaka huu.

Hali ilivyo mpaka sasa si shwari kwa kuwa soko linatatiza sana kwa maana watu walioingia kwenye kilimo hiki ni wengi sana na matokeo yake kupelekea matikiti kuwa mengi sana sokoni na mitaani na mazao mengine kuadimika.

Hii inaleta kilio hapo badae kwani kwa sasa hata madalali ndio wameongeza ukali wa manunuzi.

Wananunua tikiti kubwa kwa 1500, au 1000.

Naomba nitoe rai ya kuwa makini na watu wengine ambao bado hawajalima wajaribu kufanya simple research kwenye kilimo kwamba ni nini kinahitajika.
 
Lima suger baby kaka f1 watu wqmeikimbilia nakusahau hyo nyingne ambapo saaasa ni adim nq uhitaj ni mkubwa
 
hili anguko la bei na wingi wa chakula ni mdororo wa uchumi unaosababishwa na mzunguko mdogo wa fedha na ni dhahiri biashara nyingi zipo chini mauzo yamekuwa madogo ..... hebu fikiri hapa Dar mchele safi kabisa unauzwa Tsh. 1,200/- per kg sawa na bei ya unga wa sembe hii imepelekea hata unga wa sembe kutokununulika
 
Hii bei ni DSM soko gani Mkuu tujuzane, mimi huku Mbezi bado nauziwa 1800 kwa Kg!
 
hili anguko la bei na wingi wa chakula ni mdororo wa uchumi unaosababishwa na mzunguko mdogo wa fedha na ni dhahiri biashara nyingi zipo chini mauzo yamekuwa madogo ..... hebu fikiri hapa Dar mchele safi kabisa unauzwa Tsh. 1,200/- per kg sawa na bei ya unga wa sembe hii imepelekea hata unga wa sembe kutokununulika
Iyo bei ni wapo mkuu?
 
Dah.
Poleni sana aisee, nafikiri kilichochangia pia ni mdororo wa uchumi nchini maana hata kwenye nyanya nako ndo moja kubwa ya Tsh 15,000 inauzwa sasa kwa Tshs 700.

Ni mambo ya aibu kwa kweli.
 
Mi nayaona haya kama fursa ya kutumia kichwa sasa maana baada ya hii crisis naamini kutakuja recovery na kisha boom au sio wakuu...
 
Hali ni tete kwa matikitimaji ushauri kwa wakulima wanaoanza wajaribu kuangalia vitu hadimu sokoni ndo wavilime maana kwenye masoko mbalimbali hali sio shwari
 
Tatizo ni dhana ya Kilimo cha whatsapp, mara nyingi mkulima anakosa taarifa sahihi baada ya kuhamasishwa kufanya kilimo kupitia SMS za mitandao ya kijamii. Mbaya zaidi taarifa hizi hutumiwa kama mwongozo wa kufanya kilimo bila mkulima kufanya utafiti sahihi wa masoko na gharama alisi za uendeshaji. Kilimo cha whatsapp...
 
Dah.
Poleni sana aisee, nafikiri kilichochangia pia ni mdororo wa uchumi nchini maana hata kwenye nyanya nako ndo moja kubwa ya Tsh 15,000 inauzwa sasa kwa Tshs 700.

Ni mambo ya aibu kwa kweli.
Huko kwenye nyanya ni kilio cha wengi yani mwaka huu tumecheza pata potea
 
Nyanya+tikiti zimeshuka bei,Mbaazi pia hata Tangawizi pia bidhaa imekuwa nyingi ila wateja sasa ndo mtihani,halafu serikali jana inasema ukitaka uuze nje ukachukue kibali ambacho kwa wakulima wa kawaida kukipata ni shida
 
Back
Top Bottom