Kilimanjaro Express Kuanza Safari za Usiku

Ingependeza waanze saa 12 jioni na safari nyingine saa 2 usiku.
Miaka ya 80 kwa Jiji la Arusha kulikuwa na mabasi(ordinary) yalikuwa yanatoka saa 10 jioni na yale ya kifahali(luxury) saa mbili usiku kwenda Dar kupitia Moshi.
 
Sasa naona Ile mbinu ya kuua safari za train ya Moshi to dar to Moshi imeanza. TRC mpoo? Maza upo? Pole Pole sema neno train yetu itapata wapi wateja wa usiku?
TRC tutawaletea msanii wa bongo fleva kila safari msijali tumejipanga kweli kweli
 
Kuna hii ruti ya dar mbeya nayo ni muhimu sana kuwe na basi za usiku
Ni sawa ila hiyo njia bwana inawatemi wengi sana, Doma mpaka Mikumi hatari, Mikumi,iyovi,mtego wa simba mpaka ruaha mbuyuni hatari.
Ifunda, mafinga sao hill msituni mpaka mbala maziwa hatari, igurusi, mlima myoka mpaka uyole hatari.
 
Sasa naona Ile mbinu ya kuua safari za train ya Moshi to dar to Moshi imeanza. TRC mpoo? Maza upo? Pole Pole sema neno train yetu itapata wapi wateja wa usiku?
Innovations is life,
Waache wake wasubiri SGR,
Sie abiria wa kawaida hatupendi vitu vzr, wasuburi Mechi ya Simba na Yanga Kigoma ndo wenye kujua vitu vzr. (Burudani, vyakula vzr na vinywaji)
 
Tatizo ni kibali tu wala siyo sifa kwa Kilimanjaro, wale kapricon waliomba na kupotezewa so ni muda tu utaona kampuni zaidi ya moja zikiwa barabarani usiku.

Issue ya train kukosa abilia wala siamini, wapo wengi na hata mimi naweza kutumia usafiri huo ku_manage na kusave vitu vingi.
 
Ninavyowajua madereva wa mabus yan akiruhusiwa usiku itakua ni full kuvunja sheria za barabarani yani chuma inakaa kulia imewasha indicator hadi chuga
 
Unaondoka saa 2 usiku saa mbili asubuhi unafika. Unafanya shughuli zako jioni unageuza tena.

Wenye Guest house watapata tabu sana. Usingizi tutamalizia kwenye basi.
Siku hizi mimi huwa naenda dar na kurudi Ar, japo naunga safari. Nachukua gari za Tanga saa 18:00 hadi Segera, hapo nasubiria gari za Mbeya ...naingia Moshi 05.00.
 
Back
Top Bottom