JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Inaelezwa kuwa hatua hiyo imekuja baada kijana wa bibi huyo kutofanyia kazi amri mahakama, ambayo ilimtaka kila mwezi atoe shilingi elfu 90,000 za matumizi kwa mtalaka wake ambaye aliondoka na watoto watatu baada ya ndoa yao kuvunjika.
Aidha, Mwanaume anayedaiwa kushindwa kutoa fedha hizo kila mwezi aitwae Evarest Mrosso, amesema kuwa alishindwa kutii amri ya mahakama kutokana na hali ngumu aliyobakia nayo baada ya ndoa hiyo kuvunjika, na kisha mwanamke huyo kuondoka na mali zote pamoja na fedha za mauzo ya eneo walilokuwa wanaishi, ambazo zilidaiwa kuwa zinakwenda kutumika kuwatunzia watoto hao.
============================
Siku moja baada ya GADI TV kurusha habari inayomuhusu bibi mwenye umri wa miaka 66, aitwae Julia Albin ambaye ni mkazi wa Tarafa ya Useri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, akidai kuwa amejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya eneo lake lenye makazi yakudumu kuuzwa kwa amri ya mahakama, kutokana na mwanae kushindwa kutoa matumizi kwa mtalaka wake, hatimaye Uongozi wa juu wa wilaya hiyo umemfikia bibi huyo na kumpa msaada wa kisheria kutokana na madai yake.Ikumbukwe inaelezwa kuwa, hatua hiyo ya uuzwaji wa eneo hilo ilikuja ikiwa ni baada kijana wa bibi huyo kutofanyia kazi amri mahakama, ambayo ilimtaka atoe shilingi elfu 90,000 kila mwezi za matumizi kwa mtalaka wake ambaye aliondoka na watoto wake watatu baada ya ndoa yao kuvunjika.
Aidha, Ikumbukwe pia mwanaume anayedaiwa kushindwa kutoa fedha hizo kila mwezi aitwae Evarest Mrosso, alisema kuwa alishindwa kutii amri ya mahakama kutokana na hali ngumu aliyobakia nayo baada ya ndoa hiyo kuvunjika, na kisha mwanamke huyo kuondoka na mali zote pamoja na fedha za mauzo ya eneo walilokuwa wanaishi, ambazo zilidaiwa kuwa zinakwenda kutumika kuwatunzia watoto hao.
CHANZO: GADI TV