Mkuu Pole kwa maswahiba hayo!
Huyo Muiraq kwanza achana nae na kaa nae mbali saana kwasababu si muelewa, Alitakiwa akuvumilie japo kwa siku ile akae ajue nini kimekusibu mpaka ukaachiwa mtoto.. japo ni ngumu saana kwa mazingira ya mahusiano yenu yeye kuelewa.
Kingine ni kwanini akudai nauli tena kwa vitisho vikali, kwa hakika huyo hakufai kabsaa.
Tukirudi kwa baby mama wako yeye anakutaka toka kitamboo na ndio maana kakubebea mimba akijua uhusiano wenu utakua mkubwaa na imekua tofauti na matarajio yako. Mtafute mueleze ukweli nina imani atakuelewa kwa kuwa umekua ukishirikiana nae kwa karibu kwenye malezi. Alafu kaa nae mbali kwani huyo ataendelea kuwa kikwazo kwenye mahusiano yako yoyote yale.
Mwisho mkuu tuisendekeze tamaa za nyege kwa kukatisha ndoto za maisha yetu, Kwani wanaume wengi tunangonoka na wanawake ambao sio machaguo yetu kwakuwa tuu tumevutiwa labda na nyama nyama zao plus manyege yetu!!