Kilichonipata leo, nimekoma!!

Kilichonipata leo, nimekoma!!

Soma vizuri post yangu kwa utulivu kabisa,utaelewa,kumbuka hakuniambia kuwa ana watoto wengine watatu,nilipogundua hilo nikajisepesha tu,na kuamua kuanza upya,ndo yamenifika hayo,kosa langu mimi ni nini mkuu
wanaume tumebaki wachache sana, unadate na mwanamke kwa muda wa kutosha usijue kama ana watoto??

khaaa hii inatokeaje kwa mfano???
 
Jamani hapo nina kosa kweli???kama ndiyo kosa langu ni nini?😱🙁🙁🙁
wakati ameshikilia mtoto anataka kumnyonga wewe ulikuwa wapi??

au distance kati yake na wewe ulikuwa kilometa ngapi???

mpaka uanzee kutafuta pochi/waleti ilipo uanzee kuhesabu hela una mpaka ndio anamtupa mtoto na kuondoka huku unamwangalia......

wewe ni MPUUUUUUUZI.
 
wanawake wote hao ni wajinga hivi mwanamke mwanao wa miezi 3 unaanzaje kumuachia mtu
 
Mkuu chukue mttoto mpeleke kwa Mama yako amulee,achana na hao wanawake wote hawana akili
 
Soma vizuri post yangu kwa utulivu kabisa,utaelewa,kumbuka hakuniambia kuwa ana watoto wengine watatu,nilipogundua hilo nikajisepesha tu,na kuamua kuanza upya,ndo yamenifika hayo,kosa langu mimi ni nini mkuu
Wala huna haja ya kuwa na hofu Mkuu. Hakuna mwenye hatimiliki na wewe kati ya hao wawili. Huyo aliyeacha mtoto hajui kwamba analofanya ni kosa kubwa linaloweza kumletea matatizo kama utaamua kuchukua hatua. Kabla hujafika Polisi au ustawi Wa jamii wajulishe Viongozi wake Wa mtaa kuhusu kitendo alichofanya nao watawaita na mtajadiliana kwa busara na mtoto ataendelea kupata matunzo muhimu ya mama yake hadi atakapofikia umri wa kuweza kuwa mbali na mama yake. Lkn nakushauri kama hutamuoa mama yake jitahidi uchukue mtoto wako hata kabla ya miaka saba ya kisheria ili umtunze mwenyewe maana kutunza watoto watatu wa baba tofauti si mchezo. Kuhusu huyo Mbalabaigi hata mimi nadhani ni vema kama alivyoshauri mtu mmoja hapo juu, mwache aende; Maana kama ameshindwa kukaa na wewe kwa sababu tu umezaa na mwanamke mwingine basi hamtawezana mbeleni. Maisha ya ndoa yamejaa makosa na kujikwaa kwa pande zote, sasa mwanamke anayekushauri mumnyonge mtoto wakati mama mtoto anajua kamwacha hapo salama hafai hata kuwa hawala sembuse mke. Kuwa na amani brother maisha si meupe wakati wote.
 
wakati ameshikilia mtoto anataka kumnyonga wewe ulikuwa wapi??

au distance kati yake na wewe ulikuwa kilometa ngapi???

mpaka uanzee kutafuta pochi/waleti ilipo uanzee kuhesabu hela una mpaka ndio anamtupa mtoto na kuondoka huku unamwangalia......

wewe ni MPUUUUUUUZI.
Mkuu ningeweza kumtembezea kichapo kitakatifu vizuri kabisa,lakini sikutakankabisa kujaza watu,co ingeniondolea heshima yangu kabisa hapa mtaani,that is why niliamua kutoa tu hizo pesa
 
Huu ni mtihani mana Huyo bint anao watoto wengine wawili na huyu Wa miez 3 INA maana c wako, sasa endapo angekuambia mapema anao watoto wawili je ungekubali kua nae? Cha msingi zungumza nae umrudishe mtoto kwa mama yake mana miez 3 bado mdogo, pia huyo mpenz Wa manyara kauli akizotoa ni matishio tu na cyo maneno mazur ila pia anaweza kutenda, pia ni vizur ujifunze kwamba mwanamke akiongea anamanisha kitendo chakutaka kukuzalia mtoto kama we ulikua hutaki ungetumia zana umwambie asubir bado hujapanga kua na mtoto, pengine huyo Dada aliwaza akikuzalia utaongeza penz nakumuoa, pia yawezekana katika hao watoto aliokua nao alizalishwa akatelekezwa, nafikir kama unarizika kua anafaa kua MKE bora, amua kuanza maisha nae na kuhusu hao watoto wengine mnaweza kukaa mkapata solution mana ukianzisha mausiano mapya lazima atakuvuruga, pili wanaume ujifunze ukingia kwenye mapenz kwa ajili unamwonea huruma bint au kakupenda bint na we unampenda mwisho Wa cku huna hisia nae, kweli hiyo mbaya bora MTU kakupenda kataa kwan ukikataa utaonekana mwanamke, hivyo hapo chaggua moja, kuendeleza mapenz huko manyara au kuendelea na mzaz mwenzio
 
Jitahid kunpgia pande muiraq Mkuu nazskia tu sifa zao
 
Wala huna haja ya kuwa na hofu Mkuu. Hakuna mwenye hatimiliki na wewe kati ya hao wawili. Huyo aliyeacha mtoto hajui kwamba analofanya ni kosa kubwa linaloweza kumletea matatizo kama utaamua kuchukua hatua. Kabla hujafika Polisi au ustawi Wa jamii wajulishe Viongozi wake Wa mtaa kuhusu kitendo alichofanya nao watawaita na mtajadiliana kwa busara na mtoto ataendelea kupata matunzo muhimu ya mama yake hadi atakapofikia umri wa kuweza kuwa mbali na mama yake. Lkn nakushauri kama hutamuoa mama yake jitahidi uchukue mtoto wako hata kabla ya miaka saba ya kisheria ili umtunze mwenyewe maana kutunza watoto watatu wa baba tofauti si mchezo. Kuhusu huyo Mbalabaigi hata mimi nadhani ni vema kama alivyoshauri mtu mmoja hapo juu, mwache aende; Maana kama ameshindwa kukaa na wewe kwa sababu tu umezaa na mwanamke mwingine basi hamtawezana mbeleni. Maisha ya ndoa yamejaa makosa na kujikwaa kwa pande zote, sasa mwanamke anayekushauri mumnyonge mtoto wakati mama mtoto anajua kamwacha hapo salama hafai hata kuwa hawala sembuse mke. Kuwa na amani brother maisha si meupe wakati wote.
Nashukuru kwa ushauri wako wa kunijenga mkuu!!
 
Akienda polisi kumshitaki mama mwenye timu ya mpira si ndo ataambiwa aishi naye???
 
wanaume tumebaki wachache sana, unadate na mwanamke kwa muda wa kutosha usijue kama ana watoto??

khaaa hii inatokeaje kwa mfano???
Mkuu huyu dada watoto wake aliwaacha Mkoani,na kwa namna alivyo huwezi kudhani kama ameshazaa!!
 
Ndugu zangu wanaume wenzangu,kuna wakati tunafanya mambo na kuona ya kawaida sana,lakini ni hatari kuliko tunavyoweza kudhani.

Hapa nilipo siamini kilichonitokea,na sijui kesho yangu itakuwaje kwani vitisho nilivyopata vinaogopesha,wenzangu hapa mwaweza kunishauri.nisiwachoshe sana,iko hivi;

Nimekuwa kwenye mahusiano na msichana mmoja wa kiiraq mwenyeji wa huko Manyara,tulikuwa tunawasiliana vizuri kabisa kabla hatujaonana,kama miezi miwili hivi tukaonana Singida,it was very nice kwa kweli,tukapanga appointment nyingine msimu huu wa mapumziko,tukakubaliana aje Morogoro,(ndipo ninapoishi).

Pasipo hiana mtoto wa watu kafunga safari kutoka kwao katua Morogoro jana majira ya saa kumi hivi,nikamkaribisha nyumbani kwangu,tumefarijiana usiku kucha,pasipo na bugudha yoyote.

Kilichiharibia siku ni kwamba kuna mdada nilikuwa naye katika mahusiano,anakaa karibu na maeneo ninayoishi,nilikuwa naye katika mahusiano baada ya yeye kunishawishi sana,(tunafanya kazi ofisi moja) wakati tunaendelea na mahusiano aliniambia anataka mtoto wangu nikajua ananitania,lakini baadaye nikashangaa kweli ame-conceive,(bila makubaliano) kilichoniudhi zaidi nikagundua huyu dada ana watoto wengine wawili alikuwa amewaacha huko mkoani kwao,miezi kadhaa akawabeba watoto wake wote akakaa nao.

Sasa leo nikiwa na mgeni wangu,ambaye kiukweli ndo nimepanga kumuoa,mlango umegongwa,kufungua ni yule dada mwenye watoto wengi,hakuwa amewahi kuja karibia miezi 7 sasa,amekuja na mtoto ambaye kiukweli nimekuwa nikichangia malezi yake vema kabisa,amekuja akiwa amejaa hasira na kutaka kufanya fujo ndani kwangu,mwanaume nikalazimika kuwa mpole sana,ili kusolve mambo kimya kimya bila kujaza watu wengi,nimejitahidi sana kubembeleza mpaka kupiga magoti ili tu kulinda heshima yangu mtaani.

Akaamua kuondoka na kuniachia mtoto hapo ndani,na huyu mgeni wangu kageuka mbogo,mkali vibaya mno,akanambia anataka kuondoka,nimembembelez asiondoke kagoma,akanitaka nimpe nauli,nikampatia kama laki moja hivi akadai nimuongeze laki moja nyingine,otherwise anamnyonga mtoto,kwa muda huo alikuwa amembeba yeye,nikamuongeza laki moja akamtupa mtoto kitandani,akaondoka zake,lakini akaniambia "NAKWAMBIA UTANITAFUTA,LAZIMA NIKUTIE ADABU,LIKIKUPATA LA KUKUPATA KWETU KATESH,UTANIFUATA BILA KULAZIMISHWA" Maneno haya yameniogopesha sana japo sikuyajali sana.
Hapa nipo na mtoto wa miezi mitatu hivi,sielewi hata nifanye nini kwani mama yake hajarudi tena tamgu ameondoka.
Kama ni kweli,
WOTE WAWILI HAWAFAI:

sababuni hizi:
huyo uliyezaa nae, angefaa kama angekuwa na staha, ukweli na uvumilivu,

ukweli kabla hujamtia doa

uvumilivu baada ya kukukuta na mtu mwingine, maana yeye hujamuoa.

staha haijaonekana wala huruma, hasa baada ya kutelekeza mtoto mchanga, ambae ukilipoti polisi baada ya kukaa nae saa 24 anatafutwa kama mharifu, anafikishwa mahakamani kuthibitisha kosa lake, na jela ya miezi 6 inamhusu.

Huyo mu Iraqi
hafai kwa kuwa ana ujasiri wa kuua, kama anaweza kusema, " usipompa kile anachokitaka ananyonga mtoto" hafai jikoni, hafai hata chooni.

mwisho Usiwe unatutia mawazo kwamba una matatizo makubwa ki hivyo mpaka tunalia machozi kwa ajiri yako kumbe ni porojo zako!

"MUNGU ANAKUONA!"
 
Huu ndio ukomavu kwenye hii nyanja yetu aiseeee......
Wewe lea tu mwanao kwa kuajiri mtu wa kumtunza, na hakikisha unamlipa poa.
Kwakifupi hii kesi ndogo sana mkuu, wapuuze hao wanawake na kisha endelea na maisha yako mapya pamoja na mwanao.
 
Mkuu ningeweza kumtembezea kichapo kitakatifu vizuri kabisa,lakini sikutakankabisa kujaza watu,co ingeniondolea heshima yangu kabisa hapa mtaani,that is why niliamua kutoa tu hizo pesa
kujaza watu kwa namna gani??

unamfinya mfinyo mmoja wa hatari hata sauti haitatoka kimyaaaaaaaa!

laki nyingine?????

hii stori ni ya lini??? kama ni kipindi cha kikwete sawa!, ila kama ni kipindi HIKI cha SAADAM HUSEIN/IDDI AMINI sidhani kama inawezeka!
 
Sina cha kuzungumza wala ushauri wa aina yeyote.
Ila nakupa pole sana kwa yaliyokukuta na usikate tamaa wala kupaniki ila tulia tafakari kama mwanaume ujue unachukua maamuzi gani....??
Muombe sana mungu akulinde na kukupa amani mkuu.......... Usianze mwaka vibaya ila anza mwaka vizuri wenye furaha na amani. ( * 2017 * ) nakutakia maisha mema na maisha marefu.....
 
huyo mwanamke wa kiiraq mlifahamiana wap kwanza kabla ya kuanza uhusiano naye
-facebook
-instagram
-jf
tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom