Kilichonipata leo, nimekoma!!

Kilichonipata leo, nimekoma!!

Mkuu huo mchezo simple unakutisha nini sasa.nianze na huyo dem Wa kiirak sijui nae ulikuwa umeingia chaka kama la huyo uliezaa nae tu.alikuwa mpiga dili sema kimesanuka mapema na inabid ushukuru sio mke huyo.kuhusu huyo mama Wa mtoto usisubiri mpaka arudi.kuwa mpole mtafute uwa wanaelewa mana mtoto bado Mdogo.huyo Wa kiirak boya tu hawez Fanya lolote.akikuroga leta mrejesho hapa

hahaaaaaaaa mkuu usinichekeshe eti akikuroga leta mrejesho,atajuaje kalogwa???
 
Lakoni mwanawane sii ulimgegeda ule usiku sasa tatizo wapi?
 
Boya ww...mwanaume gani unapelekeshwa na wanawake
 
Boya ww...mwanaume gani unapelekeshwa na wanawake
Duuh,haya bhana lakini kwa mazingira yalivyokuwa,busara pekee ndo ilikuwa ya kulinda heshima yangu,kwani vinginevyo kitu ambacho kingetokea ingekuwa gumzo mtaa mzima!!!
 
Ndugu zangu wanaume wenzangu,kuna wakati tunafanya mambo na kuona ya kawaida sana,lakini ni hatari kuliko tunavyoweza kudhani.

Hapa nilipo siamini kilichonitokea,na sijui kesho yangu itakuwaje kwani vitisho nilivyopata vinaogopesha,wenzangu hapa mwaweza kunishauri.nisiwachoshe sana,iko hivi;

Nimekuwa kwenye mahusiano na msichana mmoja wa kiiraq mwenyeji wa huko Manyara,tulikuwa tunawasiliana vizuri kabisa kabla hatujaonana,kama miezi miwili hivi tukaonana Singida,it was very nice kwa kweli,tukapanga appointment nyingine msimu huu wa mapumziko,tukakubaliana aje Morogoro,(ndipo ninapoishi).

Pasipo hiana mtoto wa watu kafunga safari kutoka kwao katua Morogoro jana majira ya saa kumi hivi,nikamkaribisha nyumbani kwangu,tumefarijiana usiku kucha,pasipo na bugudha yoyote.

Kilichiharibia siku ni kwamba kuna mdada nilikuwa naye katika mahusiano,anakaa karibu na maeneo ninayoishi,nilikuwa naye katika mahusiano baada ya yeye kunishawishi sana,(tunafanya kazi ofisi moja) wakati tunaendelea na mahusiano aliniambia anataka mtoto wangu nikajua ananitania,lakini baadaye nikashangaa kweli ame-conceive,(bila makubaliano) kilichoniudhi zaidi nikagundua huyu dada ana watoto wengine wawili alikuwa amewaacha huko mkoani kwao,miezi kadhaa akawabeba watoto wake wote akakaa nao.

Sasa leo nikiwa na mgeni wangu,ambaye kiukweli ndo nimepanga kumuoa,mlango umegongwa,kufungua ni yule dada mwenye watoto wengi,hakuwa amewahi kuja karibia miezi 7 sasa,amekuja na mtoto ambaye kiukweli nimekuwa nikichangia malezi yake vema kabisa,amekuja akiwa amejaa hasira na kutaka kufanya fujo ndani kwangu,mwanaume nikalazimika kuwa mpole sana,ili kusolve mambo kimya kimya bila kujaza watu wengi,nimejitahidi sana kubembeleza mpaka kupiga magoti ili tu kulinda heshima yangu mtaani.

Akaamua kuondoka na kuniachia mtoto hapo ndani,na huyu mgeni wangu kageuka mbogo,mkali vibaya mno,akanambia anataka kuondoka,nimembembelez asiondoke kagoma,akanitaka nimpe nauli,nikampatia kama laki moja hivi akadai nimuongeze laki moja nyingine,otherwise anamnyonga mtoto,kwa muda huo alikuwa amembeba yeye,nikamuongeza laki moja akamtupa mtoto kitandani,akaondoka zake,lakini akaniambia "NAKWAMBIA UTANITAFUTA,LAZIMA NIKUTIE ADABU,LIKIKUPATA LA KUKUPATA KWETU KATESH,UTANIFUATA BILA KULAZIMISHWA" Maneno haya yameniogopesha sana japo sikuyajali sana.
Hapa nipo na mtoto wa miezi mitatu hivi,sielewi hata nifanye nini kwani mama yake hajarudi tena tamgu ameondoka.
Hata ijitetee huku ujue ntakukomesha. Mpuuzi sana wewe. Unadhani huku sifiki
 
pole sana mkuu ila hata huyo uliyezaa naye si mstaarabu siku zote alikuwa wapi na huduma muhimu za mtoto alikuwa anapata wala haina haja ya kurudiana naye,ila huduma za msingi kuhusu mtoto mpe,pili huyo wa katesh asikutishe maneno tu hayo fanya mambo mengine.
 
Pole sana mkuu, hao wanawake sijui wamekuchukuliaje! Huyo mwenye watoto12 kwani mlipanga kuoana? Kama sio kwa nn ukubali akufanyie fujo wakati yeye ndo mzinzi namna 1 na ushahidi upo? Huyu muirak kashindwa kukuelewa vile ulivomalizana na mama mtoto wako ndo maana akaona achukue chake mapema, na labda ni mpiga dili mzoefu!
We we nae umeonyesha uzaifu mkubwa kwa kuanza kulialia ndo mana wamekupanda' alivokuja kwa hasira ungemuelewesha kuwa ulienae ndo mkeo mtarajiwa, hata kama angemuacha mtt lakini ungekuwa umejihami kwa muirak lazima angekuwa mpole na asingeondoka kwa kujua yupo na MTU anaejiamini" ona sasa umekosa kila kitu!

Usiogope muirak hawezi kukuloga, anakutisha tu vile kakusoma muoga muoga.

Kati ya hao wawili hakuna Mke hapo, kidoogo Huyo mwenye watoto 12 anaeleweka"
 
Amemtishia kweli kumuua mtoto au umenogesha tuu, hapo hamna hata mmoja anaefaa yaani umuache mtoto wako mchanga sababu ya mwanaume?? Umnyonge mtoto sababu ya laki??
 
Jamani hapo nina kosa kweli???kama ndiyo kosa langu ni nini?😱🙁🙁🙁
Kosa kubwa kabisa unalolifanya katika maisha yako ni KUTELEZA(kufanya mapenzi bila kutumia Condom).

Haya mengine yote ni ya kibinadamu coz we all make mistakes...

HAKIKISHA UNATUMIA CONDOM MAISHA YAKO YOTE.
 
Jipange kulea mwanao, achana na kiruka njia wa Katesh. Wenzio wanatafuta watoto wewe unawaza mwanamke ambaye mmekutana juu kwa juu.
 
Mkuu hayo maneno aliyotamka kua utamtafuta sio ya kuyapuuzia kabisa, kuna wengine wanaeza kua wanatania ila wengine sio watu wazuri kabisa, na wanamaanisha wanachosema, miba ipo mkuu. Kwa ushauri tuu mtafute huyo muiraq uongee nae taratibu na kumuomba sana msamaha kwa kutomwambia kabla kua una mtoto. Nadhani atakusamehe
 
Hapo hamna mke hapo, nina penda sana kushughulika na mambo ya mahusiano kwa kujitazama mwenyewe na siyo kutazama partners wangu! yaani kwa kitendo tu cha kuwa ndani ya mahusiano na watu wa namna hiyo inaonekana kabisa na wewe tabia yako au level yako ya kufikiria ipo tu katika kiwango sawa na wao! fanyia kazi hilo swala la mtoto mdogo, kamwe mama hawezi muacha mtoto wake. huyo mwingine asikutishe, ingawa pia amefanya yote hayo katika hali ya hasira na wewe msimamo wako kutoeleweka ulichangia. Kaa utulie solve haya mambo yakiisha jirekebishe wewe kwanza am sure utaanza kuatract wanawake wanao faa kuwa wake
 
Consequences of ur actions bro....sasa kusuffer ndo kunakuja....Kaza buti uyashinde
 
Back
Top Bottom