CHIEFMANGU
JF-Expert Member
- Dec 19, 2016
- 499
- 737
Ndugu zangu wanaume wenzangu,kuna wakati tunafanya mambo na kuona ya kawaida sana,lakini ni hatari kuliko tunavyoweza kudhani.
Hapa nilipo siamini kilichonitokea,na sijui kesho yangu itakuwaje kwani vitisho nilivyopata vinaogopesha,wenzangu hapa mwaweza kunishauri.nisiwachoshe sana,iko hivi;
Nimekuwa kwenye mahusiano na msichana mmoja wa kiiraq mwenyeji wa huko Manyara,tulikuwa tunawasiliana vizuri kabisa kabla hatujaonana,kama miezi miwili hivi tukaonana Singida,it was very nice kwa kweli,tukapanga appointment nyingine msimu huu wa mapumziko,tukakubaliana aje Morogoro,(ndipo ninapoishi).
Pasipo hiana mtoto wa watu kafunga safari kutoka kwao katua Morogoro jana majira ya saa kumi hivi,nikamkaribisha nyumbani kwangu,tumefarijiana usiku kucha,pasipo na bugudha yoyote.
Kilichiharibia siku ni kwamba kuna mdada nilikuwa naye katika mahusiano,anakaa karibu na maeneo ninayoishi,nilikuwa naye katika mahusiano baada ya yeye kunishawishi sana,(tunafanya kazi ofisi moja) wakati tunaendelea na mahusiano aliniambia anataka mtoto wangu nikajua ananitania,lakini baadaye nikashangaa kweli ame-conceive,(bila makubaliano) kilichoniudhi zaidi nikagundua huyu dada ana watoto wengine wawili alikuwa amewaacha huko mkoani kwao,miezi kadhaa akawabeba watoto wake wote akakaa nao.
Sasa leo nikiwa na mgeni wangu,ambaye kiukweli ndo nimepanga kumuoa,mlango umegongwa,kufungua ni yule dada mwenye watoto wengi,hakuwa amewahi kuja karibia miezi 7 sasa,amekuja na mtoto ambaye kiukweli nimekuwa nikichangia malezi yake vema kabisa,amekuja akiwa amejaa hasira na kutaka kufanya fujo ndani kwangu,mwanaume nikalazimika kuwa mpole sana,ili kusolve mambo kimya kimya bila kujaza watu wengi,nimejitahidi sana kubembeleza mpaka kupiga magoti ili tu kulinda heshima yangu mtaani.
Akaamua kuondoka na kuniachia mtoto hapo ndani,na huyu mgeni wangu kageuka mbogo,mkali vibaya mno,akanambia anataka kuondoka,nimembembelez asiondoke kagoma,akanitaka nimpe nauli,nikampatia kama laki moja hivi akadai nimuongeze laki moja nyingine,otherwise anamnyonga mtoto,kwa muda huo alikuwa amembeba yeye,nikamuongeza laki moja akamtupa mtoto kitandani,akaondoka zake,lakini akaniambia "NAKWAMBIA UTANITAFUTA,LAZIMA NIKUTIE ADABU,LIKIKUPATA LA KUKUPATA KWETU KATESH,UTANIFUATA BILA KULAZIMISHWA" Maneno haya yameniogopesha sana japo sikuyajali sana.
Hapa nipo na mtoto wa miezi mitatu hivi,sielewi hata nifanye nini kwani mama yake hajarudi tena tamgu ameondoka.