Kilichonipata leo, nimekoma!!

Kilichonipata leo, nimekoma!!

Aisee hiyo papuchi mpya iliyoondoka ni hatari kwa maisha yako na ya mtoto wanawake ya vitisho design hiyo ukiwa nao nasi maisha yako yatakuwa ni hatarishi
 
Pole sana mkuu,hapo itabidi umtafute huyo mama watoto muyameleze ili mtoto aweze pata malezi ya mama,mtoto bado Mdogo mno kumtunza mwenyewe
 
Ndugu zangu wanaume wenzangu,kuna wakati tunafanya mambo na kuona ya kawaida sana,lakini ni hatari kuliko tunavyoweza kudhani.

Hapa nilipo siamini kilichonitokea,na sijui kesho yangu itakuwaje kwani vitisho nilivyopata vinaogopesha,wenzangu hapa mwaweza kunishauri.nisiwachoshe sana,iko hivi;

Nimekuwa kwenye mahusiano na msichana mmoja wa kiiraq mwenyeji wa huko Manyara,tulikuwa tunawasiliana vizuri kabisa kabla hatujaonana,kama miezi miwili hivi tukaonana Singida,it was very nice kwa kweli,tukapanga appointment nyingine msimu huu wa mapumziko,tukakubaliana aje Morogoro,(ndipo ninapoishi).

Pasipo hiana mtoto wa watu kafunga safari kutoka kwao katua Morogoro jana majira ya saa kumi hivi,nikamkaribisha nyumbani kwangu,tumefarijiana usiku kucha,pasipo na bugudha yoyote.

Kilichiharibia siku ni kwamba kuna mdada nilikuwa naye katika mahusiano,anakaa karibu na maeneo ninayoishi,nilikuwa naye katika mahusiano baada ya yeye kunishawishi sana,(tunafanya kazi ofisi moja) wakati tunaendelea na mahusiano aliniambia anataka mtoto wangu nikajua ananitania,lakini baadaye nikashangaa kweli ame-conceive,(bila makubaliano) kilichoniudhi zaidi nikagundua huyu dada ana watoto wengine wawili alikuwa amewaacha huko mkoani kwao,miezi kadhaa akawabeba watoto wake wote akakaa nao.

Sasa leo nikiwa na mgeni wangu,ambaye kiukweli ndo nimepanga kumuoa,mlango umegongwa,kufungua ni yule dada mwenye watoto wengi,hakuwa amewahi kuja karibia miezi 7 sasa,amekuja na mtoto ambaye kiukweli nimekuwa nikichangia malezi yake vema kabisa,amekuja akiwa amejaa hasira na kutaka kufanya fujo ndani kwangu,mwanaume nikalazimika kuwa mpole sana,ili kusolve mambo kimya kimya bila kujaza watu wengi,nimejitahidi sana kubembeleza mpaka kupiga magoti ili tu kulinda heshima yangu mtaani.

Akaamua kuondoka na kuniachia mtoto hapo ndani,na huyu mgeni wangu kageuka mbogo,mkali vibaya mno,akanambia anataka kuondoka,nimembembelez asiondoke kagoma,akanitaka nimpe nauli,nikampatia kama laki moja hivi akadai nimuongeze laki moja nyingine,otherwise anamnyonga mtoto,kwa muda huo alikuwa amembeba yeye,nikamuongeza laki moja akamtupa mtoto kitandani,akaondoka zake,lakini akaniambia "NAKWAMBIA UTANITAFUTA,LAZIMA NIKUTIE ADABU,LIKIKUPATA LA KUKUPATA KWETU KATESH,UTANIFUATA BILA KULAZIMISHWA" Maneno haya yameniogopesha sana japo sikuyajali sana.
Hapa nipo na mtoto wa miezi mitatu hivi,sielewi hata nifanye nini kwani mama yake hajarudi tena tamgu ameondoka.
Ndugu yangu umevuna ulichopanda, maisha Ni km taswira unayoiona kwenye kioo, ukicheka Na yenyewe inacheka. Malezi mema ndugu...
 
Ndugu yangu umevuna ulichopanda, maisha Ni km taswira unayoiona kwenye kioo, ukicheka Na yenyewe inacheka. Malezi mema ndugu...
Kosa langu ni nini mkuu,na nimevuna nilichopanda,how????
 
Achana na wote. Huyo mwenye mtoto alitaka kuzaa mwenyewe hivyo anatumia mtoto kama silaha ya kujihami, anataka nini haswa, umuoe? Ili umkomeshe jikaushe na usimtafte maadam mtoto yupo mikononi mwako, mpeleke kwa mamako najua atakuhurumia tu mwanae kama haiwezekani mpeleke kituo cha kuleana mpaka atapofikisha umri flani hivi wa kuweza kukaa nae au tafta hata maid wa kukusaidia kumlea mwanao na usonge mbele na maisha
 
A

Ahsante ndugu,hilo lilishakuwa solved,Mungu mwema
 
Duuh,kweli baadhi ya wanawake ni hatari,yule mdada wa Ki-Iraq amenijia tena,eti anaomba NIMSAMEHE kwa yaliyotokea,bado ananipenda sana,hivyo tuendelee na mahusiano yetu,lakini kwa bahati mbaya sana kilichotokea MWANZA (WANANDOA KUUANA KWA RISASI) imenijengea picha fulani ya woga wa kumrudia maana aweza kunifanyia kitu kibaya sana!!!
 
Soma vizuri post yangu kwa utulivu kabisa,utaelewa,kumbuka hakuniambia kuwa ana watoto wengine watatu,nilipogundua hilo nikajisepesha tu,na kuamua kuanza upya,ndo yamenifika hayo,kosa langu mimi ni nini mkuu
Kosa lako kujiepusha bila kumwambia huna mpango nae ila Mtoto utalea,yy akajua ushafika kwake,sasa Huyo wa kateshi achana nae,nae Hugo mzazi mwenzio achana nae ila Lea Mtoto wako bila hiana, tafuta wakuzikana nae, (oa mwingine) mweleze a-z ajue kabla ykumuweka ndani aamue kusuka au kunyoa hapo utafurahia maisha maana hao wrote hawana vigezo, mrudie muumba wako after finish your marriage
 
Duuh,kweli baadhi ya wanawake ni hatari,yule mdada wa Ki-Iraq amenijia tena,eti anaomba NIMSAMEHE kwa yaliyotokea,bado ananipenda sana,hivyo tuendelee na mahusiano yetu,lakini kwa bahati mbaya sana kilichotokea MWANZA (WANANDOA KUUANA KWA RISASI) imenijengea picha fulani ya woga wa kumrudia maana aweza kunifanyia kitu kibaya sana!!!
Kuwa makini dunia imevaa gunia ...
 
Back
Top Bottom