Hii habari ni kweli kabisa.
Attempt yangu ya kwanza ya PhD ilikuwa political anthropology nikitazama patriotism from the perspective of tribal loyalty, bahati mbaya ile project niliiachia hatua za awali baada ya funding kukatika ghafla. Lakini nilikuwa nimeshajifunza mambo mengi, mojawapo ni hili.
Supervisor wangu aliniunganisha na mtu wa Liberia anaitwa James Youboty tukawa marafiki na akawa ananitumia data nyingi. Ali-scan vitu vingi sana akanitumia, ikiwemo hata hotuba za mwisho za Samuel Doe alipokuwa anajitahidi kuungana na Prince Johnson ili kwa pamoja wamshinde Charles Taylor.
Kulikuwa na details za jinsi Doe alivyotumia machifu wa kabila lake la Krahn kutoka eneo la Grand Gedeh, minutes za vikao nk. Jinsi askari wa kabila la Krahn walivyosimama kidete nyuma ya Doe hadi siku yake ya mwisho.
Kikubwa kuliko vyote ambavyo James aliniruhusu kuona ni maktaba yake ya kanda za VHS zenye detail za mateso yote ambayo Prince Johnson alimfanyia Doe, ni ukatili wa ajabu mno na niliamini kuwa wale askari wake na yeye mwenyewe walikuwa wavuta bangi, huwezi kumtenda binadamu mwenzio hivyo!
Kabla ya kifo chake ambacho kilitokana na kuvuja damu nyingi, Samwel Doe alikatwa masikio yote mawili na uume wake ulikatwa kwa singe lakini haukumalizikia, ndiyo unapoona hapo kwenye picha uume ulikuwa umevilia damu.
Jambo moja pia ni kuwa James alikuwa kabila moja na Doe kwa hiyo alitoa sana story ya upande mmoja. Na pia kuweza kuwa na details zote za mateso ya Doe ilinipa picha kuwa alihusika na intelligence system yao pia (ingawa alidai ni mwandishi wa habari, lakini kuna kila ushahidi kuwa ni zaidi ya hapo). Kule US, wale mashushushu wa enzi ya Doe na familia zao wana umoja wao una nguvu sana.
James pia ameandika kitabu kinaitwa 'A Nation in Terror', ambacho pia alinipa a signed copy. Kina fine details za mateso na kifo cha Samuel Doe ambaye huyu James anamsifu kupita kiasi kama shujaa wa Liberia