Kilichojiri bungeni Tarehe 13 April (Muswada wa mafao)

hebu tuwatendee haki mps? wa cdm, walisimama kidete kukataa muswada! Labda mlikuwa hamjauelewa bado wakati wanaukataa
 
Tatizo watu hamkuelewa wakati mp wa cdm wanapinga, hamkujua madhala sasa naona mnaelewa taratibu, blame yourself! Lol
 
Wakati ccm wakisema 'ndioooo' , halafu wewe ukajichanganya na ka-'siyooo' chako, ni sawa na sauti ya mtoto mdogo anaelia wakati mashine ya diesel ikisaga . Unategemea asikike?
 
Da! haya mambo yanachanganya sana.
Labda kwa tuangalie kwa upande wa pili, vipi wabunge wa CCM na vyama vingine hawajatuangusha?
yes.umeuliza vizuri sana hao chama cha kijani wao wametetea vipi?serikali mmeikabidhi kwa chama chenye rangi ya mbogamboga sasa wadaini wao si ndo wameshika mpini?chadema haidhoofishwi kwa hoja dhaifu
 
Mambo mangapi cdm wana kataa lakini madhaifu wana pitisha???
Au hujui idadi kubwa bungeni ni madhaifu???sasa una tegemea nini cdm wafanye wakati sauti yao ime mezwa na madhaifu...
Ebu sumbua akili kidogo...
 
Huu utegemezi wa CHADEMA kwenye kila kitu utatupeleka pabaya, kuna siku mtu atapigwa na mke wake alafu asubiri CDM ije imtetee,kama we ni mfanyakazi ni wakati wako wakuonyesha kwamba hukubaliani na hili swala. Chadema wakisema tufanye maandamano ya amani kupinga huu unyonyaji, nyie ndio wa kwanza kusema hiki ni chama cha wapenda vurugu, kwa hiyo subirini hivyo hivyo.
My take:
Nani atakukomboa mwaka huu? Je utaisubiri CHADEMA?

good coment!
 
Ndiooooooooo....za mafala wa wabunge wa Ccm ndio zinatupeleka kote huko,mijitu ikiwa isinzia bungeni bwana na kupiga meza tu baada ya kuchambua mambo .
 
Vyama vyetu vya wafanyakazi ndio bure kabisa. Hebu angalia chama cha wafanyakazi cha Afrika Kusini! Kina-influence hata ya kumpata rais wa nchi. Sisi vyama vyetu mabuda buda tu. Tuunde chama kingine cha wafanyakazi. wanachukua hela za wafanyakazi kula tu, hawatoi miongozo yoyote. Waliitwa kwenye utunzi wa hii sheria, wakapewa allowance ya kikao wakatulia wakapitisha, sasa tunalia. Kikwete akiwatisha tu wanayeyuka. Napendekeza Dr. Ulimboka akirudi tufanye kikao na kada zote za wafanyakazi tuanzishe chama tofauti na hivi tulivyo navyo. Ikiwezekana COTU tuifumui kabisa. Tunahitaji mabadiliko.
mkuu nakuunga mkono.hawa akina MGAYA NI WACHUMIA TUMBO WA KUTUPWA HAWATUFAI Kwa lolote.
 
kwa vyovyote vile chadema na chama cha wafanya kazi tunawategemea watuongozi juu ya hii sheria ya kijinga yaani mpaka sasa siamini kama ilipita bungeni..
mkuu kumbe na wewe umeona eeh? hawa ccm tulishajua hawatusaidii kwa lolote.kazi ni ishabiki tu wa ndio mzee.lakini chadema japokuwa ni wa chache lakini sauti yenu watanzania wanaisikia sana tena bila chenga katkkati ya misauti ya ndioooo... hivyo ndio kusema hamjatetea vya kutosha.hamjapaza sauti yenu.labda kama ni kweli hicho kipengele hakikuwepo kama anavyosema edson.otherwise chadema mna kesi ya kujibu kwa wafanyaki.Please cant you do somethkng??? come on MNYIKA.ZITO.TUNDU LISSU..ETAL
 
they are not angels so sometimes they mistake,by the way we shud know that they are for both our motives as a nation also for their own benefits,i think all MP's were to consider that for our sake
 
Wabunge wa CHADEMA mnawaonea bure, jambo CCM wakilitaka hata CDM wafuke moshi litapita tu.

Mmesahau sheria ya usimamizi wa mahakama iliyowapa wakuu wa mikoa na wilaya nguvu kubwa juu ya mahakama kwenye maeneo yao. Lissu aliongea mpaka waziri mkuu alikubali sio sawa nidhamu ya mahakama kusimamiwa na hawa watu. At the end of the day, the law was passed.
 
Hivi siku zote unadhani Chadema wapo kwa ajili ya kusaidia wananchi hawa Chadema wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Wakitetea wabaya wakikaa kimya wabaya ,wafanyakazi ndio wanaoathirika tuiambie serikali juu ya hilo,wabunge 40 wa chadema wanazomewa na ccm ,wapo watu wako happy hali hiyo inapojitokeza
 
Msipende kuongelea maswala ya kitaifa kwenye kundi fulani ndio muwape mamlaka ya kuwaongelea well mnapaswa kuuliza wale mliowapigia kura na wawakilishi wenu kule bungeni wapo zaidi ya 360 si hao saba tuu mliowachagua hivyo kama lawama pelekeni kwa wote huko bungeni.

Pili kama wajua kama hata kama wao wangepinga lakini jambo hili lingepita then kauli zao za hapana mwafikiri zingekuwa zimefanya nini, wamesha sema siyo mara nyingi na wataendelea kusema hivyo mpaka siku ya mwisho la msingi ni kuwapa watu wengi zaidi watakao weza sema siyo kwa kishindo na najua mwafahamu ni kwa njia gani hili litaweza fikia ni kura yako tuu
 
Ndugu zangu wana jf,nimeshangazwa sana na kusikitishwa sana na sheria mpya ya SSRA juu ya mafao ya wafanyakaZI,NIMESIKITISHWA SANA NA WABUNGE AMBAL TUNAWAONA KAMA WATETEZI WETU KUPITISHA SHERIA HII KIMYA KIMYA WAKIJUA KUWA WAO HAIWAATHIRI... NA KWAKWELI HAPA NAMAANISHA WABUNGE WA UPINZANI HASA HASA CHADEMAA, Hapa namaanisha akina ZITO,MNYIKA,TUNDU,MBOWE.MDEE.etal...

SISEMI KUWA MNA UAMUZI WA KUIZUIA MAANA HAIWEZEKANI MAANA WA NDIOOO wengi lakini angalau mngepaza sauti tungewawikia. Lakini kwa sasa mtawaambia nini wa Tz?

I must admit,i am utterly disappointed with you guys... you havent done your home work properly..
Kama hufuatilii bunge ni bora ukakaa kimya au kuomba taarifa kwa walizonazo. Binafsi ninakumbuka kuwa Halima Mdee na wenzake walipingana sana na hoja zilizokuwa zinapigiwa chapuo na Werema ktk kikao cha mwezi Aprili lakini ilishindikana kutokana na uchache wao bungeni. Acha kutoa judgement kama huna uhakika na hoja unayojenga, omba kwanza taarifa wenye nazo watakupatia.
 
kwenye hili imenifanya niamini Tanzania hatuna wabunge kabisa? haiingii akilini wabunge wapitishe mswaada huo na Rais asaini then Wabunge nao washangae sheria waliyoipitisha wenyewe! huu ni USALITI ULIOPITILIZA
 
kanuni za bunge letu ni kuwa sheria inapitishwa na upande wenye wabunge wengi. Utalaumuje CHADEMA ilhali watanzania waliwapa CCM wabunge wengi na serikali? Mambo kama haya yanapotokea inabidi ulaumu serikali yako pamoja na CCM; siyo kulaumu chama cha upizani. Kila mara CDM wakilalamika na kususia vikao vya bunge hawajahi kusaidiwa na wanachi kupaaza sauti zao, kwa hiyo iwapo wakisema "tupunguze kelele," mimi sitawalaumu sana. Ninajua kuwa at least walitakiwa waliongelee ili lijulikane kwa wananchi, lakini je kwani ni wabunge wa CDM tu ndio wako mjengoni mle kwa ajili ya wanachi?

Fahamu kuwa kuna nchi nyingi ambazo zina umri maalum wa kuchukulia mafao; kwa mfano nadhani kule Ufaransa yule jamaa Sarkozy, aliyetoswa uchguzi uliopita, alipandisha umri huo hadi miaka 65 au 70 hivi. Kwa marekani kuna namna mbili za mafao: yapo yanayotolewa ukifikisha umri fulani, na yale ambayo unaweza kuchukua wakati wowote hata kama hujaacha kazi mradi tu uyalipie kodi na faini zake. Sijui kwa Tanzania lakini kwa vyovyote vile lawama ni lazima ziwe kwa serikali na chama chenye wabunge wengi bungeni siyo chama cha upinzani.
 
huu ujinga kwanza sisi wenye pesa zetu lazima tuwe na nguvu na mamlaka juu ya pesa zetu kuliko hawa watu sababu hizo pesa ni jasho letu liwalo na liwe

hapa kuna wabunge wengine hawakulijua hilo wachache ndo walioiona na wakaisain eti kwa kuwawakilisha wenzao
 
Back
Top Bottom