CDM wasingepiga kelele. Makosa ya CCM kwao ni mtaji. Tuwashukuru wabunge wa CDM kwa kukaa kimya. Kwa kupitisha sheria haramu na kandamizi kama hii, CCM wamejiongezea maadui na kufifisha hali yake ya kukubalika kwa wafanyakazi. Kwa maneno mengine, wamechimba na kusakafia kaburi lao wenyewe. Ukweli hata wakiifuta leo, tayari wameshatujeruhi kisaikolojia.