Kilango amwambia waziri kasema uongo!

Jana Mh. Anne Kilango alimshambulia Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu TAMISEMI Aggrey mwanry kwa madai kuwa amelidanganya bunge juu ya maji. Hata hivyo Spika/Naibu spika hakumtaka kutoa uthibitisho. Kwanini?

Tafakari, Chukua hatua

Quality
hilo ndo chama wanalosema Lowasa kaliaribu wakati lichama lenyewe ndo UPUPU mtupu!
 
kale kajamaa kanaitwa kazi Ndugai sijui Job! na bi kiroboto utasikia tulikuwa tumelala hatukusikia km siku ile Lukuvi alivyowasha mic bila kuruhusiwa na akapewa muda wa kuhutubia lkn kamandaz wetu wakafukuzwa bungeni eti kwa kuwasha mic!
 
Wana JF hebu tumsubiri Ndugai atasema nini kwa Kilango kumtuhumu waziri kasema uongo. Alifanya hivyo Lema wakaja juu kama nini na mwisho wa siku ushahidi ukaletwa sasa wameukalia.

Tunataka Anne Kilango athibitishe kwa maandishi kama kanuni inavyotaka. Kama kweli msumeno unakula kote kote tuone hapa itakuwaje.
 
Nyambali Nyangwine (Tarime-CCM): Nitawaongoza wananchi na mapanga tukawakatekate wawekezaji
Job Ndugai (Naibu Spika - CCM): Aaah, hiyo ni lugha tu ya kule Tarime, haina tatizo
 
Hawa magamba wanalindana sana,sasa naona wapinzani wametulia kidogo nadhani wanajipanga kwaajili ya ngereja msema uongo na sijui atatokea wapi?
 
angekuwa cdm angeombwa uthibitisho

hebu tuwe wakweli, chukulia hoja ya barabara ya kariakoo - mbagala iliyokataliwa na magufuli kutokana na ubora wa bora iishe na hoja ya mh...... Wa mbozi kuwa tatizo ni 10%, spika kweli asitake uthibitisho? .......... Wa hiyo 10%
 
Nyambali Nyangwine (Tarime-CCM): Nitawaongoza wananchi na mapanga tukawakatekate wawekezaji
Job Ndugai (Naibu Spika - CCM): Aaah, hiyo ni lugha tu ya kule Tarime, haina tatizo

Wana JF,

Kule tarime wakisema ntakughecha its seriously anakukata panga na ndivyo Mbunge wa CCM_Tarime Nyambali Nyangwine alivyosema sasa Job unapo sema ndio lugha yao na kwanini huko serikali imeuweka kama ni mkoa wa kanda ya kipolice which means munajua maana ya kughecha?
 
Lakini kwa vile kusema uwongo bungeni ni kosa linaloadhibiwa kwa kumsimamisha mbunge asifanye shughuli za ubunge kwa muda, je kwa nini naibu waziri naye asisimamishwe ubunge wake kwa muda?

Na kwa vile uwaziri unatokana na ubunge, baada ya waziri kusimamishwa ubunge kwa muda itabidi asimamishwe pia uwaziri wake kwa muda. Na kwa vile nafasi za uongozi wa serikali haziwezi kuachwa wazi kwa muda, itabidi rais ateue naibu waziri mwingine !!!
 
Nimekuwa nikifuatilia bunge.....mara kadhaa nimekuwa nikiwasikia baadhi wabunge wa ccm wakisema waziri kadanganya but spika hasemi wathibishe lakini wanaposema wabunge wa chadema huambiwa wathibitishe. Nadhani hii haiko fair kwani kama sheria ni msumeno inabidi itumike kwa wabunge wa pande zote
 
waziri yeyote muongo ni mshirikina. Huyu waziri anaonekana kuwa mzembe sana na mvivu. Iweje aende sasa kuona miradi ya maendeleo badala ya kwenda kabla ya kikao cha bunge kuanza. Hivi jamani tunakuwa na mijitu kama hii ili kujenga nchi kweli tutafika?
 
ccm ni chama cha kifisadi kwa hiyo hiyo dhuluma sasa wameanza kusogezeana wao wenyewe.....
 
Back
Top Bottom