Kilaini: Kikwete bado ni chaguo la Mungu

Yuda Iskariot alichaguliwa na Yesu na akawa mwanafunzi wake miaka mitatu lakini alimsaliti Yesu,Kikwete naye baadhi ya mawaziri wanamsaliti.
 
Wazo lake lakini sisi safari hatutaburuzwa,angekuwa chaguao la mungu tungelikuwa wote kwenye ufalme,katuacha solemba halafu KIlaini anakuja anabwabwaja kutuambia maneno ya zamani yaliyochuja mmh atuache tuchgue tutakeyeona anatufaa
 
Kilaini yuko sawa kabisa , wanaomuangusha Kikwete ni wasaidizi wake ambao anaona uvivu kutimua nadhani anahofia upweke maana wengi ni rafikii zake
 
Nataka nimkumbushe Askofu juu ya tukio lililotokea Mwanza mwaka 2005 wakati wa kampeni za Kikwete kugombea urais, JK aliangushwa chini na mganga wa kienyeji , mganga yule alipohojiwa na polisi alisema kuwa hakuwa na nia ya kumdhuru JK bali alikuwa anazuia zoezi la kumzindika jk kwani kwa taratibu za taaluma yao mambo hayo hayafanyki hadharani.Swali kwa Askofu, jee Mungu anapenda ushirikina? Kwa vile ushirikina ni chukizo kwa Mungu aliye umba mbingu na nchi ni dhahiri JK hakuwa chaguo la Mungu, bali ni chaguo la miungu mingine anyoitumikia.
 
Askofu Kilaini na kauli tata kuhusu Kikwete

skofu Kilaini na kauli tata kuhusu Kikwete

lC.gif
Ncheme Nchicheme?​
Mei 26, 2010
rC.jpg

KWA tafsiri ya Askofu, Dk. Methodius Kilaini, kiongozi mwenye hadhi ya kuitwa chaguo la Mungu ni yule aliyechaguliwa kwa kura nyingi na wananchi....anayependwa kama ilivyo kwa Rais Jakaya Kikwete.
Kikwete alichaguliwa kwa kura zaidi ya asilimia 80 mwaka 2005. Na kwa mujibu wa Kilaini, huyu ni chaguo la Mungu.
Tafsiri ya kauli hii ya Dk. Kilaini ambayo imejitokeza wiki hii kwenye moja ya magazeti nchini ni kwamba chaguo la Mungu ni yule mwenye kujizolea kura nyingi, kipenzi cha watu. Sijui bwana..., labda hata Mwenyekiti wa Klabu ya Simba aliyechaguliwa hivi karibuni kwa kura nyingi ni chaguo la Mungu au Mwenyekiti wa Yanga aliyewahi kuchaguliwa kwa kura nyingi kuliko wenzake naye aliwahi kuwa chaguo la Mungu.
Lakini kauli ya Dk. Kilaini sambamba na tafsiri yake ni upande mmoja wa CD, upande mwingine wa CD ni kumbukumbu ya kauli zake kuhusu masuala mbalimbali ya uongozi nchini.
Hebu tujikumbushe mwaka 2005. Wenye kumbukumbu watakumbuka kuwa Askofu Kilaini alidai Kikwete ni chaguo la Mungu, kabla hata ya upigaji kura kufanyika.
Alitoa kauli yake mapema. Alitamka Jakaya Kikwete ni chaguo la Mungu kabla hata hajachaguliwa na bila shaka wagombea wengine wa wakati huo, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na Freeman Mbowe wa CHADEMA, hawa kwa mujibu wa DK. Kilaini hawakuwa chaguo la Mungu...usiniulize, watajijua wenyewe walikuwa chaguo la nani.
Hoja ya kwanza ya msingi ya kuzingatia ni kwamba; Kilaini alitamka Kikwete chaguo la Mungu kabla ya upigaji kura na hatimaye mshindi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Leo pia anasisitiza ni chaguo la Mungu kabla hata ya upigaji kura, achilia mbali kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea.
Kwa mfano, kama mwaka 2005 alimtangaza Kikwete chaguo la Mungu kwa sababu pengine za kujaa watu kwenye mikutano yake, basi wagombea wengine wangestahili kuwa chaguo la Mungu katika baadhi ya mikoa, wilaya au vitongoji kwa kuwa huko walijaza watu, ambao wengine walitaka kushuhudia helkopta.
Lakini leo, inaelekea kutimia miaka mitano tangu amtangaze Kikwete chaguo la Mungu, anarejea na kusisitiza kauli hiyo na kutoa tafsiri yenye msingi kuwa anapendwa kwa maana ya kuwa na kura nyingi.
Hapa ndipo kwenye utata kuwa kauli yake hii inazingatia msingi upi? Anawezaje kutamka ni chaguo la Mungu wakati hata uchaguzi haujafanyika ili kuthibitisha kuwa anakubalika na mamilioni ya Watanzania? Mhh, au ni kauli ya kubahatisha na kuandaa mazingira fulani?
Anatafsiri kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, isipokuwa wasaidizi wake ndiyo wanaomwangusha na kwamba akichaguliwa tena, awateme. Je, Mungu ametelekeza ‘chaguo’ lake likizingirwa na wazembe?
Sitaki kushabikia mjadala kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu au la. Nasisitiza kuwa viongozi wakubwa wakubwa, wawe makini na kauli zao lakini pia watunze kumbukumbu za kauli hizo.
Ikumbukwe kuwa ni Kanisa Katoliki ambalo limetoa ilani au waraka wa uchaguzi na kuanisha sifa za mgombea anayestahili kuchaguliwa bila kutaja majina.
Lakini sasa kwa kauli ya Kilaini ni wazi, anaweka mwelekeo ambao ni kinyume hata cha ilani au waraka wa Kanisa lake Katoliki ambalo kupitia Chama Cha Wanataaluma Wakristo (CPT) kilitoa waraka.
Lakini katika mtiririko huo huo wa kumbukumbu, baadhi watakumbuka alichotamka Kilaini katika Kongamano la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, ukumbini Karimjee, Dar es Salaam...Jiji ambalo lina Ikulu, wanaharakati, wanasiasa, wasomi na wanamazingira hodari lakini likinuka kwa uchafu na barabara zinazogeuka mitaro wakati wa mvua.
Katika kongamano lile, Kilaini alisema nchi inatembea bila nguo akimaanisha masuala ya maadili na uongozi hayajatulia na kwa maana hiyo, kama hali ni hiyo unaweza kujiuliza je, hata hilo chaguo la Mungu ‘limetulia’? au ndio wasaidizi walioitoa nchi nguo? Ncheme Nchicheme?




Askofu Kilaini: Kikwete ameelemewa na mafisadi

lC.gif
Aristariko Konga​
Disemba 12, 2007
rC.jpg

ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, anasema baadhi ya viongozi wa serikali wanapokea pesa kutoka kwa wawekezaji wa nje, na hivyo kumfanya Rais Jakaya Kikwete awe na wakati mgumu katika kuongoza vita dhidi ya ufisadi wa kimataifa.
kilaini_1.jpg


Askofu Methodius Kilaini
Askofu Kilaini aliiambia Raia Mwema katika mahojiano maalum, yaliyofanyika wiki iliyopita, kwenye ofisi yake iliyoko katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Alisema kwamba anamwonea huruma Rais Kikwete kwa kuwa lengo lake jema, la kupambana na rushwa kubwa au ufisadi wa kimataifa, linahujumiwa na baadhi ya viongozi walioko chini yake, wenye dhamana za kusaini mikataba na wawekezaji wa nje, ambao hupewa pesa nyingi ili kuwapendelea wageni hao.
Alisema kwamba wawekezaji hao wa kigeni huja nchini na pesa nyingi kwa lengo la kuwekeza, lakini huwa na malengo mengine zaidi na hivyo kuwahonga pesa baadhi ya viongozi walioko madarakani, ili walinde maslahi yao.
"Wanakuja na vitu vyao na mapesa mengi sana. Sasa wanapofika hapa wanayatumia mapesa haya kuwapa viongozi walioko madarakani.
Viongozi wa aina hii, ambao ndio walipaswa kumsaidia Rais Kikwete, ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kumkwamisha.
"Hao ndio wanaofanya dhamira nzuri ya Rais Kikwete, ya kupambana na rushwa hii kubwa, iwe ngumu kuitekeleza. Inabakia tu kusikia kelele za rushwa kwenye mahakama zetu hizi ndogo, ikiwahusu watu wadogo.Hii haitoshi," anasema.
Kilaini anasema kwamba, ufisadi huu wa kimataifa (rushwa kubwa) unalindwa sana na viongozi hao waliohongwa, kiasi kwamba mtu akijaribu kulinda maslahi ya taifa, hushurutishwa na wakubwa wake kwamba anapaswa kunyamaza.
"Ufisadi wa kimataifa, ambao ndio unaolisumbua taifa hivi sasa, unalindwa sana na walioko madarakani. Mtu akijaribu kuingilia kati anaambiwa 'nyamaza' na walioko juu yake. "Kwa hiyo serikali yetu ina kazi kubwa sana, na hasa Rais wetu Kikwete, ambaye ameonyesha moyo wa kutaka kupambana na tatizo hilo.
Ana kazi kubwa kwa sababu kuna watu wanashirikiana na wawekezaji hawa wa nje ili kujinufaisha wao. Ni kazi ngumu sana kwake. Mafanikio yako mbali sana nasi."
Askofu anasema kwamba vita dhidi ya ufisadi wa kimataifa inakuwa ngumu sana kwa sababu mikataba yenyewe ina usiri mkubwa, kiasi kwamba hata wale ambao wanatarajiwa kuwa wa kwanza kuupiga vita, wanajikuta hawana taarifa mapema kutokana na mazingira ya kificho.
"Wale ambao wanapaswa kuwa wa kwanza kupiga vita suala hili, na wenye dhamana hiyo, wanashindwa kupata taarifa na hata wanapokuja kuzipata, wanakuwa wamechelewa sana na mambo yamekwisha kufanyika na kuleta athari.

jk_1.jpg


Rais Jakaya Kikwete
"Kutokana na usiri huu, kazi ya kupigana vita na ufisadi inakuwa ngumu sana. Hapa ndipo dhamira ya Rais Kikwete inakuwa vigumu kutekelezeka.
Hata hivyo, Askofu Kilaini anasema suala la ufisadi wa kimataifa halikujitokeza wakati wa utawala wa Rais Kikwete, bali lilianza kujitokeza wakati wa utawala wa Awamu ya Tatu, wakati Rais Benjamin Mkapa alipofungua zaidi milango ya uwekezaji wa nje.
Mara kadhaa wabunge wamekuwa wakilalamika ndani ya Bunge, kwamba mikataba hiyo ingekuwa inawekwa wazi mbele yao, lakini upande wa serikali umekuwa ukipinga dhana hiyo kwa madai kuwa mambo mengi ni ya siri baina ya wale wanaoingia kwenye makubaliano ya mkataba.
Katika hotuba yake ya kwanza bungeni, Rais Kikwete alionyesha kuguswa na mikataba mbalimbali na hivi karibuni amebainisha kwa kusema kwamba mikataba aliyoizungumzia wakati ule ilikuwa ni ile kati ya serikali na makampuni ya madini na tayari amechukua hatua kwa kuunda tume ya serikali na baadaye kamati ya kupitia upya mikataba ya madini.
Hata hivyo, Mkapa alipoingia madarakani kwa 'gia ya Mr Clean' aliunda Tume ya Kero za Rushwa mara tu alipoingia madarakani, tume iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba, lakini matokeo ya tume hiyo ya kihistoria hayajaonyesha kuzaa matunda yaliyokusudiwa. Badala yake imekuja kubainika kwamba kipindi cha utawala wa awamu ya tatu kilisheheni rushwa kubwa kubwa ambayo imeliingiza taifa katika matatizo makubwa.
Kabla hata ya kuanza kwa kipindi cha pili cha utawala wake, Mkapa alijiingiza katika biashara akiihusisha familia yake na baadaye mawaziri wake na mfano maarufu ni ule wa kujihusisha kwake na ununuzi wa mradi mkubwa wa mkaa wa mawe wa Kiwira.
Mkapa kupitia kampuni yake ya ANBEM Limited alianzisha kampuni (kabla ya kujitoa) iitwayo TANPOWER kwa kushirikiana na kampuni ya Waziri wake, Daniel Yona, kampuni iliyonunua hisa za mradi wa Kiwira, mauziano ambayo yamezua gumzo kubwa hasa ikizingatiwa kwamba kwa wakati huo wote walikuwa madarakani kama Rais na Waziri wa Nishati na Madini.
Hivi karibuni, wanasiasa wa kambi ya upinzani na zaidi Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, waliibua kile kilichoitwa 'orodha ya mafisadi' ambayo pamoja na mapungufu yake, iliibua mjadala mkubwa katika siasa za Tanzania kiasi cha kuwachanganya viongozi na watendaji wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Tuhuma hizo, mbali ya kutaja majina ya baadhi ya watu, ziliibua hoja kadhaa ambazo baadhi zimejibiwa na baadhi hadi leo hazijatolewa maelezo, angalau ya kubabaisha. Baadhi ya mawaziri na watendaji walitishia kwenda mahakamani lakini hadi sasa hakuna taarifa rasmi za kufunguliwa kesi mahakamani.
 
Ya Mungu tumwachie mwenyewe Mungu, tushughulike na ya kwetu"Kaisari"!!!! Mungu anafahamu chaguo lake ni nani!!! Kiongozi yeyote anayechaguliwa kidemokrasia anakuwa mtawala na watawal Mungu ndiye anayewaweka!!! Mungu anamakusudi yake ambayo kamwe hayafanani na ya kwetu wanadamu!!!
 
Nadhani hapa ameongea kama Kilaini na si kiongozi wa dini

Kilaini alishajitoa kama kiongozi wa dini kwa kutoa kauli tata zisizoendana na maandiko matakatifu. Hii ndio moja ya sababu za kumuondoa Dar na kumpeleka Bukoba !! Chaguo la Mungu haliwezi kufanya mambo ya kiharamia ya kuwalinda mafisadi wanaowaibia maskini; hilo linakuwa chaguo la Shetani.!!
 
Sasa ni dhahiri zaidi kwamba CCM hakuna chaguo la Mungu. Uteuzi wa kugombea nafasi za kuchaguliwa ndani ya CCM zimejaa vituko, rushwa, fujo, fitina, udanganyifu, uwongo, n.k. Chama cha CCM sasa kimekuwa ni kimbilio la kupata uongozi kwa njia za hila na ufisadi. CCM inaatamia mafisadi kama nguzo kuu ya chama. Baada ya uteuzi wa wagombea matendo hayo ya CCM watayafanya dhidi ya vyama vya upinzani. Sasa watu tunajiuliza Mungu gani wa sasa ambaye ni wa fujo, fitana, udanganyifu, wivu, rushwa, ufisadi. Tuwaulize wapambe wa CCM haya matendo yanaambatana na changuo la Mungu? Tuliite panga ni panga ni siyo kisu kikubwa. CCM yote hakuna chaguo la Mungu, iwe udiwani, ubunge na urais, n.k.
 
ni kweli Mkono wa Mungu hapo hauwezi kuwepo. kwasababu watu kibao kwa sasa wanaota ndoto za kuwa wabunge na kuwa viongozi mbalimbali wa CCM, ndipo sasa hila vituko, ubabe wa physic ,na nguvu za giza vinaanza.
inasikitisha pale ambapo experts (Walimu, madaktari, wakufunzi, mainjinia ....) nao wanaacha silaha na kuanza kutafuta uongozi.
tujiulize kuna nini? kama si hela zetu zinatafunwa huko na mbaya zaidi ni pale ambapo ni hela za watu masikini sana.
Sasa fikiri kama Docta, na mwalimu wataondoka, na hao wanaobaki mishahara haipandi si ndio mixed operations za ubongo badala ya kucha
zitaongezeka!
Kimsingi pesa zetu zinatafunwa na watu bila jasho, ndiyo maana Malaria Sugu naye anataka kuhamia kwenye siasa.
kweli Kwenye rushwa na fitina mkono wa Mungu Haupo!!!
 
ni kweli Mkono wa Mungu hapo hauwezi kuwepo. kwasababu watu kibao kwa sasa wanaota ndoto za kuwa wabunge na kuwa viongozi mbalimbali wa CCM, ndipo sasa hila vituko, ubabe wa physic ,na nguvu za giza vinaanza.
inasikitisha pale ambapo experts (Walimu, madaktari, wakufunzi, mainjinia ....) nao wanaacha silaha na kuanza kutafuta uongozi.
tujiulize kuna nini? kama si hela zetu zinatafunwa huko na mbaya zaidi ni pale ambapo ni hela za watu masikini sana.
Sasa fikiri kama Docta, na mwalimu wataondoka, na hao wanaobaki mishahara haipandi si ndio mixed operations za ubongo badala ya kucha
zitaongezeka! kweli Kwenye rushwa na fitina mkono wa Mungu Haupo!!!

Sasa hapo chaguo la Mungu linatoka wapi CCM? Hakuna chaguo la Mungu CCM, simwoni hata mmoja
 
1689bp1.jpg


UBISHI TUUU: HUU UTITIRI WA MASHANGINGI SIO UTHIBITISHO WA MAISHA BORA?SASA HIYO NI AWAMU YA KWANZA.AWAMU IJAYO NI BAJAJ KWA WAJAWAZITO NCHI NZIMA

Maji+1%5B1%5D.jpg

MAJI BWERERE

MAISHA+BORA.jpg

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YAMEWEZEKANA

HURUMA.jpg

USHAHIDI WA MAISHA BORA UNAONEKANA HATA KWA WATOTO WADOGO



ADHA+YA+MAJI.JPG

YOU SEE, TATIZO LA MAJI MIJINI NA VIJIJINI LIMEPATIWA UFUMBUZI WA KUDUMU
USAFIRI+WA+WANAFUNZI.jpg

TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI MIJINI LIMEMALIZWA.MNATAKA MAISHA BORA YAPI ZAIDI YA HAYA?



POLISI+MSIMBAZI.jpg

MNAONA?POLISI WENYE MAKAZI DUNI SASA WANA SWIMMING POOL HAPO MSIMBAZI POLICE FLATS.MAISHA BORA KWA POLISI YAMEPELEKEA WAACHE KUDAI RUSHWA NA KUBAMBIKIZA KESI KWA WALALAHOI

zjgfo4.jpg
KURA ZA ALBINO ZIMEZAA MATUNDA.HUYO MGOMBEA WA CCM WANAYEDAI NI MTUHUMIWA WA BIASHARA YA VIUNGO VYA ALBINO NI SIASA ZA MAJITAKA TU


25p4yv6.jpg
HATA SUPAMODO NAOMI CAMPBELL ALIPOTEMBELEZA TANZANIA ALIRIDHISHWA NA HALI ALIYOKUTA WODI YA AKINAMAMA.NA AKATOA MACHOZI YA FURAHA


MATREKTA+KILIMO+KWANZA.JPG
BARABARA ZETU NI MARIDADI.TUMELETEWA MATREKTA MENGI MNO KWA KILIMO KWANZA HADI INABIDI YAFANYE KAZI YA KUVUTA MALORI.EBO!KWANI CHA AJABU NINI TREKTA KUVUTA LORI?NI FERI ZA NCHI KAVU HIZO


MATOPE.JPG
CHAGUA KIKWETE NA CCM KWA BARABARA BORA.NA 2010-2015 BARABARA KAMA HIYO HAPO JUU ZITAKUWA UPGRADED TO FLYOVER.


ELIMU+CHINI+TENA.jpg
SERIKALI YA KIKWETE IMEWAJALI SANA WANAFUNZI NA KUWANUNULIA MADAWATI BORA MNO HADI YANAWACHOSHA KUYAKALIA NA KUAMUA KUKAA SAKAFUNI

KIBANO+UDSM.jpg
HAPANA.KOSA LA MSOMI HUYO WA CHUO KIKUU ANAYEFUKUZWA NA FFU NI KUGOMA KUCHUKUA HELA ZA KUJIKIMU ZILIZOINGIZWA KWENYE AKAUNTI YAKE KABLA HAJAWASILI CHUONI.HAPO ASKARI WA FFU ANAMHAMASISHA MSOMI HUYO AENDE BENKI.CHAGUA KIKWETE USOME KWA RAHA MUSTAREHE


elimu+chini+.jpg
NDIO MAANA RAIS MPENDWA JAKAYA KIKWETE ALISEMA MIMBA ZA WANAFUNZI NI KIMBELEMBELE CHAO TU.ANGALIA MWENYEWE MAZINGIRA BORA KABISA YA NAMNA VIJANA WETU WANAVYOPATA ELIMU.KIKWETE OYEEE


kikwete+na+pipi.JPG
BAADA YA MABILIONI YA KIKWETE,NA KAGODA KUREJESHA MABILIONI,SASA MAISHA BORA NI KWA MWENDO WA PIPI KWA KILA MTOTO.YAH,PIPI KWANZA KISHA LAPTOP KWA KILA MWANAFUNZI.HALAFU HUYO SLAA ANAPOSEMA ATATOA ELIMU YA BURE KWANI MIE NAUZA HIZI PIPI?


Jakaya-safarini-218x300.jpg
SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE.KWANI MLIPONICHAGUA MLITAKA NIOTE MATENDE IKULU?

rostam_1.jpg
MFANO HAI WA AMANI NA UTULIVU


SAFARI+MOJA.JPG
ZAPATERO ANAELEKEA KUSHANGAA: HIVI KAMA HUYO JAMAA ANA MAWAZO YA HALI YA JUU KIASI HIKI KWANINI BADO NCHI YAKE NI MASIKINI?NO,HAPO KIKWETE ANAHUBIRI KUHUSU CHANZO CHA UMASIKINI WA AFRIKA JAPO HAFAHAMU KWANINI TANZANIA NI MASIKINI


AKINAMAMA.JPG
AKINAMAMA WAMEPEWA KIPAUMBELE CHA HALI YA JUU KATIKA MIPANGO YA SERIKALI YA KIKWETE.PICHA INAWAONYESHA KAMA WANA MAJONZI LAKINI UKWELI NI KUWA WAMESHIKWA NA BUTWAA KUTOKANA NA KAZI NZURI YA CHAGUO LA MUNGU KIKWETE





TwinTowers.jpg
MMENG'ANG'ANIA TU SUALA LA EPA NA KAGODA NA KUSAHAU MINARA PACHA.BY THE WAY,FEDHA ZA EPA HAZIKUIBWA BALI ZILIAZIMWA TU,NDIO MAANA NILIWASIHI TULIOWAAZIMA WAZIREJESHE.WALIOAZIMWA WANAREJESHA IN KIND KWA KUCHANGIA KAMPENI ZA CCM


Richmond.jpg
TEH TEH TEH,NICHEKE MIE.KIKWETE MTU BOMBA SANA.SIE TUMEKUJA NA KABRASHA TUPU LEO HII TUNA MABILIONI KWENYE AKAUNTI.ASANTE DOWANS KWA KUTURITHI,ASANTE KARAMAGI NA MSABAHA.ASANTE WATANZANIA KWA KUMWAMINI KIKWETE.SI MNAONA SASA TATIZO LA UMEME NI HISTORIA KAMA ALIVYOAHIDI CHAGUO LA MUNGU KIKWETE?
regina.jpg

MWAKYEMBE NA TUME YAKE NI ROHO MBAYA TU.KAMA MUME WANGU LOWASSA ALIHUSIKA NA UFISADI WA RICHMOND MBONA KIKWETE AMEKUJA JIMBONI KUMPIGIA DEBE?
lowassa.jpg

TATIZO LENU WATANZANIA MNA KUMBUKUMBU HAFIFU.MMESAHAU ENZI ZA Boyz II Men?MIE NA JAKAYA HATUJAFAHAMIANA MTAANI.MNABISHA?SI MMEONA JINSI MAJUZI ALIVYOMWAGIA SIFA JIMBONI MONDULI?




SAFARI+ZAIDI.JPG

MNASEMA NASAFIRI SANA?KWANI MLIPONICHAGUA MLIKUWA HAMFAHAMU KUWA NILIPOKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NILIKUWA NASAFIRI SANA?ACHENI UZUSHI,SAFARI ZANGU ZITAILETEA TANZANIA SIFA YA KUVUNJA REKODI YA VASCO DA GAMA.

SAFARI+ZAIDI.JPG
MNASEMA NASAFIRI SANA?KWANI MLIPONICHAGUA MLIKUWA HAMFAHAMU KUWA NILIPOKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NILIKUWA NASAFIRI SANA?ACHENI UZUSHI,SAFARI ZANGU ZITAILETEA TANZANIA SIFA YA KUVUNJA REKODI YA VASCO DA GAMA.


Bartlett+with+Jakaya+Mrisho+Kikwete+and+wife+at+Mystic+Mountain.jpg
MTAJIJU....ACHE MIE NIBEMBEE


KIKWETE+MWANAE.jpg
JIJENGE HUKO UVCCM.SI UMEONA FAMILIA YA BUSH ILITOA MARAIS WAWILI KAMA YA KABILA HUKO DRC?BASI NA WEWE JIANDAE.MIE NAITWA CHAGUO LA MUNGU,WEWE UTAITWA CHAGUO LA BABA
JK+RIZI+WANI+CLASS.jpg
WE KATUNI HUELEWI SOMO LIPI TENA?YANI UNAKUWA KAMAMIE NISIYEELEWA KWANINI TANZANIA NI MASIKINI!


dance+kikwete.jpg
PICHA YA JUU NA YA CHINI: CHAGUO LA MUNGU DANCING.BY THE WAY "Never Trust a Spiritual Leader who cannot Dance".-Mr Miyagi,The Next Karate Kid,1994



MAKAMBA.jpg
HUYU SLAA ANATAKA KUNIWEKEA MCHANGA BADALA YA UBWABWA KWENYE SAHANI HII.HIZI HABARI ZA MIE KUFUKUZWA UALIMU ZA NINI TENA MUDA HUU?
Makamba+%281%29.jpg
WANAKUJA NA USHAHIDI NINI?WANATOKEA HUKU AU KULE?ANYWAY,HAWAWEZI KUTHIBITISHA LOLOTE
makamb.jpg
MGOSI,UNAKUMBUKA SIKU ZILEEEE KATIKA SHULE ILEEE...BASI SLAA KAINYAKA HIYO ISHU.
 
Mwaka 2005 maaskofu walijifunga vibwebwe na kufanya kile ambacho kisingetarajiwa kifanywe na viongozi wa dini. Bila kujali kuwa walichokuwa wanakifanya ni kinyume kabisa na maadili ya 'FAIR PLAY', yaani kutocheza rafu ya makusudi, walijitoa hadharani na kudai kuwa Taifa lilikuwa linahitaji kiongozi mwadilifu na mcha Mungu; na huyo hakuwa mwingine bali Jakaya Kikwete kwa kuwa huyo ndiye aliyekuwa 'CHAGUO LA MUNGU'!

Hakuna shaka yoyote kuwa kwa kitendo kile maaskofu walicheza rafu ya makusudi. Ni kwa nini nasema hivi? Nasema hivi kwa sababu kwa jinsi mfumo wa uendeshaji wa dini ya kikiristo ulivyo, na hasa kwa dhehebu la Roman Catholic, mlei, yaani muumini wa kawaida, mahusiano yake na muumba wake ni lazima yapitie kwa kiungo ambaye ni padri au askofu. Wabunifu wa utaratibu huu wameweka kanuni mbili muhimu ambazo zinawahakikishia utiifu wa waumini wao kwa muda wote.

Kwanza ni kanuni ya kujumuika kundini. Kwa mujibu wa kanuni hii utahesabiwa kuwa wewe ni muumini wa kweli na mwenye haki za kiroho sawa na waumini wengine, pale tu viongozi wa kanisa watakapojiridhisha kwamba umo 'kundini'; kwa maana ya kuwa unashiriki kikamilifu katika shughuli za kanisa lako chini ya miongozo ya padri wako. Kwa kutumia kanuni hii, wale wanaokwenda kinyume na miongozo ya mapadri na maaskofu wao hujikuta wakipewa adhabu ya kutengwa; na hii ni adhabu kubwa sana kwa sababu unatengwa ukiwa hai mpaka maiti yako!

Kanuni ya pili, ni ile ya mapadri na maaskofu kuwa na mamlaka ya kupokea toba za waumini wao. Kwa mujibu wa kanuni hii, waumini wakifanya dhambi, suala la toba siyo la binafsi kati ya mfanya dhambi na muumba wake, bali ni lazima toba ipitie kwa padri au askofu; ambaye baada ya kusikiliza ungamo lako ana mamlaka ya kutamka kuwa umesamehewa.

Mfumo huu unaozuia mawasiliano ya moja kwa moja kati ya muumini na muumba wake umeweza kujenga utii mkubwa sana wa waumini kwa mapadri na maaskofu wao na kusababisha kanisa kuwa na nguvu ya ajabu. Nguvu hii inatokana na ukweli kuwa kwa kutumia mfumo huu mapadri na maaskofu wamekuwa na mamlaka makubwa sana juu ya waumini wao kuhusu nini wafanye na nini wasifanye.

Maaskofu waliposema kuwa JK ni 'CHAGUO LA MUNGU' ilikuwa ni rafu ya makusudi kwa sababu walikuwa wanajua fika kuwa kwa mamlaka waliyonayo juu ya waumini wao tamko lao lilikuwa ni agizo kwa waumini wao kuhakikisha kuwa siku ya kupiga kura, kura zao zinaenda kwa JK.

Kwa mkristo mkereketwa kutotii agizo la askofu wake siyo tu kuwa ni dhambi, lakini pia ni kutafuta kufukuzwa kutoka 'kundini'. Sasa nani yuko tayari kufanya 'dhambi' ya waziwazi kabisa kama hiyo na kutengwa akiwa hai hadi maiti yake?

Tatizo la kanisa kuwachagulia waumini wao viongozi ni la kihistoria na wala halijajifunga katika mipaka ya kijiografia. Wakina Vladmir Lenin kule Urusi mwanzoni mwa karne ya ishirini walipokuwa wanafanya jitihada za kuwazindua wafanyakazi na wakulima wa huko kuupindua mfumo wa kibwenyenye uliokuwa unawatawala na kuwanyonya, kikwazo chao kikubwa kilikuwa ni viongozi wa kanisa.

Utiifu wa walalahoi hao wa kirusi kwa viongozi wao wa kanisa ulikuwa mkubwa kiasi cha kumlazimisha Lenin kutamka hadharani kwa uchungu kuwa 'DINI NI KASUMBA YA WATU'. Kasumba kama vilivyo vilevi vingine, kazi yake kubwa ni kumzuia mtu kujitambua na kuyatambua mazingira yake katika uhalisia wake.

Wakati vichwa vikiwauma wakina Lenin na Trosky kule Urusi jinsi ya kufuta kasumba ya ukristo kwenye akili za Warusi, kasumba hiyo pia ilikuwa imekamata akili za watu wengi katika mataifa mengine ya Ulaya. Kwa mfano, pamoja na kwamba kule nchini Uingereza hali ya wafanyakazi wengi ilikuwa ni duni sana, jitihada za chama chao cha Labor kushika madaraka ya dola ili kuboresha hali zao za maisha zilikuwa

zinakwamishwa na wafanyakazi wenyewe! Makada wa Labor walikuwa wakitukanwa, kubezwa na hata wakati mwingine kupigwa. Hali kwa makada wa Labor waliokuwa wanaendesha 'Operesheni Zinduka' hiyo iliendelea kuwa mbaya hadi mwaka 1914 pale kitabu cha hadithi cha mwandishi Robert Tressel, kinachoitwa 'The Ragged Trousered Philanthropists', yaani, 'Wasamaria wema waliovaa viraka', kwa tafsri isiyo rasmi, kilipochapishwa.

Kwa kifupi kitabu hiki kilikuwa kinawazungumzia wafanyakazi wa Uingereza ambao hali zao za kimaisha zilikuwa duni sana. Kilikuwa kinawaashangaa ni kiasi gani walikuwa HAWAJIONEI au KUWAONEA HURUMA WATOTO WAO kwa kuleta mabadiliko ya kisiasa, ukizingatia kuwa uwezo wa kufanya hivyo walikuwa nao kupitia kura zao.

Juu ya hali hiyo, mwandishi wa kitabu hicho, Robert Tressel, alielekeza lawama zote kwa kwa kanisa. Alilituhumu kuwa lilikuwa linatumiwa na watawala mabwenyenye na wakandamizaji waliokuwa wameshikilia mamlaka ya kisiasa kuwadanganya waumini wao - kuwa kuendelea kuwatii waliokuwa na mamlaka ya kisiasa juu yao ni KUMTII MUNGU - kwa sababu ati mamlaka zote za kisiasa zimewekwa na Mungu! Kupitia mhusika mkuu ndani ya hadithi hiyo, Tressel aliwaambia wafanyakazi kuwa njia nyepesi ya kuthibitisha kuwa makasisi wao walikuwa wanasema uwongo ni kuwapa changamoto ya kunywa sumu hadharani kwa sababu Bibilia inasema wazi kuwa muumini wa kweli kabisa hata akinywa sumu haitamdhuru!

Wachambuzi wa siasa za Uingereza za kipindi hicho cha mwanzoni mwa karne ya ishirini wanaamini kuwa kitabu hicho cha Tressel kilikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa chama cha Labor pale chama hicho kiliposhinda kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuunda serikali mnamo mwaka 1924.

Mkakati wa watawala na mabwenyenye ya Ulaya kutumia ukristo kama 'kasumba' ya kuwaleweshea watu ili watawalike na kunyonywa kwa urahisi haukuishia kwenye mipaka ya bara hilo. Wakati tawala za Ulaya zilipokutana na kuamua kugawana bara la Afrika, wamishenari walitumiwa kama 'advance party', yaani wasafisha njia.

Kutokana na uzoefu ziliokuwa nao, tawala hizo zilijua fika kwamba itakuwa ni rahisi zaidi kwa wenyeji wa bara hili kuukubali ukoloni iwapo wenyeji hao tayari watakuwa wametiwa kwenye ukristo.

Afrika Mashariki ni mfano mzuri. Mnamo mwaka wa 1863, makasisi wa Holy Ghost Fathers walitua Zanzibar - nchi ya kiislamu – na kuomba waruhusiwe kufungua kituo chao. Tukio hili ambalo lilikuwa la kwanza la kurasimisha ukristo katika ukanda wa Afrika Mashariki lilitokea takriban miaka 20 kabla ya mkutano wa Berlin wa mwaka 1884. Mkutano huu ndio ulioigawa rasmi ardhi ya Afrika katika mapande mapande na kila tawala iliyohudhuria mkutano huo kukabidhiwa kipande au mapande yake ili kusimika ukoloni.

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia, Marekani ilianza kuweka shinikizo kwa mataifa ya Ulaya ili yatoe uhuru wa bendera kwa makoloni yao; na kupisha njia ya kusimikwa kwa ukoloni mamboleo. Kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni mkongwe, ukristo ulitumiwa tena kama mbeleko ya kuubebea huo ukoloni mamboleo.

Zilitumika juhudi kubwa kuhakikisha kuwa takriban viongozi wote wa mwanzo wa zile nchi ambazo zilikuwa zimekabidhiwa uhuru wa bendera ni wakristo, ambao pamoja na mambo mengine, wana jukumu pia la kulinda maslahi ya ukristo dhidi ya yale ya Taifa.

Tanzania ni mfano mzuri. Pamoja na jitihada kubwa sana zinazoendelea usiku na mchana za kumtukuza Mwal. Julius Kambarage Nyerere, Nyerere alikuwa ni mmoja wa viongozi hao. Mwandishi Jan P van Bergen katika kitabu chake Development and religion in Tanzania, amefichua taarifa za kikao cha siri Ikulu ya Dar es Salaam mnamo Agosti 3, 1970 kati ya Rais Julius Nyerere, Padri Robert Rweyemamu na muwakilishi wa Papa, Giovanni Cerrano. Kwa mujibu wa van Bergen, katika kikao hicho Nyerere aliwaeleza viongozi wake wa dini kuwa ameunda idara ya elimu ya siasa katika TANU na amemuweka Padri aiongoze kwa sababu ya imani yake madhubuti. Aliwaeleza pia kuwa katika Kamati kuu ya chama ameweka Mapadri lengo likiwa kulipa Kanisa fursa na uwezo mkubwa hapa Tanzania.

Kutokana na matendo na kauli za maaskofu mbalimbali katika kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea hivi sasa inaonekana dhahiri kuwa rais Kikwete hatakiwi tena na maaskofu. Moja ya matendo ya dhahiri kabisa kufanywa na maaskofu yanayoonyesha msimamo wao ni lile tukio la kuukataa mwaliko wake wa kufuturu naye kule Mbeya wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani uliomalizika hivi karibuni.

Lakini ukitaka kujua kuwa kweli safari hii hawamtaki, rejea matamshi ya askofu Zakariah Kakobe wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwa waumini wake, ambapo pia aliitumia fursa hiyo kufuta ibada katika makanisa yake yote siku ya Jumapili ya uchaguzi, ili tu awe na uhakika kuwa kila muumini wake hatakuwa na kisingizio cha kuacha kwenda kupiga kura.

Kakobe amenukuliwa akiwataka waumini wake wasitilie maanani tabia binafsi za wagombea zinazohusu mahusiano yao ya kingono, na badala yake waangalie kile ambacho amekiita, 'kipaji' cha mgombea. Pamoja na kwamba hakumtaja kwa jina, lakini kwa kuzingatia kuwa kati ya wagombea wote wanaowania nafasi ya uraisi kwa sasa, ni Dr. Slaa pekee ndiye aliyekumbwa na kashfa ya ngono, moja kwa moja inaonyesha kuwa Kakobe alikuwa anawapa maagizo waumini wake wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura na kumpigia Dr. Wilbrod Slaa.

Jambo la kushangaza sana kwa ndugu zangu maaskofu ni kwamba, ukiondoa mambo kadhaa yanayomwongezea sifa, 'Kikwete chaguo la Mungu' wa 2005, ndiye huyo huyo ambaye tunaye mwaka 2010. Hata hivyo tofauti na Kikwete wa 2005, hivi sasa Kikwete amekomaa zaidi, kwa maana ya kwamba ameongezeka umri na pia amepata uzoefu wa ziada. Katika tamaduni zetu za Kiafrika 'Mtu mzima ni dawa' , na katika taratibu za uendeshaji wa mambo 'uzoefu wa kina' ni jambo linalotukuzwa.

Aidha Kikwete na serikali yake wameweka mtandao mkubwa wa shule za sekondari za kata na kuongeza kwa kiwango kikubwa sana nafasi za masomo katika taasisi za elimu ya juu, hususan kupitia ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma kinachochukua zaidi ya wanafunzi 40,000 na kile ambacho kiko mbioni kujengwa mkoani Mara kitakachochukua idadi hiyo hiyo ya Wanafunzi. Ni wazi kabisa kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo mtandao huu wa shule za sekondari na vyuo vikuu utakuwa umefuta kabisa pengo kubwa la kielimu lililopo siyo tu kijiografia, lakini pia kati ya jamii mbalimbali nchini.

Miaka kumi ijayo jamii ya Waislamu haitakuwa tena na sababu za kusema kuwa serikali inawapendelea Wakristo katika nyanja ya elimu; na viongozi wa serikali nao hawatakuwa tena na wakati mgumu wa kuwaambia Waislamu kuwa 'tatizo lao ni la kihistoria' kila wanapofikishiwa malalamiko ya Waislamu. Bila shaka hali hii siyo tu kuwa itaimaarisha mshikamano nchini, lakini pia itakuwa imeweka msingi mzuri kutuhakikishia kuwa amani tuliyonayo nchini inazidi kudumu.

Kikwete pia ametoa mchango mkubwa sana kwa demokrasia nchini kwa kitendo chake cha kubariki maridhiano baina ya vyama vya CCM na CUF kule Zanzibar. Tofauti na Watangulizi wake ambao walikuwa wakifanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa Zanzibar muda wote inaendelea kuwa chini ya genge la CCM wahafidhina, Kikwete kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu amejenga mazingira ya kuhamisha kitovu cha madaraka kutoka kwenye mikono ya wahafidhina hao, na kukiweka kwenye mikono ya Wananchi. Kama jina lake lilivyo, Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar itakuwa ni serikali ya Wananchi kwa kila hali.

Aidha, tofauti na Mkapa ambaye aliunda tume ya Warioba kwa nia ya kutambua vyanzo na mianya ya rushwa na kisha baada ya kukabidhiwa ripoti akaifungia kabatini na kuisahau; Kikwete kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi amethubutu kuondoa kulindana na u-mwenzetu katika vita dhidi ya ufisadi.

Kitendo chake cha kuruhusu kesi kadhaa za vigogo wa serikali yake na ile ya mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, kufikikishwa mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali za ufisadi; ni kielelezo cha wazi cha mabadiliko hayo ya msingi yanayolenga kuondoa dhana kuwa kuna watu 'wasioguswa' na sheria.

Thamani ya kitendo chake haimo kwenye utambulisho binafsi wa nani kafikishwa mahakamani na nani hajafikishwa, ila iko katika 'ujasiri wa kuvunja mwiko' ambao tumeuzoea kuwa siku zote wanaokamatwa na kufikishwa mahakani ni vidagaa tu wakati mapapa, masangara na manyangumi ya ufisadi yanaachiwa yaendelee 'kutesa'.

Aidha kitendo chake cha kuliachia bunge lichunguze kwa kina zabuni ya ukodishaji wa mitambo ya umeme iliyozaa kashfa ya Richmond na kupelekea aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowasa na mawaziri wenzake wawili kujiuzulu, ni moja ya vielelezo vya 'ujasiri huo wa kuvunja mwiko'.

Kashfa ya Richmond haina tofauti sana na kashfa ya ununuzi wa meli ya MV Bukoba enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere. Hata hivyo tofauti ni kwamba enzi ya Nyerere bunge halikuwa na uhuru wa kujadili lolote kwa kina; na kwa maana hiyo basi mjadala wa kina juu ya kashfa ya meli hiyo ukaepukwa.

Enzi ya Nyerere zilikuwepo pia kashfa za kukodi ndege mbovu, kashfa ya farasi wa makatibu kata, nakadhalika. Utawala wa Nyerere ulikwepa kashfa hizi kwa sababu tu vyombo huru vya habari havikuwepo; na pia kwa sababu Nyerere hakuona haya kutumia mamlaka ya kikatiba aliyokuwa nayo kutishia kuvunja bunge pale lilipoonekana kutaka kuchafua hali ya hewa. Tusisahau kuwa hadi leo raisi wa Tanzania bado ana mamlaka hayo kikatiba, na Kikwete angeweza kuyatumia kama angetaka.

Kama nia ni mabadiliko, huenda maaskofu wangehangaika kumpigia debe Prof. Lipumba kwa kigezo cha sifa huenda kidogo tungewaelewa; kwani hakuna mtu yeyote mkweli ambaye hatakiri kuwa Prof. Lipumba kawazidi sifa kwa kila hali wagombea wenzake wanaowania nafasi ya uraisi kwa sasa.

Lakini maaskofu hao wanapojifunga vibwebwe kujaribu kuwaghilibu wafuasi wao kuwa 'wasiangalie mambo binafsi ya wagombea' wakati wa kupiga kura, hata kama mambo hayo yanakiuka zile AMRI KUMI ZA MUNGU, hapo ni lazima tupate wasiwasi juu ya ajenda halisi ya maaskofu wetu. Ndiyo maana tunauliza: Hivi kweli hizi ni kampeni, au ni vita ya msalaba?
 
Please edit ur content, put some space in it; no one can read that! :mad2:
 
Hili li-article lako hakuna atakayelisoma. Umeliandika ovyo sana. Weka aya, na maandishi makubwa zaidi kidogo.
 
Daboman,
Mkipiga kampeni za mwisho kwa kutumia propaganda hizi mtakuwa mnaota kuvuka Mto Kagera kwa Kuvunja Dalaja.
 
Dabomani kwanza karibu sana jukwaani!!!!
Hebu edit hiyo post yako ili watu tuweze kuisoma kwa utulivu na kuielewa!
 
Back
Top Bottom