Kilaini: Kikwete bado ni chaguo la Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilaini: Kikwete bado ni chaguo la Mungu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, May 23, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  May 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  • LAKINI ATAKA AWATIMUE MAWAZIRI, WASAIDIZI WANAOMUANGUSHA
  Sunday, 23 May 2010
  Julieth Kulangwa

  MIAKA minne iliyopita Askofu Methedious Kilaini wa Kanisa Katoliki alimuelezea Rais Jakaya Kikwete kuwa ni "chaguo la Mungu" na hadi sasa hajabadili msimamo wake, lakini anasema wasaidizi wake na mawaziri wake wanamuangusha na hana budi kuachana nao iwapo atachaguliwa tena kuongoza nchi.

  “Mwaka 2005 niliwahi kusema kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu... kwa maana kwamba kiongozi yeyote anayechaguliwa na watu anakuwa amesimamishwa na Mungu," alisema Kilaini katika mazungumzo na Mwananchi Jumapili.

  "Miaka minne baadaye ameendelea kupendwa kwa kiasi kilekile na wananchi kwa kuwa kweli ni chaguo hasa ambalo Watanzania walilihitaji.”

  Askofu Kilaini ametoa kauli hiyo wakati Rais Kikwete akiangaliwa kwa mtazamo tofauti katika kipindi ambacho anaelekea kumaliza kipindi cha miaka mitano cha utawala wake, na hasa baada ya kutoa kauli kali dhidi ya wafanyakazi mapema mwezi huu.


  Serikali ya JK pia iliingia kwenye mgogoro mkubwa na viongozi wa kidini katikati ya mwaka jana baada ya bajeti kuu kuonyesha kuwa taasisi hizo zimefutiwa msamaha wa kodi uliokuwa unatolewa kwenye vifaa mbalimbali vinavyoingizwa kwa ajili yab huduma, kiasi cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kulazimika kufanya mikutano ya haraka iliyomalizika kwa msamaha huo kurejeshwa.


  Lakini Askofu Kilaini anaona kuwa mapungufu yaliyoibuka kwenye serikali ya JK yalitokana na udhaifu wa mawaziri na wasaidizi wake.


  “Yapo mambo ambayo hayakwenda vizuri katika kipindi hiki, lakini ukiangalia yeye kama rais hawezi kujua kila kitu... anahitaji kusaidiwa na watendaji wake wa karibu na hawa wamekuwa wakimwangusha mara kwa mara," alisema Askofu Kilaini katika mahojiano na Mwananchi Jumapili.


  Kiongozi huyo wa kiroho alisema wapo baadhi ya mawaziri ambao hawajamsaidia rais wala kutimiza wajibu wao kwa nyadhifa walizopewa na kwamba hao ndio waliochangia kuitia doa serikali ya Kikwete.
  “Wapo mawaziri ambao hawajafanya chochote tangu alipowateua," alisema askofu huyo ingawa hakuwa tayari kuwataja mawaziri hao.

  "Inafikia wakati rais au waziri mkuu analazimika kufanya majukumu yao (ya mawaziri hao). Hawa hawamfai na rais inabidi asiwateue tena baada ya uchaguzi ujao.”


  Askofu huyo, ambaye amekuwa hasiti kuzungumzia masuala mbalimbali kila anapotakiwa kufanya hivyo na vyombo vya habari, pia aligeukia wasaidizi wake na kueleza kuwa kwa kiasi kikubwa ndio waliochangia kumwangusha JK.


  Alisema rais hawezi kujua kama hoteli anayokwenda kuizindua imejengwa kwenye hifadhi ya barabarani, alisema Kilaini akirejea tukio la hoteli ya kitalii ya Arusha ambayo Kikwete aliifungua rasmi na sikku moja baadaye ofisi ya Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Arusha ikavunja ukuta wa uzio kwa sababu ulijengwa ndani ya hifadhi ya barabara.

  "Ni kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na watu ambao wanalipwa mishahara mikubwa inayotokana na fedha za walipa kodi. Hawa wamekuwa wakimwangusha kwa kumuingiza katika mambo yasiyofaa," alisema Kilaini.

  Awali akifafanua sababu za kuendelea na msimamo wake kuwa Rais Kikwete ni kipenzi cha wengi, Askofu Kilaini alisema kuwa kiongozi huyo wa serikali ya awamu ya nne amekuwa karibu na wananchi, hivyo si vibaya wakampa tena nafasi ya kuongoza nchi.

  Lakini, Kilaini ambaye ni askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba, aliliambia gazeti hili kuwa katika kipindi cha utawala wake wa miaka minne iliyopita, Rais Kikwete alijiweka karibu na wananchi ndio maana ameendelea kupendwa.


  Askofu huyo, mwenye msimamo wa wastani dhidi ya serikali, aliongeza kwamba Kikwete anapendwa kwa kuwa ni rais aliyejiweka karibu na jamii tofauti na marais wengine, hali iliyosababisha kupendwa na wananchi.

  Kilaini alimsifu Kikwete kuwa ni rais pekee aliyefungua milango ya ukweli na uwazi kwa kuacha kila kitu kizungumzwe na kuchambuliwa kwenye vyombo vya habari kwa mapana yake bila mipaka.

  “Ni Rais aliyeruhusu uhuru wa kuongea; vyombo vya habari vinaandika na watu wanazungumza kila kitu bila kuingiliwa au kunyamazishwa. Kwa dhamana aliyonayo angeweza kuzuia mambo haya, lakini anaawaacha watu wachambue mambo yanayowahusu mpaka ukweli utakapopatikana," alisema.


  Aliongeza kusema: "Mfano, kuna habari iliwahi kuandikwa na gazeti moja kuwa Rais Kikwete alinilipia matibabu nchini India wakati fulani nilipougua. Haikuwa habari ya kweli, lakini rais hakutaka kulizungumzia na kuwaachia walioanzisha walimalize.”

  Alisema kwa uhuru huo alioutoa mkuu huyo wa nchi, umemfanya kuwa mmoja kati ya marais walioandikwa sana na vyombo vya habari na kushambuliwa na vyama vya siasa.


  Kilaini aliongeza kwamba Rais Kikwete anapaswa kuendelea kuongoza hasa kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha katika suala la kuushugulikia mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar.


  “Suala la Zanzibar lilikuwa gumu na hakuna aliyefikiri kama angeweza kulishughulikia na kulifikisha hapa lilipo katika kipindi kimoja tu... kwa hili amejitahidi na kwa kweli anahitaji msaada ili nchi yetu iendelee kuwa kisiwa cha amani ulimwenguni,” aliasa Watanzania.

  SOURCE: GAZETI LA MWANANCHI
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuna msemo unaosema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Kama huo msemo ni kweli basi kila kiongozi aliye chaguliwa kidemokrasia na wengi ni chaguo la Mungu. Vote 2010.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  si wampake mafuta awe mfalme juu yao kama Sauli!!?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani hapa ameongea kama Kilaini na si kiongozi wa dini
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  May 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu,

  Maneno ya Askofu huyu yasichukuliwe kimzaha kabia. Kuna ukweli mwingi kuliko kufikiria vitu hivi kwa haraka pasipo kupima maneno ya Askofu.

  Nilichomwelewa mimi Askofu kaelezea matatizo yaliyopo ktk Uongozi wa Kikwete na hakika ukisoma kwa makini utagundua kwamba Mambo yote haya yanatokana na UDHAIFU wa kiongozi huyu ktk utendaji kazi wake pamoja na kwamba alikuwa na malengo mazuri.

  Tusijidanganye kabisa kwamba Kikwete hapendwi, bado wapo wengi wanampenda kwa ile nia yake nzuri kama wanavyosema wao na lawama hizi ziwafikie wale walioshindwa pamoja na kwamba JK kashindwa kuwachukulia hatua. Hisia hizi zipo kwa Watzanania wengi sanma kama vile wanavyoshindwa kukihukumu chama kizima cha CCM kwa Ufisadi na kushindwa kuongoza isipokuwa tuwashutumu baadhi ya viongozi wenye mapungufu hata kama chama kimeshindwa kuwachukulia hatua.

  Bado CCM ni chaguo la wengi hivyo kuna ukweli mkubwa kwamba bado Kikwete ni chaguo la wengi..Hivyo maadam watu wamechagua hivyo basi bila shaka ni chaguo la Mungu. Huyu ni nchungaji mlitaka atumie kitabu gani au lugha gani zaidi?.. By the way hata mimi naamini - Nothing happens ,but by the power of the grace of God..
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkadara wakati mwingine huwa unaandika pumba sana! I am not convinced
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,184
  Trophy Points: 280
  Tangu enzi za Wasumeria, Wababeli na Wamisri na Wachina wa kale, viongozi wa kisiasa , wafalme na MaFirauni walitumia dini kuendeleza matakwa yao ya kisiasa. Kwa kweli suala zima la mungu, na mfalme kuwa amechaguliwa na mungu lilianzishwa na wanasiasa.In fact idea nzima ya organized religion imeanzishwa na wanasiasa ili kuweza kuwa control vizuri watu.

  Kilaini hana tofauri na ma "high priests" wa Firauni ambao wangeweza kusema lolote ili kubakia katika favors za Firauuni. Ni pimp wa kumuuza Kikwete.

  Huyu Kilaini sisi ambao hatuamini katika kuwepo kwa mungu hawezi hata kuanza kutudanganya, audience yake ni kwa wale wanaoamini mungu tu.

  Makes you wonder what else is he lying about under the banner of "mungu"
   
 8. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngoja nirudi kwenye Sunday School, kwenye kitabu cha Hosea 8.4;

  Mungu anasema juu ya Wana wa Israel " Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari".

  ......Hivyo si kila aliyechaguliwa na wengi ni chaguo la Mungu.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani kuna tofauti gani kubwa kati ya hao wawili?
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Masanilo,
  wewe uko sahihi asilimia 100, hapo kweli ameongea kama Kilaini na si kiogozi wa dini na kama amesema kama kiongozi wa dini, nina mashaka na huyo Mungu, aliye hai yaani JEHOVA ama mungu mzimu, ama ameongozwa na katekisimo!

  Hapo naona ni sawa kama kiongozi wa dini anahamasisha matumizi ya Kondomu wakati yeye anapaswa kusimamia maandiko ya kitabu anachotumia kuongoza dini yake kwa kwa kusimamia watu waache uzinifu na uasherati hasa kwa kuwa ni chukizo kwa Mungu.

  Atakuwa Mungu huyo alolala usingizi?
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hilo nalo neno!
   
 12. k

  kashwagala Senior Member

  #12
  May 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu asifanye tukamtukana tukapata dhambi bure! huyo rais anayesema ni chaguo la Mungu yuko wapi? kwani Tz tuna rais?
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  chaguo la mungu? mungu gani? chaguo la mungu haliko hivyo.....si cha rais wala mbunge wala yeyote yule si chaguo la Mungu aliyeumba mbingi na nchi. kama Mungu angekuwa anawachagua tusingeona wanashinda kwa waganga wa kienyeji, mungu gani huyo anachanganywa na waaguzi, kina shee yahya wachawi warozi wasoma nyota na wauaji?tz hatujawahi kupata rais chaguo la Mungu hata siku moja. nyerere mwenyewe alikuwa chaguo la yule aliyempa kifimbo chake ashike mkononi kama hirizi.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nadhani alichozungumza Kilaini ni kwamba Kikwete ana mazuri yake na mabaya yake hivyo watu tunapomchagua tumchague kutokana na vile tunavyompima. Nakubaliana nae ikiwa wananchi watamtaka basi ni kweli yeye ni chaguo la mungu. Ni ngumu sana kwa kiongozi wa kidini kusema rais hafai kwasababu rais ni institution ambayo inatawala nchi sasa hilo jambo linaweza kuleta matatizo baadae. Kiufupi hapo Kilaini ametumia hekima kusema Kikwete achaguliwe vile tunavyomuona. Huo utendaji na nini ni siasa tupu hamna jengine.
   
 15. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo unapokosea,..kama unajua atachaguliwa na wananchi kwanini asingiziwe Mungu?kwanini isitoshe kusema ni chaguo la watu?
   
 16. P

  Paul S.S Verified User

  #16
  May 23, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  nadhani kilaini hapo amechemsha, kama kweli jk nichaguo la Mungu basi huyo Mungu haitakii mema nchi hii kutuchagulia kiongozi wa jinsi hii
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama kila anayechaguliwa na wengi ni chaguo la Mungu basi hata Sadam alikuwa chaguo la Mungu kwa sababu alikuwa akipata asilimia 100 kwenye uchaguzi wake.

  Tatizo la Kilaini anachanganya utendaji na mapenzi(uchaguzi) unaweza ukachaguliwa na Mungu lakini ukamwangusha Mungu katika utendaji, Yuda Iskaliote alikuwa chaguo la Mungu lakini alikuja kumuuza Yesu, hata Malaika Lusifa (shetani) alikuwa nyota ya asubuhi ing'aayo pande zote iliyopendwa na wengi lakini alikuja kufeli katika utendaji, kuna mifano mingi katika biblia ambapo viongozi waliochaguliwa na Mungu walishindwa katika utendaji, vivyo hivyo kwa Kikwete ingawa bado anapendwa na wengi lakini anatuangusha katika utendaji wake.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kusikia kocha anayesifiwa baada ya timu kushindwa kwa kosa la kupanga vibaya timu yake. Inawezekana kabisa Kikwete bado ni kipenzi cha watu wengi. Lakini mimi simuangalii Kikwete kama mtu mwovu au mwenye tatizo la kuweza kunifanya kumchukia. Nisichokubaliana nacho ni jinsi nchi inavyokwenda kwa bahati bahati ilihali yeye akijua hilo. Amewapa watu wasio na uwezo madaraka na wameshiondwa kumsaidia. Hilo ni tatizo la kiungozi la JK na kwa bahati mbaya hata kama tunampenda vipi, kama meli hii inazama huku tunashuhudia, ikifika chini ya bahari na sisi wengine hatujui kuogolea basi tutakufa maji. Mtu mfu hawezi kumuimbia JK sifa yoyote. Anajua analotakiwa kufanya kuepukana na kutuletea kushindwa anasita nini?
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Unajua Kilaini naye akipewa kipaza sauti huwa anasema sana....isije kuwa ndio maana aepelekwa pembezoni mwa nchi ili sauti yake isiwe kali kama ilivyokuwa miaka ileeee
   
 20. Mujuni2

  Mujuni2 Senior Member

  #20
  May 23, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "kama mnampenda sana kanyweni nae chai" au "hatutakunywa mvinyo mpaka atakapowasili ili tugonganishe naye bilauri zetu" J.K.Nyerere, nasaba haina nafasi ktk maswala ya msingi ya kitaifa.
   
Loading...