Kilaini: Kikwete bado ni chaguo la Mungu

Huyu Askofu ange shut up!Ndio tatizo la viongozi wa dini Tanzania!Wanapotosha waumini wao ambao wengi ni poor hawajui dunia inakwendaje.

Huyu Askofu anhehubiri zaidi ya morality,ulevi,umaskini badal ya kutoa kauli hii.Si ajabu alisema hivi kuhusu Mkapa!

What a shame!
 
jamani jamani dini na siasa....wapi na wapi...hebu tuache haya mambo!!!inakera mno!!!
 
Wakuu zangu,
...
Bado CCM ni chaguo la wengi hivyo kuna ukweli mkubwa kwamba bado Kikwete ni chaguo la wengi..Hivyo maadam watu wamechagua hivyo basi bila shaka ni chaguo la Mungu. Huyu ni nchungaji mlitaka atumie kitabu gani au lugha gani zaidi?.. By the way hata mimi naamini - Nothing happens ,but by the power of the grace of God..

Hata kwa ujinga(ignorance) au uoga wa wengi? Mungu yupi huyo anayetufunika ujinga almuradi amweke mbabaishaji madarakani?
 
si wampake mafuta awe mfalme juu yao kama Sauli!!?

Kiongozi aliyechaguliwa na Mungu, mfano wake utakuwa kama Daudi kwenye Bible, Suleiman mwanae, hezekia kwenye kitabu cha wafalme aliyevunjavunja madhabahu za miungu mingine etc.

Mungu humchagua mtu aliye mcha Mungu, kama mtu si mcha Mungu hata akiwa madarakani, ni kwamba Mungu anatulinda naye tu ili asitudhuru, ila si chaguo la Mungu kama atakuwa na michanganyo kama walivyo viongozi wengi wa kiafrica. Mungu wetu hachanganywi na uchawi, waganga wa kienyeji etc. sijasema rais anafanya hivyo, sina uhakika, ila ni dhahiri kwamba marais wengi wa africa wanakuwa na waganga na wachawi wao kama ilivyokuwa kwa mfalme Nebukadneza wa Uajemi (iran) miake ile, mfalme Dario..yule aliyemwoa malkia Estha..etc...so anakuwa sio chaguo la Mungu.

However, Mungu aweza kutumia hata mawe au hata punda kufanya kitu. unakumbuka kuna punda alishawai kuongea? Pia, Mungu alishawai kumtumia Koresh kitabu cha Isaya 45 hata kama alikuwa hamchi yeye, kama Mungu akiamua, anawezamtumia mtu yeyote aliyewekwa madarakani na watu, ila si kwamba Mungu ndo kamuweka madarakani huyo mtu...kigezo ambacho kinaweza kumfanya Mungu amchague mtu kama alivyofanya kwa Koresh, ni pale hata kama si mcha Mungu atakapo ruhusu mambo ya Kimungu kufanyika, kama ilivyokuwa kwa wafalme wale wa enzi zile walivyowaruhusu wayahudi kurudi kwao kwenda kujenga Jerusalem etc..kumbuka kitabu cha Yeremia....Nehemia etc.

Hivyo, sina uhakika kama KIKWETE NI CHAGUO LA MUNGU, kwasababu simjui kama hana waganga na wasoma nyota wake, pia sijaona amefanya mambo ya kimungu kwa binafsi yangu, ya kumfanya Mungu amtumie hata kama si mcha Mungu kwa imani yangu. namheshimu kama rais wangu, ila simpi kura yangu kwasababu sijaona amefanya mambo niliyotarajia angeyafanya.

However, mimi ni mwanadamu, changuo langu mimi linaweza kuwa si chaguo la MUNGU...nitahakikisha kwenda kupiga kura, pamoja na kumwomba Mungu atusaidie watanzania kumpata rais ambaye ni chaguo la Mungu, ambaye kwa sasa sijawa na uhakika na yeyote kwa macho ya kimungu...ila kibinadamu wapo, ambao sio wanaotoka ccm.
 
Jamani ni kweli kabisa tunahitaji kutumia akili ya kuzaliwa kama ya shule hatuna Mungu kasingiziwa sana, na hawa watu kama Mungu angetuchagulia Kikwete ni lazima angefanana, Kujua kusudi la Mungu hatutumii elimu ya darasa la 7 form IV, SIX ama chuo.

Ni wazi kuwa Mungu hufanya mambo kwa ajili yake mwenyewe, huyu kikwete ana % kubwa ya udikiteta najaribu kuiita wa kihuni, kuliko chembe japo ya haradali ya hekima, busara na maarifa.

Sasa utakapo sema ni chaguo la Mungu, sijui pengine ni kweli maana hata wanaomiliki mali nyingi kwa kuua maalubino nao watakwambia wamebarikiwa na Mungu lakini ukweli uko nyuma ya mambo yao, ni kweli hatupaswi kuhukumu lakini huyu kilaini aweke wazi ni kwa ushahidi gani anaoweza kulidhihirishia taifa kuwa kikwete ni chaguo la Mungu?

Kama ni mungu yule aliyewabariki watu kuwa na mali nyingi walizozipata kwa kuwauwa na kuchukua viungo vya maalubino hapo nitamwelewa, lakini Mungu yaani wa watu wote nachelea kuita hiyo ni kufuru.
 
Eh! Mungu tusaidie na Tanzania yetu!

Eti anaangushwa na Mawaziri wake! Sasa kama wanamuangusha kwanini asiwafukuze kazi? ukiondoa wale waliojizulu kwa ufisadi akina Lowassa, Karamagi na kama sikosei Msabaha kishawafukuza Mawaziri wangapi wanaomuangusha?
 
Eh! Mungu tusaidie na Tanzania yetu!

Eti anaangushwa na Mawaziri wake! Sasa kama wanamuangusha kwanini asiwafukuze kazi? ukiondoa wale waliojizulu kwa ufisadi akina Lowassa, Karamagi na kama sikosei Msabaha kishawafukuza Mawaziri wangapi wanaomuangusha?

Huyu paroko bwana! Hawa ndio wanafanya hata kanisa la Bwana linatukanwa. Wamezoea kuupaka uongo marhamu yenye kunukia, kama vile wahubiripo wasipoulizwa maswali.

Kama vitendea kazi vyote vipo, na mkuu wa shule ndio anaetumika kwenye usajili wa walimu wake, Je ikitokea shule inatoa daraja sifuri kwa wanafunzi wote, basi tuwasingizie walimu na sio mkuu wa shule?

Mkuu wa shule ameajiri walimu wa siasa kufundisha somo la hisabati, huku mwalimu wa historia akifundisha Fizikia n.k

Usipojua tatizo wewe ndio tatizo, which means JK hajui tatizo, hivyo yeye ndiye tatizo na mzigo mzito ambao waTanzania huenda ikabidi waubebe tena kwa miaka mitano. Sijui kama hili taifa likiendelea hivi kama halitavunjiaka, hasa ukitilia maanani miaka 5 ya mwisho ni ya wizi na unyanganyi wa mali ya serikali.
 
Huyu paroko bwana! Hawa ndio wanafanya hata kanisa la Bwana linatukanwa. Wamezoea kuupaka uongo marhamu yenye kunukia, kama vile wahubiripo wasipoulizwa maswali.

Kama vitendea kazi vyote vipo, na mkuu wa shule ndio anaetumika kwenye usajili wa walimu wake, Je ikitokea shule inatoa daraja sifuri kwa wanafunzi wote, basi tuwasingizie walimu na sio mkuu wa shule?

Mkuu wa shule ameajiri walimu wa siasa kufundisha somo la hisabati, huku mwalimu wa historia akifundisha Fizikia n.k

Usipojua tatizo wewe ndio tatizo, which means JK hajui tatizo, hivyo yeye ndiye tatizo na mzigo mzito ambao waTanzania huenda ikabidi waubebe tena kwa miaka mitano. Sijui kama hili taifa likiendelea hivi kama halitavunjiaka, hasa ukitilia maanani miaka 5 ya mwisho ni ya wizi na unyanganyi wa mali ya serikali.

Nimependa hiyo reddish..

It is about time watz wakajisomea zaidi na kuelimika na taratibu wataanza wenyewe kujua ukweli ni upi na kuchukua hatua muafaka. Watz hawahitaji viongozi wa dini kuwashikia akili zao na wala hawahitaji councelling kutoka kwa yeyote. Watu kama akina Kilaini is a big failure, kila siku wanauma na kupuliza kuhusu utendaji wa serikali, and this says a lot about nini haswa wanakisimamia. Wanajali maslahi yao binafsi na ndio maana ilipotokea ishu ya kulipia kodi mnamo mwaka jana walipaaza sauti zao kaa mtu aliyepigwa mshale wa makalioni. Lakini pale mtz wa kawaida anapopigika (which is so obvious) they turn the blind eye. Ukitaka kujua these people are untouchable jaribu kutembelea wanapoishi na kujua lifestyle yao, IT IS FAR BEYOND MAISHA YA MVUJA JASHO WA KAWAIDA. Hawa watu sasa wamekuwa kama part of aristocrats na watafanya kila sarakasi kumantain status quo.
 
Mkadara wakati mwingine huwa unaandika pumba sana! I am not convinced
Pumba ndio starehe ya JF...

Mkuu wangu nachosema mimi maneno ya huyu mchungaji tusiyadharau kabisa hata kama wewe huoni mantiki ndani yake. Wapo watu wengi sana wanampenda Kikwete na kwa sababu alizozisema Mchungaji..Wapo watu wanaamini JK anaangushwa na Mawaziri wake na baadhi viongozi lakini sii yeye. Mawazo kama haya pamoja na kwamba unapingana nayo lakini huwezi kuyaondoa akilini mwa wapenzi wake..

Nimetoa mfano wa CCM kushindwa kuongoza ambako wewe na mimi tunauona lakini wapo watu kwa hesabu kubwa hawaoni mapungufu haya ila kuna baadhi ya watu ndio sii wazuri... Na hata hao CCM wenyewe kama alivyo JK hawaoni makosa ila baadhi ya viongozi ndani ya chama chao ndio wenye makosa sii Mapungufu lakini pamoja na kuelewa huko hawajachukuliwa hatua.

Hii ndio Tanzania yetu mkuu, tunaweza tu kujipanga kwa kuelewa ukweli wa watu na mazingira tuliyopo kukabiri yanayokuja na utata wa kumshinda JK au CCM..

Na kuhusu Mchungaji yeye ni msomi wa dini na mara zote hawezi kusema vitu kinyume cha imani yake ya dini.. Hata mimi nimesema hivi Hakuna JEMA linalowezekana pasipo kuwezeshwa na Mwenyezi Mungu..
Lakini labda nimeacha kusema tu kwamba - Pia hakuna SHARI inayowezekana pasipo kuwezeshwa na Shetani...

Hivyo maadam huyu mchungaji anaamini kwamba sisi sii watu wa shetani na tumenmchagua kiongozi yule kwa kura zetu halafu hadi leo bado anapendwa kwa nguvu ile ile ya mwaka 2005 basi bila shaka ni maamuzi ya Mungu. Kwa maana nyingine Mungu hujalia wanadamu wa kile tulichokiomba..Sipendi uongozi wa JK na chama CCM lakini kuna asilimia 80 waliomchagua na bado watamchagua..Mchungaji katuambia ukweli wa hali halisi hivyo kazi kwetu, tuamini tusiamini ndio ukweli JK ataweza kupita kwa kishindo!
Sasa kama hizi ni Pumba niachie mwenyewe!
 
Matokeo na matunda mazuri ya serikali au umoja wowote ni kiongozi wake. Ukisema watendaji kazi wake ni wabovu ambao amewachagua yeye mwenyewe basi naye ni mbovu kwani hawezi kuona ubovu. Timu ya mpira wa miguu inaposhindwa mfululizo, kocha wake utimuliwa na kapteni ubadilishwa au kukosa usajili msimu ujao, sasa jeje hii timu ya serikali ya Tanzania hijashindwa kutokana na kocha?
 
Wakuu zangu,
Maneno ya Askofu huyu yasichukuliwe kimzaha kabia. Kuna ukweli mwingi kuliko kufikiria vitu hivi kwa haraka pasipo kupima maneno ya Askofu.
Nilichomwelewa mimi Askofu kaelezea matatizo yaliyopo ktk Uongozi wa Kikwete na hakika ukisoma kwa makini utagundua kwamba Mambo yote haya yanatokana na UDHAIFU wa kiongozi huyu ktk utendaji kazi wake pamoja na kwamba alikuwa na malengo mazuri.

Tusijidanganye kabisa kwamba Kikwete hapendwi, bado wapo wengi wanampenda kwa ile nia yake nzuri kama wanavyosema wao na lawama hizi ziwafikie wale walioshindwa pamoja na kwamba JK kashindwa kuwachukulia hatua. Hisia hizi zipo kwa Watzanania wengi sanma kama vile wanavyoshindwa kukihukumu chama kizima cha CCM kwa Ufisadi na kushindwa kuongoza isipokuwa tuwashutumu baadhi ya viongozi wenye mapungufu hata kama chama kimeshindwa kuwachukulia hatua.

Bado CCM ni chaguo la wengi hivyo kuna ukweli mkubwa kwamba bado Kikwete ni chaguo la wengi..Hivyo maadam watu wamechagua hivyo basi bila shaka ni chaguo la Mungu. Huyu ni nchungaji mlitaka atumie kitabu gani au lugha gani zaidi?.. By the way hata mimi naamini - Nothing happens ,but by the power of the grace of God..

Kwani nani kasema kuwa Kikwete hapendwi?tunafahamu kuwa wapo watu ambao piga ua watakufa na JK akiwemo Kilaini.Hawa ni marafiki na nikubaliane na mtu aliyesema kuwa Kilaini hajazungumza kama kiongozi wa dini nami niongeze kuwa kazungumza kama rafiki wa JK...
 
Jamani mimi Namuomba Mungu anisamehe.

Natangulisha Ombi hii kutokana na kitakachofuata:

> Kwanza ningetamani sana huyu mtumishi wa Bwana Anyamaze. Aache hizi kauli zake kabisa. Zinakera.

Mnakumbuka Maneno ya Yesu Akiwaambia wafuasi wake? "ASIYEKUWA WANGU, HANA SHIRIKA NAMI - NAYE ALIYE WANGU HUYAFANYA YOTE NILIYO WAAGIZA"

Sasa hebu Tujiulize Mawaziri si wanafunzi wa Kikwete? Je si Kikwete aliyewachagua... Sasa tukichukulia mfano wa Yesu. Ina maana kama mawaziri wana shirika na Kikwete then Pumba wanazofanya zina Muhusu... Sasa mpaka Hapo bado tuseme ni Chaguo la Mungu?

Huu ni mtazamo wangu tu Kibinadamu. Ila kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na Askofu KIlaini! Tena Kuna Maneno Yanasema Mtawatambua kwa matunda yao. Je Tumtambue raisi kwa matunda gani?

Nawakilisha
 
Viongozi wa dini walikuwepo zamani. Hivi sasa tuna viongozi wa dini ambao wengi wao ni wababaishaji, walaghai, matapeli, mafisadi, wazinzi ... you name it! Ndio maana migogoro makanisani haiishi.
 
Anarudisha fadhira kama mzee wa Kilalacha au mzee wetu wa Magomeni wa utabiri wa kimiujiza.
 
Tangu enzi za Wasumeria, Wababeli na Wamisri na Wachina wa kale, viongozi wa kisiasa , wafalme na MaFirauni walitumia dini kuendeleza matakwa yao ya kisiasa. Kwa kweli suala zima la mungu, na mfalme kuwa amechaguliwa na mungu lilianzishwa na wanasiasa.In fact idea nzima ya organized religion imeanzishwa na wanasiasa ili kuweza kuwa control vizuri watu.

Kilaini hana tofauri na ma "high priests" wa Firauni ambao wangeweza kusema lolote ili kubakia katika favors za Firauuni. Ni pimp wa kumuuza Kikwete.

Huyu Kilaini sisi ambao hatuamini katika kuwepo kwa mungu hawezi hata kuanza kutudanganya, audience yake ni kwa wale wanaoamini mungu tu.

Makes you wonder what else is he lying about under the banner of "mungu"
Msio amini Mungu mnaitwa wapagani kwa nini usitumie term "sisi wapagani!"
Kisha Mungu wetu anaandikwa kwa jina kuanzia capital letter "M". Wa kwako anayeanza na "m" sidhanikama ndiye Kilaini alikuwa anamzungumzia.
 
Chaguo la mungu yupi kila dini inadescribe mungu kivyake. Mungu wa wakiristo si wa wawaislamu.
 
Tangu enzi za Wasumeria, Wababeli na Wamisri na Wachina wa kale, viongozi wa kisiasa , wafalme na MaFirauni walitumia dini kuendeleza matakwa yao ya kisiasa. Kwa kweli suala zima la mungu, na mfalme kuwa amechaguliwa na mungu lilianzishwa na wanasiasa.In fact idea nzima ya organized religion imeanzishwa na wanasiasa ili kuweza kuwa control vizuri watu.

Kilaini hana tofauri na ma "high priests" wa Firauni ambao wangeweza kusema lolote ili kubakia katika favors za Firauuni. Ni pimp wa kumuuza Kikwete.

Huyu Kilaini sisi ambao hatuamini katika kuwepo kwa mungu hawezi hata kuanza kutudanganya, audience yake ni kwa wale wanaoamini mungu tu.

Makes you wonder what else is he lying about under the banner of "mungu"

(Hapo kwenye red) Ni kweli kama haumini MUNGU una haki ya kutamka uliyotamka kwa iyo waachie hao wanaoamini kuna MUNGU hasa WARUMI 13:1 watafakari.
Mimi naamini mwaka 2005 alikuwa chaguo la MUNGU, MUNGU alituchagulia lakini kwa 2010 naamini baada ya uchaguzi tutajua nani chaguo la MUNGU mwaka huu kwa sasa ni mapema mno kutangaza kuwa MUNGU ameshamchagua huo ni uaguzi na unabii wa uongo.
Tusubiri baada ya uchaguzi MUNGU atatupa rais nani! LLakini hii ninkwa wale tu wanaoamini katika MUNGU na NENO LAKE
'Za kuambiwa changanya na za kwako"
 
Back
Top Bottom