Kila tunapoonana nakuwa kwenye hali ya ovyo ovyo lakini nampenda

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Mpaka nahisi kama vile napitishwa kwenye majaribu. Mwezi ulioisha niliyabananga kwa ofisi, hivyo nikalimwa ban la wiki tatu. Ndipo huyu mwanamke alipohamia jirani na mahali ninapoishi. Kama kawaida nikaamua kumuimbisha.

Mida ya saa nne ninapita gheto, saa nane, saa kumi na moja mpaka akafikia hatua ya kuniuliza, "Hivi wewe ni randa randa? Mbona kama hauko siriazi na maisha? Maake kila muda nakuona nyumbani". Hivyo nikajiwekea ratiba ya kuzurura kuanzia asubuhi ili jioni tena usiku kabisa wa saa 1 hivi ndio nirudi maghetoni

Mara ya kwanza alinikuta kwenye kijiwe cha Simba na Yanga saa tano asubuhi nakunywa kahawa.

Mara ya pili alinikuta mgahawani saa sita mchana nimesinzia huku domo nimeacha wazi.

Mara ya tatu alipishana na mimi nikiwa natokea kwenye jumba la kusukia mikeka huku nimeukunjua mkeka wangu ulionifikia magotini.

Mara ya nne alinikuta nazichapa na mwanamama mmoja hivi mishale ya jua kali kwa sababu X.

Mara ya tano alipishana na mimi nikiwa namtongoza mwanamke, tena aliyenizidi umri mbali sana mithili ya jishangazi (namshukuru Mola kwa kuwa sasa nimerudi kwenye kitengo).

Majuzi kanikuta barabarani natafuna nusu ya mtikiti maji, nilivyoushikilia mithili ya mtu ananyonya mbususu huku mimaji ikiangukia kunako shati.

Jana jioni kanikuta nakimbizana na vitoto akatikisa kichwa kuashiria yamekwisha.

Sijui haya yote yananikuta kwanini.
 
😂😂😂 Daah wewe umezidi

Namimi nimepunzika job miezi minne japo job Kuna ishu naifanya japo ile job haina maslahi ila siunajua inakufanya utoke, u-shine na pesa za vocha huyu manzi nimemuoa kipindi hiki kilamara ananiona Home uwani, barazani, kitaa unajua hata Kama unafuatilia mitikasi mingine huwezi kutoka morning kurudi jioni Consistency bana ananiona Kama mtoto wa mama.

Mbali na Fan side ya situation Kama hii wanawake wanakosa skills Sana za mahusiano wanawake wanaweza kosa kitu kizuri au tuseme mtu sahihi muda mwengine kwa kipima aligyomuona yeye Week moja mfano yupo kalala Geto kumbe uchumi wa Sasa hasa ishu za kazi kawaida Sana mtu kukuta yupo home mkataba umeisha mwezi ulipita, anasuka mchongo, Kuna kazi anatuatilia maana mikataba imekuwa mifupi Sana nk.
 
Dah jamaa nimecheka.

Mi kuna demu nilikua katika process, sa enzi izo nakaa Mbagala Kongowe. Hiyo siku jioni nimevaa kandambili, pensi na vest ya Jordan 26, miguu vumbi huku nakula bagia nikaona meseji yake imeingia.

Kwamba ameniona natembea mitaa ya kabisani hapo ye kapita na daladala.
 
Mpaka nahisi kama vile napitishwa kwenye majaribu. Mwezi ulioisha niliyabananga kwa ofisi, hivyo nikalimwa ban la wiki tatu. Ndipo huyu mwanamke alipohamia jirani na mahali ninapoishi. Kama kawaida nikaamua kumuimbisha.

Mida ya saa nne ninapita gheto, saa nane, saa kumi na moja mpaka akafikia hatua ya kuniuliza, "Hivi wewe ni randa randa? Mbona kama hauko siriazi na maisha? Maake kila muda nakuona nyumbani". Hivyo nikajiwekea ratiba ya kuzurura kuanzia asubuhi ili jioni tena usiku kabisa wa saa 1 hivi ndio nirudi maghetoni

Mara ya kwanza alinikuta kwenye kijiwe cha Simba na Yanga saa tano asubuhi nakunywa kahawa.

Mara ya pili alinikuta mgahawani saa sita mchana nimesinzia huku domo nimeacha wazi.

Mara ya tatu alipishana na mimi nikiwa natokea kwenye jumba la kusukia mikeka huku nimeukunjua mkeka wangu ulionifikia magotini.

Mara ya nne alinikuta nazichapa na mwanamama mmoja hivi mishale ya jua kali kwa sababu X.

Mara ya tano alipishana na mimi nikiwa namtongoza mwanamke, tena aliyenizidi umri mbali sana mithili ya jishangazi (namshukuru Mola kwa kuwa sasa nimerudi kwenye kitengo).

Majuzi kanikuta barabarani natafuna nusu ya mtikiti maji, nilivyoushikilia mithili ya mtu ananyonya mbususu huku mimaji ikiangukia kunako shati.

Jana jioni kanikuta nakimbizana na vitoto akatikisa kichwa kuashiria yamekwisha.

Sijui haya yote yananikuta kwanini.
Dah🤣
 
Yaani we acha tu. Sometimes najieka smart sana kisha najilitisha angle zake ili anione wa tofauti. Lakini ndo kwanza sikutani naye. Muda mwingine huwa naenda kubisha hodi kwake pasi na mafanikio ya kukutana naye
Jitahidi iko siku atakuja kukufuma umekaa na manager wa bank kwenye kikao
 
Daah wewe umezidi

Namimi nimepunzika job miezi minne japo job Kuna ishu naifanya japo ile job haina maslahi ila siunajua inakufanya utoke, u-shine na pesa za vocha huyu manzi nimemuoa kipindi hiki kilamara ananiona Home uwani, barazani, kitaa unajua hata Kama unafuatilia mitikasi mingine huwezi kutoka morning kurudi jioni Consistency bana ananiona Kama mtoto wa mama.

Mbali na Fan side ya situation Kama hii wanawake wanakosa skills Sana za mahusiano wanawake wanaweza kosa kitu kizuri au tuseme mtu sahihi muda mwengine kwa kipima aligyomuona yeye Week moja mfano yupo kalala Geto kumbe uchumi wa Sasa hasa ishu za kazi kawaida Sana mtu kukuta yupo home mkataba umeisha mwezi ulipita, anasuka mchongo, Kuna kazi anatuatilia maana mikataba imekuwa mifupi Sana nk.
Lkn hiyo ni nzuri kwa mwanaume inasaidia kujua yupo sahihi wa kuongozana nae, sio mbio za mamba hata kenge wamo.
 
Mwanamke kabla ya kuingia kwenye mahusiano kumuona mwanaume week moja tena marambili kwa week haikufanyi kumjua ni wanamna gani.

Mwanaume utamjua akikutongoza sentences zake, uandishi, psychological tounch...unaweza mjua kilakitu kiuchumi, imani mpaka malengo... mwanamke smart hupe da physical appointment, life la Sasa lipo DISRAPTED SANA.
 
Ndo ile unampenda mtoto wa mtu jirani had ukisikia sauti yake unatoka nje kuanika nguo zilizokauka nimekumbuka kipindi hcho nikiwa kwenye mavazi ya hovyo ndo nakutana na pisi nnayoifukuzia najaribu hadi kuvaa vizur najipitisha kwao simuoni maisha haya wanaume tumeumbiwa mateso hadi basi yan :D Sema niliacha mapenzi now lyf la single ni raha had linakera :D
 
Back
Top Bottom