KiLA SIKU WANATUNZWA....

Nikweli mkuu hata mimi najaribu hata kujilazimisha mno kuzipenda lakini waapi! hamna uhalisia kabisa!! naishia kutukana tu na sizimalizi......Wajitahidi bwana mbona wenzao wanafanya muvi nzuri tuuu? Kifupi kama wewe ni mtu makini picha zao zinaboa mno!

Kuna film mbili za Kitanzania niliangalia. Sijui moja inaitwa Johari? Eti mtu kakaa msituni anasubiri gari, maeneo ambayo kakulia na anaambiwa eti hapo kuna Simba ndiyo anakurupuka na kukimbilia kuingia kwenye Basi. Niliangalia kidogo, nikapeleka mbele kidogo na nikabonyeza EJECT. Kutoka hapo sijaangalia tena hizi film. Niiamua kurudi kwenye download na nikamalizia kuangalia movie zangu za Prison break.
Mkuu Balantanda, kwenye hilo picha kwa kweli UNATISHA.

Ombi langu kwa hawa akina Kanumba ni kuwa au muwe wachezaji au muwe Director wa hizo film. Tafuteni shule nzuri za hii fani na mtaona jinsi ambavyo hata wasiopenda film zenu wataanza kuzitafuta kwa udi na uvumba. Pia pamoja na kutozipenda, nawapa HONGERA kwa kuwa WAANZILISHI wa hii biashara pamoja na ugumu wa soko lenyewe. HONGERENI SANA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom