Kila nikimshauri mchumba wangu anunue kiwanja anasema kipo mbali

Kila nikimshauri mchumba wangu anunue kiwanja anasema kipo mbali

Joined
Dec 9, 2025
Posts
89
Reaction score
213
Wakuu habari,

Mwenzenu niombeeni tu nahisi haya mambo ya mahusiano kama siyo riziki kwangu, ni mwaka jana tu nilipigwa na tukio, nimempata mwingine naye anachangamoto zake. Nimehama hadi Mkoa ila ninaopata ndo hivo.

Nina mchumba (boyfriend) wangu ambaye ana kazi nzuri na anapata posho za kutosha. Kutokana na kipato chake kuwa kizuri, hivi karibuni nilimshauri anunue kiwanja hata cha Shilingi Milioni 5 maeneo ya Chalinze ili akitunze kama uwekezaji. Hata hivyo, kila nikizungumza naye, anasema huko ni mbali sana na mjini.

Nilimshauri pia anunue kiwanja Kibaha kwenye mradi mmoja wa Shilingi Milioni 4, lakini pia alikataa. Yeye anasisitiza anataka viwanja vya maeneo ya Makongo, Salasala, au Kimara akidai kuwa huko ndiko karibu na mjini.

Changamoto ni kwamba pesa anazopata zinaishia kwenye matumizi ya kawaida tu bila kufanya jambo lolote la maana au la maendeleo.
 
Kama haelewi kula hela zake huku na ww ukiwekeza kidogo kidogo.
 
Back
Top Bottom