Kila mmoja wetu ana kashetani kake

Kila mmoja wetu ana kashetani kake

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,976
Reaction score
861,587
vishetani vyetu tumevibatiza jina la ugonjwa utamsikia mtu akikwambia mimi ugonjwa wangu ni mwanamke mwenye makalio makubwa(lakini hakwambii tiba yake wala atapona lini)
Vishetani viko vingi vingine ni vizuri vingine havisomeki na vingine vinatisha... .shetani ni roho yenye nguvu sana na ushawishi wa aina ya kipekee kabisa wengi wetu tumekamatika huko na hatuna uwezo wala nguvu za kujitoa kwakuwa hicho kitu ndio shetani wako unayemwabudu
1455891853870.jpg

Imagine mtu yuko tayari kukosa kwenda kuabudu kuliko kwenda kwenye mpira...mtu yuko tayari kukosa kipindi cha dini kwenye tv kuliko bongo movie, mtu yuko tayari kufuta video yenye kufundisha mambo mema ili tu aweke video ya matusi....hii ni laana..!!!
Jichunguze kishetani chako ni kipi kisha tafakari...kupenda JF ni hobby kupenda mambo ya kishirikina ni maarifa sio ushetani...usichanganye mada
 

Attachments

  • 1455891494139.jpg
    1455891494139.jpg
    18.5 KB · Views: 453
Mungu ni mwema ila safari bado ni ndefu kaka
Ni kweli.

Poleni sana, ila ndio Ibada.

Siku Arobaini si mchezo.

Hapo ndio kipimo cha Imani.

Mwenyezi Mungu awaangaze na kuwalinda kwenye kipindi hiki, mmalize salama
 
Ni kweli.

Poleni sana, ila ndio Ibada.

Siku Arobaini si mchezo.

Hapo ndio kipimo cha Imani.

Mwenyezi Mungu awaangaze na kuwalinda kwenye kipindi hiki, mmalize salama
Barikiwa kiongozi
 
Mkuu Mshana Jr, umeniacha kidogo uliposema vishetani viko vingi. Mimi nilidhani kuna shetani mmoja tu anaejidhihirisha katika matendo mbalimbali mabaya na pia Mungu mmoja tu anaejidhihirisha katika matendo mbalimbali mema. Kwa vile kwa upande wa shetani umesema kuna vishetani vingi ina maana na kwa upande wa Mungu nako kuna vimungu vingi? Naomba kueleweshwa hapo.
 
Back
Top Bottom