Kila kitambulisho cha Taifa kimegharimu tsh 89,800

Kila kitambulisho cha Taifa kimegharimu tsh 89,800

Bilioni moja ni milioni milioni moja.Ngoja nikuandikie kabisa bilioni moja ina sifuri 12.Kwa tarakimu inaandikwa hivi

1,000,000,000,000
Hii ni trillion moja.

Ebu cheki mdogo mdogo tueleweshane!
10 ni kumi
100 ni mia moja.
1,000 ni elfu moja.
10, 000 ni elfu kumi.
100, 000 ni laki moja.
1,000,000 ni milioni moja.
10,000,000 ni milioni kumi.
100,000,000 ni milioni mia.
1,000,000,000 ni BILIONI moja au milioni elfu moja.
10, 000,000,000 ni bilioni kumi.
100,000,000,000 ni bilioni mia moja.
1,000,000,000,000 ni bilioni elfu moja au TRILIONI MOJA.
 
Jamani kitambulisho ni katika mtindo wa smart card, taarifa zako zote zipo ndani ya hicho kitambulisho na hakuna sahihi nje kwa Sababu kinasoma na finger print...mambo ya digital...
 
Kuwa makini. 89800 nini? Shilingi, million au nini????
Tatizo nini hapa? Ina maana kuisoma hiyo namba hupati jibu kama iko ktk tens, thousands, millions au billions?? Kazi tunayo.
 
Nitoe ufafanuzi kwa nini natofautiana na wewe.
Kama umesoma marekani bilioni moja kwa mmarekani ina sifuri 9 nikiandika kwa tarakimu bilioni moja ni ni 1,000,000,000 ukipiga kwa kutumia hii ya wamarekani kila kitambulisho kimoja utapata kimegharimu shilingi 89,800 ULIZOSEMA wewe.

Mfumo wetu wa elimu Tanzania ni wa KIINGEREZA sio kimarekani Kwa mfumo wa kiingereza tunaoutumia Bilioni moja ina sifuri 12.Ukiiandika inakuwa 1,000,000,000,000.Ukipiga hesabu unapata milioni 89.8

WeWE BILIONI YAKO uliyotumia ina sifuri 9 YA KWANGU INA SIFURI 12 .Wamarekani bilioni moja ni milioni elfu moja ambayo ndio umetumia Waingereza bilioni moja ni milioni milioni moja ambayo ndio nimetumia sababu ndio inatumika tanzania
Tuandikie trilioni moja,
 
Uko sahihi kaka ila hiyo ilikua ni zamani, siku hizi zote ziko sawa tu

"In British English, a billion used to be equivalent to a million million (i.e. 1,000,000,000,000), while in American English it has always equated to a thousand million (i.e. 1,000,000,000). British English has now adopted the American figure, though, so that a billion equals a thousand million in both varieties of English"

Soma hapa How many is a billion? - Oxford Dictionaries
Umesaidia kumtoa tongotongo
 
Jamani kitambulisho ni katika mtindo wa smart card, taarifa zako zote zipo ndani ya hicho kitambulisho na hakuna sahihi nje kwa Sababu kinasoma na finger print...mambo ya digital...
Hata leseni ya udereva ya Tanzania inasoma na finger print!!
 
YEHODAYA mtu mzima taulo likimvuka uwa anachutama na si kusimama,tunajua NIDA wametutia hasira sana,Hesabu ni tatizo sio kwako ni kwa watanzania wengi tu,

179,000,000,000/2,000,000 Unapata ngapi? Jibu ni 89,500.
 
Hiki kitambulisho nilichonacho Mimi ndo cha ghalama hii yote.

Siamini Kama cha ghalama yote hiyo halafu kinazidi nyumba, matumizi na mshahara kwa mwaka mzima. Mbona Kama serikali inakinyma hadhi kupewa mm.

Hii nchi siielewi. Kama naumwa nakoswa pesa ya drip halafu nimepewa kitambulisho cha mamilion. Kweli serikali inawatu wa bageti ????????????
 
Nitoe ufafanuzi kwa nini natofautiana na wewe.
Kama umesoma marekani bilioni moja kwa mmarekani ina sifuri 9 nikiandika kwa tarakimu bilioni moja ni ni 1,000,000,000 ...

Niulize swali rahisi tu regardless ni bilioni ya UK au US. Bilioni walizopewa NIDA zina tarakimu 9 au 12? Yaani vitabu vya hesabu na transactions mbali mbali vya NIDA, Serikali, n.k. vinaonesha tarakimu ngapi? Labda hii ndio ingekuwa basis ya hii hoja mfu isiyo na maana.
 
NIDA walipewa shilingi bilioni 179.6 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho vya taifa.Vitambulisho walivyotegeneza na kugawia wananchi ni milioni mbili.Ukigawa pesa walizopewa na vitambulisho walivyotengeneza utapata jawabu kuwa kila kitambulisho kimoja kimegharimu shilingi milioni 89.8.

Nchi hii ina wezi.Ndio maana Maghufuli kweli ana hasira nao.
hii nchi chini ya serikali ya CCM Wizi umeshamiri.

cha ajabu hata katibu mkuu wao anatuhumiwa kwa ujangili
 
Umekosea umechukua bilioni ipi ile ya american bilioni au English BILION?

Bilioni ya mwingireza ina sifuri 12.Bilioni moja ni sawa na milioni milioni
ya mmarekani bilioni moja ina sifuri 9 yaani milioni elfu moja.
Kwa TANZANIA bilioni ni milioni milioni ndio niliyotumia
Nabaki na msimamo wangu Kitambulisho kimoja ni milioni 89.8 sio elfu 89.8 uliyotamka

ELIMU ELIMU ELIMU
 
duuuu!! mkuu hembu pitia trilioni za bajeti ya tanzania halafu ulinganishe na hizo bilioni zako za sifuri 12, na ujiulize mwenyewe hiyo serekali ilipata wapi hizo bilioni zako za kuwapa nida wakati hata trilioni zao za sifuri 12 hazifiki huko? au ulitamani kuchangamsha genge?
 
Mleteni huyo yehodaya hapa Kambangwa sec. nimpe darasa. Na anachoshindani ni vya std vi primary mada ya kwanza kabisa. Hiyo bilioni take ya USA haipo kwani hesabu na namba zote za dunia zipo sawa. Arejee SI units kwenye fizikia ya form one. Karbuni darasani Lumumba boys.
 
NIDA walipewa shilingi bilioni 179.6 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho vya taifa.Vitambulisho walivyotegeneza na kugawia wananchi ni milioni mbili.Ukigawa pesa walizopewa na vitambulisho walivyotengeneza utapata jawabu kuwa kila kitambulisho kimoja kimegharimu shilingi milioni 89.8.

Nchi hii ina wezi.Ndio maana Maghufuli kweli ana hasira nao.
Ndio mjue jinsi serikali ya ccm inavyo fuga majambazi na kulifilisi taifa letu,ni bora ifie mbali kabisa
1454748049439.jpg
 
duuuu!! mkuu hembu pitia trilioni za bajeti ya tanzania halafu ulinganishe na hizo bilioni zako za sifuri 12, na ujiulize mwenyewe hiyo serekali ilipata wapi hizo bilioni zako za kuwapa nida wakati hata trilioni zao za sifuri 12 hazifiki huko? au ulitamani kuchangamsha genge?
Hao ndio vijana wa lumumba, wao ni kuchapia tu
 
😀😀😀Ati kuna English Billion na American Billion??? Kwi kwi kwiii!! Mbavu zangu mweeee!!😀😀😀
 
YEHODAYA bana, ana jirohongumisha mno but where!!
Anapewa shule ya bure yeye kakomaa na hisia zake.
 
Back
Top Bottom