Kila Kiongozi anaona sifa kutatua kero badala ya kujisifu kwa kuzuia kero

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,794
3,361
Katika nchi yetu imeonekana kwa sasa sifa kuu ya klongozi ni kuwa mahiri wa kutatua kero.

Kiongozi anateuliwa leo, anaambiwa wewe utafaa kwenye kutatua kero hii.

Mfano ni kero ya mgawo wa umeme nchini. Zaidi ya maraisi 3 waliopita wamekuwa wakiteua mawaziri na wakurugenzi wa Tanesco kwa kigezo cha kudhani wana uwezo wa kutatua kero ya mgawo. Hadi leo kero iko palepale. Ilibuniwa Net group solution, ikaja Richmond, nk. Hizo mbinu zote zimekuwa hazizai matunda yenye kuonekana.

Raisi wetu wa kwanza Hayati Mwl. Nyerere alikuwa na tabia ya kuteua wabunifu wa vyanzo vya nishati ya umeme, na ndiyo haya mabwawa tunapoyatumia hadi leo. Hata hili jipya linalojengwa ilikuwa ni ubunifu wake.

Ina maana, tangu baraza la mawaziri la Mwl. Nyerere litoweke, mabaraza yaliyofuata kazi yao ni kutatua tu kero za umeme na siyo kubuni vyanzo vipya?

Tuna makaa ya mawe, gesi ya Mtwara, nishati ya jua na upepo, eneo kubwa la bahari, madini ya uranium, joto la ardhini, nk. Vyanzo vyote hivyo tumeshindwa kutumia?

We are not serious!

Naomba uongozi wa juu wa nchi yetu uache kuteua vilaza kwa vigezo dhaifu.
 
Back
Top Bottom