Ni aibu, Kinana na CCM mnawaza vyeo badala ya kutatua changamoto zinazolikabili taifa?

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Ni aibu kwa kiongozi mkubwa wa chama cha CCM.

kinachoiongoza na kuisimamia Serikali iliyoko madarakani kuzunguka nchini akitoa onyo kuzuia wale wanaotaka kujipanga kutafuta teuzi za kugombea nafasi za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu 2025.jambo ambalo kimsingi ni haki yao ya kikatiba.

Tulitarajia kwamba Makamu Mwenyekiti huyu wa CCM.Angeitumia ziara yake kukemea maovu makubwa ikiwemo ubadhirifu mkubwa unaoripotiwa katika miradi mbalimbali ya kimkakati pamoja na halmashauri za miji na majiji nchini TAMISEMI.

Badala ya kuitumia kugombea vyeo.

Wakati "Kinana" anayafanya hayo nchi iko gizani kutokana na ukosefu wa usambazaji umeme wa kutosha,bila kueleweka sababu za msingi za ukosefu huo wa umeme kutoka shirika la ugavi wa Umeme nchini Tanesco.

Jambo linaloathiri uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa,kwa sababu umeme ndio nyenzo muhimu katika shughuli za viwanda na pia kwa ujasiriamali mkubwa na mdogo nchini.

"Kinana" anawaza vyeo badala ya kuihimiza serikali ya Chama chake kutatua mgogoro mkubwa wa ukosefu wa mafuta ya Kuendeshea magari nchini. Kutokana na kinachoelezwa kuwa ni hujuma ya wafanyabiashara wakubwa wa sekta hiyo kuunda Syndicate ya kuficha Mafuta kwenye maghara ya kuhifadhia Nishati hiyo muhim, ili kusubiri bei mpya inayotangazwa na EWURA kila Jumatano ya kwanza ya kila Mwezi.

Wakati "Kinana" na CCM wanahombea vyeo, nchi iko kwenye mgogoro mkubwa wa ukosefu wa pesa za kigeni nchini.

Hali inayopelekea kuathiri mfumo mzima wa uagizaji bidhaa muhimu nchini.ikiwemo hiyo ya mafuta ya Dizeli na Petroli.

Tulitarajia Kinana kuyatumia majukwaa hayo kutuambia ni nini chama chake kimeishauri serikali kuhusiana na kadhia kubwa ya mkataba mbovu wa Kubinafsisha bandari na Maziwa yetu makuu pamoja na vipande vya ardhi ya maeneo husika kupitia Kampuni ya DP-WORLD ya Dubai.

Ni hivi karibuni tulishuhudia kupitia video clips mbalimbali mitandaoni ikimuonyesha Kinana huyu huyu akiwapokea wamiliki wa eneo katika wilaya ya Ngorongoro kule Loliondo.kupitia kampuni ya Ortelo Business Company OBC.

Jambo lililozua sintofahamu kwa jamii ya kitanzania ikileta maswali kutaka kuelewa Je! Kinana alikuwa pale Loliondo kama nani?

Na...
Je, alikuwa pale kama muwakilishi wa CCM kitaifa au kama mdau binafsi wa OBC.
 
Back
Top Bottom