Misri wamecheza mpira mzuri ndani ya dakika 45 zilopita,tegemeo la Afrika ni kuona Misri washinda hii game.
Baada ya kuwaona Cape Verde wakiwatoa jasho Hispania na sasa Misri kuongoza kwa goli 1, yatosha kuamini kuwa moja ya timu za afrika itafika nusu fainali ingine.
Jambo jingine nilojifunza ni kwamba safari hii mabeki wa timu za Afrika ni mabeki mshahara na hawapo Marekani kutalii, kwani Lamine kawekwa mfukoni na mabeki wa Cape Verde.
Jeremy Doku wa Ubelgiji nae kawekwa mfukoni na mabeki mshahara watatu wa Misri.
Ivory Coast nao wameshinda mechi yao ya kwanza.
Hivyo timu za Afrika nguvu mojawapo itayowasaidia ni kuwa na mabeki mshahara wanotekeleza majukumu yao vilivyo.
Kila la kheri timu za Afrika.