Ndugu yangu hata nchi nipewe mimi au wewe au yule, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania. Si mtalamu wa Jiographia au siasa au history; naomba kuuliza kuna nchi hapa duniani ambayo KILA mwananchi wake anamaisha bora?....jamaa yangu hapa ananiambia Luxembourg.
KILA mtanzania kuwa na maisha bora ni kazi....haiwezekani. Si kwamba nimekata tamaa kuwa raisi wetu hataweza, nachofahamu na nilivyofahamu tangia hii style ya uombaji wa kula KAMWE maisha bora kwa KILA mtanzania hayataletwa. Inawezekana "kwa kila mtanzania" ina maana yake.
Ni kweli watanzania yatubidi kufanya kazi kwa bidii ili tuwe na maisha bora; lakini kumbuka background ya mtu, mazingira ya mtu, uwezo wa mtu na support ya mtu. Hivi vyota, na mengineyo, yanamfanya mtu kuwa na uwezo wa kujuwa/kufikili ni jinsi gani ya kutatua au ya kuwa na maisha bora. mf Elimu tuipatayo mashuleni, shule nyingi zilizopo Tanzania, si elimu inayoweza kumkwamua mtu pindi aiishiapo kidato cha nne. Haimfanyi mtu awe endelevu. Hebu fananisha contents za mtu wa computer science aliemaliza pale UDSM na yule aliemaliza pale Bath university; je wanafanana? waliandaliwaje walipokuwa primary, secondary au utotoni.
Kwahiyo, HATA NIWE MIMI AU WEWE AU YEYE AU YULE, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania