Kikwete's most embarassing statements...

Hiyo siyo speech ni "Joke" ambazo wanasiasa wote wantumia. Obama ndiyo smart President, lakini anazungumza vitu vya kijinga kila wakati. Ukiwa mwanasiasa lazima ujue njia ya kukonect na watu wa mjini. Kwa sisi tuliotoka Dar (Kikwete pia) hizo ndizo lugha tunazotumia. Watu wa Bara wapo tofauti na watu wa Dar.

Haki you could be right lakini kibaya zaidi kwa huyu baba wa Bagamoyo ni kwamba hata matendo yake yanaendana na anachokifanya, he is never serious tofauti na mtu kama Obama ambaye anapiga mzigo. By the way, Haki tunakupa nafasi uombe radhi maana kwa kumlinganisha huyo jamaa na Obama ni kama vile umelinganisha dimbwi la maji na bahari.
 
Kwangu his most embarassing speech ni pale aliposema maisha bora kwa kila Mtanzania. Nilijua kutokana na rekodi yake hataweza lakini nikabishiwa, nikabezwa, nikaambiwa JK we acha tu...



maisha bora kwa kila mtanzania haikumaanisha watanzania wote ila ' kila mtanzania' anafahamika na mwenyekiti wa tanzania
 
..the most embarassing statement ni pale aliposema kuwa serikali ikiruhusu wanafunzi waliojifungua kurudi shuleni matiti yao yatakuwa yakichirizika maziwa madarasani.

NB:

..naomba mwenye ile speech atuletee hapa jamii forums.

Noooo! Kweli alisema haya? Nadhani unamsingizia, Mkuu!

Amandla......
 
..hii hapa chini aliitoa ktk mkutano wa UWT-CCM uliofanyika Dodoma.

KINA MAMA ENDELEENI KUZAA WASICHANA WAZURI KWANI KATIKA MIAKA HII MIWILI HATA KWENYE MASHINDANO YA UREMBO DUNIANI TUMETAMBA.

..tena hii anaelekea iliandikiwa ktk hotuba yake.

Pleeease JokaKuu! Na wakina mama wakapiga makofi na vigelegele? Haiwezekani.

Amandla......

Nimerudi tena kusoma. Sina la kusema.
 
This is sad , mimi bado sitaki SITAKI KUAMINI kama kweli alisema hayo maneno.
 
Mr. President suck the publicist

The writers and some of your advisors

ps. timing is every thing
 
Watanzania sio wavivu, lakini sera za siri za serikali yetu ni kujenga matabaka wazi ya uchumi. Wananchi wakitafuta mbinu za kujipatia mitaji hufilisiwa. Angalia DECI pesa zote za watu imekalia serikali na porojo kibao, wakiwazuga watu kwamba kesi iko mahakamani. Sikuwahi kusikia mwanadeci akilalamika juu ya DECI mpaka serikali ilipowapora watu hao kwa visingizio kibao.

Waliobahatika na matunda ya DECI sasa wako mbali kwelikweli, maana walishavuna na kuvuna na kuvuna wakaanzisha shughuri za uzalishaji na kuajiri. Serikali inasisitiza watu wakope benki na kulipa faida kuuuuubwa! Hata mahela ya Raisi tunayasikia redioni tu kwamba wateule wachache ndio wamepata, lakini hadithi haiendelei.... Wajinga ndio waliwao. Wao waliliua Azimio la Arusha la Mwalimu kwa kupenda ubepari, wanatekeleza kweli kweli sera za ubepari - kuwapo kwa matajiri sana na masikini sana. Mtu akiinua kichwa anakong'otwa. Kama mtu anabisha, irudi DECI na muone kama umasikini haujatokomezwa kwa wananchi wa kawaida.

Leka

...kwa hili la DECI hatupo pamoja. Inashangaza mpaka leo huamini kuwa DECi ni utapeli. Hizo fedha za DECI zilikuwa zinamultipl vipi, kwa miujiza?
 
Huyu alishindwa kabla hajaanza hata huo urais! Ujasiri ni pale mtu unapoweza kujigundua kuwa kuna mambo mengine huwezi, inawezekana kuna mambo anayaweza kwa ufasaha kabisa, lakini hili la Urais angesema jamani inatosha, mnisamehe!
 
Ndugu yangu hata nchi nipewe mimi au wewe au yule, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania.
Sasa kwa nini walitudanganya wakati wa kampeni?
Waje basi watuombe msamaha kwa kutudanganya halafu wasubiri hukumu yetu - tuwaambie msamaha umekubaliwa au umekataliwa basi ondokeni madarakani kwani mmeyapata kwa njia ya ghilba!
 
..the most embarassing statement ni pale aliposema kuwa serikali ikiruhusu wanafunzi waliojifungua kurudi shuleni matiti yao yatakuwa yakichirizika maziwa madarasani.

NB:

..naomba mwenye ile speech atuletee hapa jamii forums.

Duh hiyo imepitilizza kweli kweli..!
 
nafikilia Prezident kwenye kampeni zijazo atatumia maneno gani -Nguvu mpya kasi mpya na ari mpya ni zero katika miaka hii 5
sijui miaka mitano ijayo itakuwa ..?
 
Kwangu his most embarassing speech ni pale aliposema maisha bora kwa kila Mtanzania. Nilijua kutokana na rekodi yake hataweza lakini nikabishiwa, nikabezwa, nikaambiwa JK we acha tu...

Hii nafikiri bwana mkubwa alimaanisha kuwa "maisha bora kwa kila mwanamtandao" tena kwa njia ambazo si halali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom