Kikwete's most embarassing statements...

Juzi kwenye maswali mwisho aliwaomba radhi eti ohh kachukua muda mwingi hadi mechi ya mpira karibia inaisha ..... lol

mpira ni muhimu!!!!
Alijua kuwa anawaboa watu na maneno yake yasiyo na mbele wala nyuma, ndio maana watu wanaona bora kuangalia mpira kuliko kumsikiliza kiongozi wao. Na analifahamu hilo fika ndio maana aliwaomba radhi
 
kuhusu maisha bora kwa kila mtanzania...........ndiyo maana mimi huwa siwezi kupoteza muda wangu kusimama kwenye mstari muda mrefu ili kupiga kura..KAMWE SINTOFANYA UPUUZI HUU....huwa nawaambia watu wananishangaa...huwa nawauliza nifanye effort zote ili iweje???kwa faida ya nani???..sababu naamini kabisa hakuna faida ya pamoja...ila ni kwa baadhi ya watu ambao wanahusiana kwa namna moja au nyingine na atakayechaguliwa...hivyo siwezi kumchangua mtu ambaye sintopata faida kwake...yaani kama hatujuani kabisa,ni hapana...........ndivyo ilivyo

Na huko kutokukaa kwenye mstari mrefu kumchagua umpendae ndio kunampa nafasi ya urahisi huyo usiyempenda.

Jiulize kwa mfano kuna mtu unamfikiria kwamba anafaa na akashindwa kwa kura mbili tu, si utakuja kuijutia haki yako?

Kitu kinachowashinda watanzania wengi ni msimamo.

Kwa maana hio wakipatikana Zamanizamani wengi na wakaaamua kutokwenda kupiga kura, ndio kwamnza mheshimiwa anazidi kufurahi kwani anapita kiurahisi.

Nenda katoe sauti yako.

Haba na haba hujaza kibaba.
 
Kila mtu ana ambitions zake in life.Wengine kuwa Rais tu inatosha. Legacy gani ameiacha nyuma hilo sio shauri lake.
 
"nataka kulibadilisha hili jiji lenu liwe kama carlifornia" Pengine alimaanisha kuwa ataliboresha jiji la mwanza na sio kuli substitute. Mbona bongo tunamisemo mingi tu ya kimtindo huo? kama vile Bongo New York, hii huwa haimaanishi kuwa bongo ni sawa sawa na NY bali inaamanisha kuna maendeleo fulani. Pengine do maana ya JK. Ofcourse sio kama na halalisha pumba zake. Mnyonge mnyongeni jamaa
 
Kweli wewe ni Firstlady.

am sorry mie ni first lady nafight pia kwa haki za raia wa nchi

sio kwamba nimemuhurumia kwa sababu ya machafu yake na ndani ya serikari yake ,ila da ile post pole niliyo-quote imenichekesha nikajisikia ka ubinadamu kwa huyo sir mheshimiwa Prezidaa ,,
sorry but mie ni kamanda kikosi cha mbele kabisa kumake sure haki yetu inapatikana hata kama si kirahisi namna hii
 
Watanzania sio wavivu, lakini sera za siri za serikali yetu ni kujenga matabaka wazi ya uchumi. Wananchi wakitafuta mbinu za kujipatia mitaji hufilisiwa. Angalia DECI pesa zote za watu imekalia serikali na porojo kibao, wakiwazuga watu kwamba kesi iko mahakamani. Sikuwahi kusikia mwanadeci akilalamika juu ya DECI mpaka serikali ilipowapora watu hao kwa visingizio kibao.

Waliobahatika na matunda ya DECI sasa wako mbali kwelikweli, maana walishavuna na kuvuna na kuvuna wakaanzisha shughuri za uzalishaji na kuajiri. Serikali inasisitiza watu wakope benki na kulipa faida kuuuuubwa! Hata mahela ya Raisi tunayasikia redioni tu kwamba wateule wachache ndio wamepata, lakini hadithi haiendelei.... Wajinga ndio waliwao. Wao waliliua Azimio la Arusha la Mwalimu kwa kupenda ubepari, wanatekeleza kweli kweli sera za ubepari - kuwapo kwa matajiri sana na masikini sana. Mtu akiinua kichwa anakong'otwa. Kama mtu anabisha, irudi DECI na muone kama umasikini haujatokomezwa kwa wananchi wa kawaida.

Leka
 
sijaahidiwa chochote ahadi zetu sisi huwa ni fake promise ,,
nachoomba tu serikali inipe matrekta na Mafuta ya kilimo mwaka huu
mnisamehe ...

nakuelewa, kusema ukweli anatia huruma kweli baba wa watu. sijui baada ya kujikanyaga mpaka kutoa vidole na kutema pumba zoote hizo mbele ya kadamnasi huwa anajisikiaje, ningekuwa mimi ningekuwa nakosa usingizi,
na akienda nje afadhali wamshauri awe anaongea kiswahili halafu kunakuwa na mkalimani...
 
..hii hapa chini aliitoa ktk mkutano wa UWT-CCM uliofanyika Dodoma.

KINA MAMA ENDELEENI KUZAA WASICHANA WAZURI KWANI KATIKA MIAKA HII MIWILI HATA KWENYE MASHINDANO YA UREMBO DUNIANI TUMETAMBA.

..tena hii anaelekea iliandikiwa ktk hotuba yake.
 
Kina mama pia endeleeni kuzaa wasichana wazuri kwani katika miaka hii miwili hata kwenye mashindano ya urembo duniani tumetamba

Hii ni kweli JK (Joka Kuu) ?
 
Masanilo,

..nimesema alitoa kauli hiyo ktk mkutano wa UWT-CCM.

..najua ni vigumu kuamini kwamba alitoa kauli hiyo. mimi kilichonishangaza zaidi ni kuikuta ktk text ya hotuba yake. sasa naogopa kuamini kwamba aliandikiwa na akaisoma.

..au labda aliandika mwenyewe hiyo hotuba, manaake kama wewe ni speech writer lazima uwe na uoga kidogo kumuandikia Raisi utumbo kama huo.

..hotuba mzima iko kwenye link hii hapa chini ambayo ni website ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

.. bonyeza hapa
 
Masanilo,

..nimesema alitoa kauli hiyo ktk mkutano wa UWT-CCM.

..najua ni vigumu kuamini kwamba alitoa kauli hiyo. mimi kilichonishangaza zaidi ni kuikuta ktk text ya hotuba yake. sasa naogopa kuamini kwamba aliandikiwa na akaisoma.

..au labda aliandika mwenyewe hiyo hotuba, manaake kama wewe ni speech writer lazima uwe na uoga kidogo kumuandikia Raisi utumbo kama huo.

..hotuba mzima iko kwenye link hii hapa chini ambayo ni website ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

.. bonyeza hapa

Hii hata kama aliandikiwa lakini ni reflection ya Kikwete. Anaweza kusifia urembo wakati watoto kibao wanakaa chini kwenye vumbi wakati wakijaribu kujua maana ya neno jiografia.
 
Masanilo,

..au labda aliandika mwenyewe hiyo hotuba, manaake kama wewe ni speech writer lazima uwe na uoga kidogo kumuandikia Raisi utumbo kama huo.

..hotuba mzima iko kwenye link hii hapa chini ambayo ni website ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

.. bonyeza hapa

Hii kubwa kuliko....

Nimeiona hiyo sehemu nanukuu
Kina mama pia endeleeni kuzaa wasichana wazuri kwani katika miaka hii miwili hata kwenye mashindano ya urembo duniani tumetamba. Nancy Sumari alipata tuzo ya Mrembo Bora wa Afrika katika mashindano ya Miss World mwaka jana. Mwaka huu, kwenye mashindano ya Miss Universe, binti wa Kitanzania, Flaviana Matata, naye alifanya vizuri.
 
..tena hii anaelekea iliandikiwa ktk hotuba yake

Duh! aisee inaniwia vigumu kuamini kama hiyo hotuba aliandikiwa. Niko inclined kukubali kuwa alikuwa anaongea (anatoa hotuba) bila kusoma na baadae alichosema ndiyo kikawekwa kwenye maandishi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom