Kikwete yuko New York Marekani

Kikwete yuko New York Marekani

Jopo la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kupendekeza Namna Bora ya Dunia Kukabiliana na Majanga ya Afya limekamilisha kazi yake wiki iliyopita jijini New York.

Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete lilikabidhiwa jukumu hilo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon tarehe 2 Aprili, 2015 na kupewa muda wa kuanzia Mei hadi Desemba 2015 kukamilisha kazi yake.

Jopo limefanya mikutano minne na kukutana na wadau mbalimbali wa afya zikiwemo taasisi za Umoja wa Mataifa, wadau wa maendeleo, wataalam mbalimbali na kupokea maoni na uzoefu kutoka kwa nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola.

Watu mashuhuri wanaounda Jopo hilo ni Mheshimiwa Michelin Calm-Roy aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Uswisi; Mheshimiwa Marty Natelagawa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia; Mheshimiwa Joy Phumaphi, aliyekuwa Waziri wa Afya wa Botswana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Mheshimiwa Celso Amorim aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil na Rajiv Shah aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID).

Jopo hilo linatarajia kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi January, 2016 na baadae kuwasilishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
 
Kila Mtanzania ana haki ya kusafriri nje ya nchi. Wako Watz tele wanakwenda nje na kurudi mara kwa mara. Cha ajabu ni nini JMK kusafiri nje ya nchi? Tunaelewa maana ya Holiday na utalii, au tunadhani Waafrika ni duni sana kutalii nje ya nchi? Lets mind our own business and leave JMK alone.
 
Duh! Punguzeni chuki binafsi hivi mh. Kikwete kawafanyia nini hadi mumchukie hivyo? Yaani hakuna kizuri hata kimoja alichofanya? Kweli jamani! Basi anayejiona ni msafi na hana hatia aendelee na masimango yake. Ingawa majungu na matusi hayatawasaidia kitu.
 
Kwa sasa safari analipiwa na serikali au mshahara wake WA kustaafu?
kwakuwa alikuwa kiongozi WA umma watu kuhoji Ni haki Yao.
tuone sasa nani atachukua kombe la afrika mashariki na Kati,yeye au kenyatta?
 
Kila Mtanzania ana haki ya kusafriri nje ya nchi. Wako Watz tele wanakwenda nje na kurudi mara kwa mara. Cha ajabu ni nini JMK kusafiri nje ya nchi? Tunaelewa maana ya Holiday na utalii, au tunadhani Waafrika ni duni sana kutalii nje ya nchi? Lets mind our own business and leave JMK alone.

Huyo ni rais mstaafu, ungejua stahili za rais mstaafu basi ungeelewa kuwa ktkt safari zake hela ya serikali inahusika pia. Rais mstaafu ana wasaidizi ambao wanalipwa na serikali/ni waajirwa wa serikali anaosafiri nao, Hivyo lazima tuumie huyu mtu na tabia zake za kutapanya mapato ya nchi
 
Dumelang waswahili wa pwani ni wajanja c mafala km wabara,ht late nyerere analijua hili,kaja mjini kakuta wa mjini wameshaanza harakati za kutafuta uhuru,akaonyesha ushirikiano wakampa nafasi kubwa tu kwsbb wt wa pwani ni waungwana c washenzi km wabara,mwacheni jk afanye yk,msiwe na wivu km wtt wa kike,hakuna rais mjanja tangu nchi hii ianzishwe kumzidi jakaya huo ndo ukweli,muulizeni baba yenu lowassa anajua mjanja wake ni nani?remote ipo msoga na nchi inakwenda

Hilo nalo neno,,, watu wapwani walimpa nchi Nyerere,, watu wapwani wakamleta Mwinyi,, hawajakaa sawa watu wa pwani tena wakamleta MKAPA,, watu wapwani tena wakapambana wakamleta MAGUFURI,,, hawa jamaa jeuri yao inawaponza hawataki kukaa karibu na watu wapwani mwisho wa siku urais wanaukosa kila siku,, jamaa yao alijifanya mjanja na jeuri sasa kaonyeshwa jeuri ya pwani anabaki analialia tu,,, hii nchi ipo kwa hisani ya watu wa dar es salaam na pwani kwa ujumla ukijifanya mjanja inakula kwako,, na 2025 wakileta tena jeuri tunawaletea KHASIM MAJALIWA yaani mpaka raha...
 
ana pepo mchafu huyu MTU sio bure.... haiwezekani MTU uwe unapenda safari zisizo na kichwa wala miguu

duh,, hiyo safari haina kichwa wala miguu??
hiyo kazi ni ya UN na amepewa na BAN KI MOON
kawafanya nini huyu jamaa mpaka mnachuki naye kiasi hiki??
 
Mara nyingi nawaambia kumjadili kikwete ni kupoteza Muda, kutwanga maji kwenye kinu.
Tujielekeze kwenye Mada zenye tija.
Kikwete sasa anafanya kazi za kimataifa, nyinyi endeleeni kulalama bongo.
 
Mwacheni mzee apumzike nae anahaki kama watu wengine mnyonge mnyongeni lkn hakiyake apewe
 
Kosa langu ni lipi hapo? Kwamba nimemsingizia Raisi Mstaafu hayuko York Mpya Marekani? au ni nini? Mbona sikuelewi?

Ungekuwa wa maana kama ungesema anafanya nini kwa taarifa yako ana majukumu ya kimataifa alikuwa akiyasimamia toka akiwa Rais katika masuala ya afya. Umejaa chuki na stress utabaki kumgoogle tu wakati ukipigwa jua
 
Back
Top Bottom