Kikwete: Wanaokwepa Kodi hawataacha kirahisi, Magufuli endeleza mapambano

"Wanasema JK hachomoi,kwani mimi nilichomeka nini"
Daaaah huyu mkwere huyu,futuhi wampe chance!
 
kikwete ni raisi aliyeshindwa , haache kujiaibisha kwa kutoa kauli za kushindwa. Yeye alikuwa mfanya biashara na maswaiba wake wote ni wafanya biashara utawezaje kukusanya kodi kwa marafiki zako. Magufuri ni mtu wa kazi hana urafiki na mtu katika kazi
Point like1
 
CCM wanatakiwa kumkemea huyu Mzee akakae Msoga amuache raisi mpya afanye kazi kwa uhuru. Huenda anajitokeza hivi makusudi ili kumjengea woga rais mpya asiwabane wakwepa kodi. Kwa kauli kama hizi Magufuli lazima atakuwa anaogopa kivuli cha JK. Hiki kibabu cha Msoga inatakiwa kifunge bakuli na kurudi Msoga, sio busara kuonekana kwenye media mara nyingi kuliko raisi aliyeko madarakani
 
Tatizo la Kikwete ni kwamba hataki kukubali kuwa awamu zake zimeisha. Bado anang'ang'ania airtime ya Magufuli. Aliupenda sana urais na kuutafuta kwa udi na uvumba.

Alipoupata hakuutendea haki, akawa mtu wa ushkaji, starehe,fadhila na kusafiri kwenda Ulaya. He has to accept he is a failed president. Atulie nyumban kama Mwinyi na Mkapa walipomaliza zamu zao.

Tena kama anapenda siasa, aendelee na uenyekiti wa CCM lakini ajue kazi itafanyika hata kama hapendi.
 
mswahili shida sana hili zeeee. aibu sana kuwa na rais huyu. atolewe katika hesabu za watu walio tawala tz. kwanza ccm ilitakiwa imtoe katika uenyekiti. Huyu zimwi ndio aliyeiua ccm
 
Thanks ; kikwete....................... Watu walitegemea ungetoka na negative - umewaumbua kwa positive argurment
Nasisitiza,JF ni moja ya sehemu nzuri sana kupima IQ ya watanzina wewe ukiwa mmoja wao.

Akili yako sijui iko likizo?!
 
Leo ni siku ya usafi hivyo kama ulichafuliwa ni fursa kujisafisha kwa kujibu tuhuma
Mimi sioni alicho kosea hapo! Ni kweli wakwepa kodi kila diku wana buni mbinu mpya za kukwepa kodi hii ni vita ya kudumu na tukubaliane si rahisi kuitokomeza moja kwa moja kama wengi wetu tunavyo dhani,binafsi sina shaka JK ameyasema hayo kwa nia njema tu, watu wanakuja na maneno chungu nzima yenye lengo la kuchonganish? JK na JPM!!
 
Amewatuhumu wanao mlaumu kuwa wakati wa utawala wake ameruhusu misamaha mingi ya kodi na pia kuwa alizembea kuwabana watu wasilipe kodi.

Amesema Magufuli amewashinda sasa wanatafuta sababu za kushindwa kwao. Amesema kasi ya Magufili inawatisha ndiyo maana wanatafuta sababu zisizo za msingi na kuanza kumlaumu yeye kikwete.

SOURCE: TBC habari (DIRA) mchana huu.
 
Waache watapetape wachaga hawawezi kumsahau Kikwete na ile sacoss ndio inakufa kwa mziki wa Magufuli
 
Si alisema atafungua foundation yake?siasa aziache mana hana tena mvuto na hatuna muda naye,nashangaa kila siku unakuletwa uzi mpya kuhusu jk,hii haijakaa vizuri kwa uongozi uliopo sasa,kwa nn jk unatumia nguvu nyingi sana kupata publicity?
 
Ulishamaliza Uraisi wako na sasa siyo muda wa wewe kuanza kuwajibu watu wanaokushutumu kwenye mambo mbalimbali, kuna watu wanakupenda na kuna watu hawakupendi na hakuna kitu utafanya kubadishsa hawo watu wawili ningekushauri achana na media potea kabisa na endelea na maisha yako na achilia Historia ikuhukumu!

Jaribu kujifunza kwa maraisi wenzako waliopita kama Mzee Mwinyi na Mkapa kila siku wanaitwa Ruksa au sijui Mkapa mwizi n.k lkn hakuna siku Mzee Mwinyi au Mkapa wamejitokeza na kuanza kujiteteta hadharani kama ufanyavyo wewe, au hata Thabo Mbeki amesemwa sana baada ya kuacha Uraisi lkn hakuna siku amekuja na kuanza kuwajibu watu vile vile George Bush tangu amemaliza Uraisi wake amekaa kimya na anaendelea na mambo mengine wanaomchukia wanamchukia wanaompenda wanampenda!

Hivyo acha kutafuta kuwapa watu cha kuongea na kila unavyoongea ndivyo jinsi unavyozidi kuwapandisha watu chati ambayo wengine hata hawana, haiwezekani mtu mdogo kama Tundu Lisu aseme kitu Raisi au raisi mstaafu ahahahe usiku na mchana kujaribu kumjibu, common Kikwete wewe ulikuwa Raisi wa JMTZ , Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya Usalama TanZania, Bosi wa kila Mtanzania unabishana na mtu kama Tundu Lisu kweli?


Unanishangaza sana Kikwete kama alivyosema Maalim Seif!


Na ndio maana amewashauri kuwa, acheni kumsema sema kwa maana mnapoteza muda wenu.
 
Sina nipochomeka na sina haja ya kuchomoa.Hilo ndio neno nimelisia tu
 
Back
Top Bottom