JK na kunyanyapaaa! Jisomee gazeti la mwananchi, 29/09/2010
Akizungumza katika mkutano wake wa awali uliofanyika Kijiji cha Lalago, Kikwete aliunyamazisha umati huo baada ya kuanza kuelezea maambukizi ya Ukimwi yalivyoshamiri kijijini hapo na wilaya nzima ya Maswa.
"Ndugu zangu maambuziki ya ukimwi hapa yako juu sana. Maambukizi hapa Lalago ni asilimia saba, nikiwa na maana kuwa kati ya watu 100, saba wanaugua ukimwi. Maswa ina wagonjwa 3,000 wanaohudumiwa na serikali," alisema Kikwete.
"Sasa, naomba akina mama wanapokwenda kliniki, muombe kupima ukimwi. Ukipata Ukimwi unajitakia kwa hiari yako; unaweza kujikinga kwa kuwa kupata Ukimwi si bahati mbaya; ni bahati mbaya ni kwa mtu aliyebakwa au aliyeongezewa damu isiyo salama."
Kikwete aliongeza kusema: "Lakini wengine ni kwa viherehere; wanapanga kupata kwa kuwa mnapanga siku; saa; na mahala pa kukutania. Sasa basi, mkipanga mkubaliane, nani alete kinga, wewe
au yeye... ndugu zangu tufuate mafundisho ya viongozi wa dini kuwa msivunje amri ya sita.
"Wale ambao bado wasubiri wakati wao na wale ambao wako kwenye ndoa zao wadumishe uaminifu... hapa uaminifu ni mgogoro."