Kikwete: Walioambukizwa UKIMWI ni kiherehere chao

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Kauli aliyotoa Rais Kikwete akiwa katika mkutano wa kampeni wilayani Tarime, kuwa watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi inatokana na kiherehere chao, imezua utata.

Umoja wa mashirika yanayoshughulikia na waathirika wa VVU Kanda ya Ziwa wamemtaka awaombe radhi kwa madai kuwa kauli hiyo inawanyanyapaa waathirika wa ukimwi.

Mwenyekiti wa mashirika yanayotetea waathirika wa VVU Kanda ya Ziwa (LAZONEFA), James Lumumba, alisema mgombea huyo akiwa kama kiongozi wan chi ameonyesha njia ya kuanzisha unyanyapaa dhidi ya waathirika wa ukimwi, kinyume cha kampeni yake alioanzisha ya kupima kwa hiari.

Alisema mara kwa mara kiongozi huyo wan chi amekuwa akitoa kauli tata kuhusu masuala ya kitaifa, akitolea mfano kauli ya hivi karibunium aliyotoa dhidi ya vyama vya wafanyakazi kuwa hahitaji kura zao ikiwa watashinikiza kulipwa mishahara waliyopendekeza kupitia vyama vyao.

"Rais Kikwete alianzisha kampeni ya kupima kwa hiari kama ishara ya kupambana na maambukizi mapya ya VVU nchini, sasa iweje leo hii atupakazie kuwa tulkioambukizwa tulikuwa na kiherehere, au ndiyo kusema nasi hataki kura zetu kama wafanyakazi?" alihoji Lumumba ambaye pia alijitangaza hadharani kuwa mmoja wa watru wanaoishi na VVU…..

Chanzo: Tanzania Daima.
 
Huyu Rais si mzima. Ana matatizo makubwa sana. Mbona anatoa kauli za ajabu-ajabu? Kwa kweli lazima awaombe radhi wenye VVU/Ukimwi.
 
Kwani kauli yake hii kaanza leo? JK hana mapenzi au huruma na wananchi wake, ana uchu wa madaraka, na ndiyo maana kipindi hiki anajipendekeza hata kujigalagaza vumbini kuomba kura. Ila wakati mwingine anajisahau kama huko Tarime na kuonyesha dharau zake!
 
Ugonjwa huu unampata mtu kwa njia nyingi sana...Huwezi tamka just from the blues kuwa ni kiherehere!...mbaya kabisa hii!
 
Na nyie pia haitaji kura zenu. Mie naamini kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kumpa kura Kikwete.
 
aombe radhi, ila nna uhakika hatathubutu kuomba radhi kwa sababu hata wanafunzi wa kike hakuwaombaga radhi. Rais mipoint iliisha akaropoka tuuu!!! Watu si washapewa makofia?
 
Hi to all who commented, on the topic

huyu jamaa, uwezo wake wa kufiriki ni mdogo, tumuhukumu kwa kuzingatia hilo
 
Hii ni kauli mbaya zaidi kuliko hata ile ya kukataa kura za wafanyakazi. Fikiria mtu aliyepata VVU kwa kubakwa anaambiwa ana kiherehere wakati bado maumivu ya kubakwa nayo. Pia kumbuka kuwa wanandoa wengi wameambukizwa na wenzi wao ambao hawajatulia, je twawezasema kuwa walipata kutokana na kiherehere chao cha kuolewa? Huyu jamaa anafikiria umbali wa pua yake. Aombe radhi
 
Huyu Rais si mzima. Ana matatizo makubwa sana. Mbona anatoa kauli za ajabu-ajabu? Kwa kweli lazima awaombe radhi wenye VVU/Ukimwi.

You are right! Akipimwe akili huyu, but viherehere vya wanafunzi+Viherehere vya wenye ukimwi=Viherehere vya Taifa zima, du! ama kweli presidaaa hatuna.
 
What???? JK mwogope mungu wako. Hii ni kauli ambayo hata mwenye roho kama ya mwendawazimu hawezi kutamka. Unataka kuwaambia nini watoto wanaozaliwa na virusi nao ni kiherehere chao???? Haya mnaotaka kumpigia kura mtu asiye na huruma hata kwa wagonjwa. JK si umezaa watoto halijakukuta laiti lingekuwa limekukuta usingethubutu kutamka maneno haya.
 
Naamza kuhofia hata uwezo wa JK kufikiri. Siamini kabisa. Au ndio maradhi yake yamepanda kichwani?
 
Huyo ndiye JK ninayemfahamu, kukoboa ndio asili yake. Mwaka 2015 mkimuuliza mbona hukutimiza ahadi hii na ile na ile, atawajibu very simple, "si mlinipigia kura kwa viherehere vyenu". Wenye viherehere mpigieni kura JK.
 
mh!!!??? kwanza ingependeza walau tukapata hiyo stori ya huko tarime ilivyokaaa maana ndo yaleyale ya waandishi wabovu wa kitanzania, huo ni upande mmoja wa hadithi
ila ikiwa aliyoyatamka ni sahihi na kwa namna inayoashiria unyanyapaa, kwa kweli hafai,hafai na hafai kuwa kiongozi wa jamii yetu, kwetu sio tunaowaona wateja wa ukimwi na ukichukulia kutopatikana kwa baadhi ya dawa katika baadhi ya maeneo hapa nchini, hili linatushtua mno
 
Aliwahi kusema kuwa wanafunzi wanaopata mimba ni VIHEREHERE vyao. Huo ni ubaguzi na ukatili kutoka sakafu za moyoni bila kuchuja. na kwakuwa hili la ukimwi amelinena amini nakuambia kuwa hatuna rais hapo.

Kauli aliyotoa Rais Kikwete akiwa katika mkutano wa kampeni wilayani Tarime, kuwa watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi inatokana na kiherehere chao, imezua utata.

Umoja wa mashirika yanayoshughulikia na waathirika wa VVU Kanda ya Ziwa wamemtaka awaombe radhi kwa madai kuwa kauli hiyo inawanyanyapaa waathirika wa ukimwi.

Mwenyekiti wa mashirika yanayotetea waathirika wa VVU Kanda ya Ziwa (LAZONEFA), James Lumumba, alisema mgombea huyo akiwa kama kiongozi wan chi ameonyesha njia ya kuanzisha unyanyapaa dhidi ya waathirika wa ukimwi, kinyume cha kampeni yake alioanzisha ya kupima kwa hiari.

Alisema mara kwa mara kiongozi huyo wan chi amekuwa akitoa kauli tata kuhusu masuala ya kitaifa, akitolea mfano kauli ya hivi karibunium aliyotoa dhidi ya vyama vya wafanyakazi kuwa hahitaji kura zao ikiwa watashinikiza kulipwa mishahara waliyopendekeza kupitia vyama vyao.

"rais Kikwete alianzisha kampeni ya kupima kwa hiari kama ishara ya kupambana na maambukizi mapya ya VVU nchini, sasa iweje leo hii atupakazie kuwa tulkioambukizwa tulikuwa na kiherehere, au ndiyo kusema nasi hataki kura zetu kama wafanyakazi?" alihoji Lumumba ambaye pia alijitangaza hadharani kuwa mmoja wa watru wanaoishi na VVU…..

Chanzo: Tanzania Daima.
Nimeishiwa nguvu sijui how to hate him akafahamu. but i know what i will do in the ballot box.

Naamza kuhofia hata uwezo wa JK kufikiri. Siamini kabisa. Au ndio maradhi yake yamepanda kichwani?
Mkuu wangu, hiyo ni zaidi ya maradhi. NI UKATILI na UBAGUZI dhidi ya wananchi wake.

Jamani jamani mnaona how GOD anavyotufunulia how this man is?
 
Huyo ndiye JK ninayemfahamu, kukoboa ndio asili yake. Mwaka 2015 mkimuuliza mbona hukutimiza ahadi hii na ile na ile, atawajibu very simple, "si mlinipigia kura kwa viherehere vyenu". Wenye viherehere mpigieni kura JK.

This is good one!
 
Kauli hizi za ajabu ajabu ni kipimo kizuri cha uwezo wa mtu, sasa yeye anaendelea kupeta kwa sababu ya uzoba wa wadanganyika, na atasema mengi tu. Ujinga umekuwa tatizo kubwa nchini kwetu na hii inafanya viongozi wasio na hekima kuwa madarakani hama huyu, na cha ajabu wanaojiita wasaidizi wake ndio hao wengine tumewaona nao wanazamia kwenye ubunge na kusema ati mie nilimsaidia sana JK, ndio hao wanaomsadia kuibuka na kauli za ajabu ajabu, zisizo na mashiko yoyote!!
 
Hii si mara ya kwanza JK kutoa kauli kama hii. Wiki iliyopita akiwa Iringa kwenye kampeni, aliwauliza wananchi kwamba ikiwa watu wawili hupanga muda/wakati na mahali pa kukutana basi pia wakubaliane ni yupi atakayeleta kinga....

Binafsi kauli hii ilinikera kwa maana ilimaanisha kuwa watu hupata maabukizi
1. kwa kupanga - kwa sababu hukubaliana muda na mahali pa kukutania
2. watu wote wenye maabukizi wameyapata kwa kujamiiana kitu ambacho si kweli.

Kuna watu wamepata maabukizi kwa kubakwa, kuongezewa damu na wengine wameambukizwa baada ya kuuguza wapendwa wao.

Kilichokera zaidi ni kwamba ingawa clip ya habari hii ilirusha kwenye luninga (ITV kama sikosei) si asasi, wala mwandishi walau mmoja, wala watu binafsi waliokemea kitendo hiki.

Ikiwa raisi, ambaye ndiye kiongozi mkubwa kabisa katika nchi, anakuwa na perception kwamba ukimwi unaenezwa katika hali ya kujitakia...je sisi kama nchi tutegemee nini katika kupambana na ugonjwa huu ??
 
Back
Top Bottom