Kikwete vs Lissu, naomba tujikumbushe ya nyuma!

Kikwete vs Lissu, naomba tujikumbushe ya nyuma!

JK anajua kuwa TUNDU LISU ana matatizo ya akili na alishaugua kichaa. so kauli hiyo ilikuwa na maana kubwa na ujumbe mzito kwa watanzania. kwa maana mtu kichaa anaweza kuleta maangamizi kwa muda mfupi

Umeambiwa au unauthibitisho juu ya kuugua huko? Maanake magamba mnapenda sana vya kuambiwa(umbeya) mfano dhaifu ktk hotuba yake jana.ZINGATIA: TUMIA AKILI ZAKO KUFIRIKI KABLA YA KULOPOKA.
 
Jk mjanja sana!
"NILIKUWA SAFARINI",
"NIMEELEZWA"
"LABDA SIJAELEZWA" (hapa kakwepa kwa makusudi kusema LABDA NIMEDANGANYWA). Hahahaaaaaaaa! Kama kawaida ili wasimshitukie magamba sugu kuwa amewatosa" Akazuga kumpiga madongo TL huku akijua kabisa kakubaliana na hoja zake karibu zote za msingi.Sasa ngoja tuone jangwani wanaenda kusema nini maana kamchana live Nepi,Bulemba,tyson na lukuvu waache kumshambulia Waliob na wajumbe wake.
wapo boat moja,,,,,ila madaraja tofaut,najiuliza wamejihisije???mtu kama Bule-Mboo
 
JK anajua kuwa TUNDU LISU ana matatizo ya akili na alishaugua kichaa. so kauli hiyo ilikuwa na maana kubwa na ujumbe mzito kwa watanzania. kwa maana mtu kichaa anaweza kuleta maangamizi kwa muda mfupi

Nani huhangaika na kichaa???
Mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe! Acha kulala wewe!
 
Hadi unaandika/kuandikiwa hotuba na kuja kuisoma bado tu hujapata clarifications za hayo ambayo labda hujaelezwa? Sihasa bana!
 
Siasa za Tanzania ni kama mpira wa Tanzania.Chadema Vs CCM Simba Vs Yanga
 
JK anajua kuwa TUNDU LISU ana matatizo ya akili na alishaugua kichaa. so kauli hiyo ilikuwa na maana kubwa na ujumbe mzito kwa watanzania. kwa maana mtu kichaa anaweza kuleta maangamizi kwa muda mfupi

kwa sababu JK ndiye mama'ke wa kambo
 
my take,
ninashauri pia mkuu wa kaya akutane na muheshimiwa tundulisu ili kujiridhisha juu ya maneno aliyosema. Hii itamsaidia sana kupembua ukweli na uongo ni upi. Mara nyingi kusikia habari kutoka kwa mtu wa pili badala ya muhusika hupotosha. Nashauri apate audiene na mh. Tundulisu. Pia ni vyema mkuu wa kaya akafungua masikio kusikia wananchi wanasemaje bara na huko zanzibar akakosema wameshirikishwa. Ikiwa waziri wa sheria zanzibar analalamika juu ya mswaada huo huo je ukweli ni upi. Tunajua nia njema aliyonayo mkuu wa kaya hasa ktk mchakato huu wa katiba. Mungu bariki tanzania, tunataka katiba ya nchi.

hana muda wa kukutana na lissu!
 
Wadau, jana mkuu wa kaya alimchana live jembe la ukweli tundu lissu! Lakini naomba mwenye video clip ya yale maneno ya mkuu kuhusu tundu lissu kwenda bungeni, plz tuwekeeni ili ukweli udhihirike kuwa jk anamhanya tundu tangu kitambo! (samahani kwa ku2mia lugha ya vijana wa dijitali, am sorry)

Ninakumbuka katika Mkutano wa jangwani Lissu hakutaja vikundi vya dini na alitamka maneno yale alikuwa ni Lipumba .Kama nimekosea naomba kurekebishwa tafadhali ila jana nimeshanaga hotuba nzima JK na Tundu Lissu
 
my take,
ninashauri pia mkuu wa kaya akutane na muheshimiwa tundulisu ili kujiridhisha juu ya maneno aliyosema. Hii itamsaidia sana kupembua ukweli na uongo ni upi. Mara nyingi kusikia habari kutoka kwa mtu wa pili badala ya muhusika hupotosha. Nashauri apate audiene na mh. Tundulisu. Pia ni vyema mkuu wa kaya akafungua masikio kusikia wananchi wanasemaje bara na huko zanzibar akakosema wameshirikishwa. Ikiwa waziri wa sheria zanzibar analalamika juu ya mswaada huo huo je ukweli ni upi. Tunajua nia njema aliyonayo mkuu wa kaya hasa ktk mchakato huu wa katiba. Mungu bariki tanzania, tunataka katiba ya nchi.

kwanza hotuba yake imejaa maneno kama"nimeambiwa au nimeelezwa"kwahiyo mambo yote ameambiwa hajafanya uchunguzi anatakiwaachanganye na zakwakwe.
 
Kauli kwamba?
Kwa hiyo mswada utasainiwa au la?!

"Ndugu Wananchi;
Kama mtakavyokumbuka, Bunge lilitunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Novemba, 2011. Sheria hii imeweka mchakato mzima wa kupata Katiba hiyo na kuunda taasisi zake. Mwezi Mei, 2012, Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa na imekamilisha hatua tatu muhimu katika mchakato huo. Hatua hizo ni kupokea maoni ya wananchi, kutayarisha rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya na kupokea maoni ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na ya taasisi. Hivi sasa Tume inaandaa mapendekezo ya Rasimu ya Pili ya Katiba itakayopelekwa kwenye Bunge Maalum. Baada ya tafakuri zake, Bunge Maalum litatoa rasimu ya mwisho ya Katiba ambayo itapelekwa kwa wananchi kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kupitia kura ya maoni. Baada ya hatua hiyo, ndipo tutakapokuwa tumepata Katiba Mpya.
"
 
Wadau naona mada ya JK na Lissu inashika moto na watu kufikia kurusha matusi .Chabruma kaenda mbali na kumwita Lissu ni Mgonjwa wa akili .Mimi niliangalia ile hotuba ya Jangwani.Wenye clips wanaweza kuweka hapa kumaliza ubishi.Sikumbuki kusikia Lissu anaongelea habari za TEC nk ila Lipumba katika hotuba yale ndiye aliye ongelea hayo .Nilishangaa siku ile Lipumba kuongelea TEC wakati wanawatuhumu na Memorandum .Nataka tuweke records sawa na si kubishana na kuonekana sote tunayumba.Rais atakuwa kadanganywa na kwa kuwa clips zipo naomba tuziweke ili kuondoa uhama huu mkubwa na hasira a Rais kwa Tundu Lissu .Najua walipambana siku za nyuma akiwa waziri wa Nje nadhani inaweza kuwa ndiyo sababu ya kumuota LISSU ila kama sehemu Lissu alisema na si Lipumba tafadhali I am hereI stand to be corrected .

Tutafute ukweli na tuone kama kweli Rais alidanganywa au ni kweli Lissu alisema .Na kama Rais alidanganywa nia ya uongo wa mtoa habari ni ipi ?
 
Ikulu ipo wazi jamani! Kiongozi mkuu wa nchi anapokuwa mzembe wa kuifuatilia nchi yake ni hatari sana! Inavyoonekana JK anamuogopa sana Lisu.. Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini amuogope Mhe. Mbunge mmoja wakati ile ni hoja inayosimamiwa na wapinzani wote?
 


"Siyo tu kauli hiyo ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu."

lissu angekuwa ally usinge mtusi hivyo, nikujuwavyo
 
hapa jk hasitudanganye kuwa mawazo ya mh. Lissu yalikuwa ni ya uongo na kuwa mh. Lissu alikuwa na hiana. Kiukweli jk anamujua vizuri mh.lissu na ndo maana alishawai kusema kuwa ni bora dr. Slaa awe rais kuliko tundu lissu kuwa mbunge. Ameishakubaliana na hoja ya lissu kama tayari ameamuri mswaada urudishwe bungeni ili ujadiliwe tena,kwa maana hiyo jk amekataa kuusaini. Sasa jk atasemaje kuwa hoja ya lissu ni ya uongo na wakati watanzania walio wengi wamekubaliana na hoja ya mh. Lissu ya kuukataa mswada? Basi angesaini. Hivyo, hoja ya mh. Lissu na upinzani imekubalika kwa asilimia kubwa.
Hapa jk hasitudanganye, sema tu ameona aibu ya kumsifia mh. Lissu

tundu ni jembe jamani!!!!!tukubaliiiiiiiiiii.hata jk anamkubali lakini hataki kuwa wazi.
 
Back
Top Bottom