Kikwete unamuogopa Mwakyembe

Mwakyembe HAJAKEMEA Uovu wowote. Ni rafiki tu wa vyombo vya habari, hivyo anaripotiwa zaidi ya wenzake! Sasa atuambie waliomtegea huko Ihemi Iringa mwaka ule, wakampaka poda pale kazini kwake mpaka akapewa kofia kule India. Mbona yu kimya mpaka leo? Kwa sababu ya "zawadi" ya Uwaziri? Ama kweli hizi ni Pepo za mabwege!
 
Jamani haya yote,wamaweza kua saw a au si sawa,ila nijuavyo mm kwa maoni yangu mwakwembe kahamishwa wizara kwa kua wakubwa Fulani walikua wanashindwa kupitisha poda zao hapa D.I.A kwani Hali ilikua ngumu sana na wapo wanajulikana ss kwa shinikizo lao hao mazungu Wa poda walimshauri Mzee tutolee huyu kiumbe hapa watu tufanye mambo wetu mbona inajulikana
 
Dawa ya Mwakyembe sio kumtetea na kulalama kila kona! Kama yeye jasiri na mchapakazi anayekataa wezi na waovu, anajua majina yote ya vigogo anaosema wamemwondoa ili kufanikisha biashara zao kupitia 'kuliangamiza' shirika la reli (TRL), au kupitia njia haramu za usafirishaji kama magengo, na 'unga' aiport, na kupitisha nyara au bidhaa mipakani, kwa manufaa yao binafsi, AWATAJE MMOJA BAADA YA MWINGINE, aache woga! la sivyo kama anapiga porojo na woga, atakuwa anawahadaa watanzania, kuwadanganya na kuomba huruma 'ambayo hataipata kwa porojo' bali na kuwasema kiukweli-kweli! "Mwaga mboga nami nimwage ugali!" hatasahaulika akisema ukweli! Kama yeye mzalendo AWATAJE ili vyombo husika, PAC na taasisi nyingine zenye uzalendo zifuatilie na kuwawajibisha viongozi hao na familia zao!

Uhhhmmmmm!!
 
Jamani tusidanganyane sababu za uhamisho wa mwakyembe


Kilichofanyika (kumbadilishia portfolio) kimetafsiriwa na wengi kimakosa kwamba ametoswa wakati ukweli sio huo. Sanasana kilichotokea amehamishiwa kwenye wizara ambayo weledi wake, usomi wake na uzalendo wake utatumika kikamilifu na matunda makubwa zaidi kupatikana kwa nchi. Kwa maneno mengine kule aendako atamudu zaidi kulikohata kule atokako.


Na kweli kabisa tukitizama objectively, huku atokako Mhe Mwakyembe alipwaya. Tuache ushabiki- na kuwa move na television stunts za kufukuza wafanyakazi kwenye mikutano ya hadhara, kukamata wezi bandarini, kukamata wauza unga airport na kuchimba mikwara ya hapa na pale- kimsingi Mwakyembe hana accomplishment za msingi katika sekta ya uchukuzi nchini. Nitaelezea kwanini:


Sekta ya Anga
Mwakyembe ameingia madarakani, ATC ilikuwa na hali mbaya, leo anaondoka wizara ile ATC bado ikiwa taabani. Pamoja na jitihada za makampuni kadhaa ya nje kutaka kuingia Ubia na ATCL ikiwemo Turkish Airline, AVIC,Flydubai, Oman Air, Mwakyembe ameshindwa kuwezesha ubia mzuri kutokea ili Shirika hilo liondokane na laana ya kuwa shirika hoi na hatimaye lishindane na mashirika kama Fastjet, Rwandair, n.k- hapo Kenya Airways wala sina haja ya kujilinganisha nayo.


Sekta ya Bandari
kwenye sekta ya bandari Mwakyembe hakufanikiwa kuongeza ufanisi mkubwa uliotegemewa. Kikubwa alichoweza na hapo nampongeza ni kudhibiti wizi wa mizigo. Lakini mengine yote hakufankiwa. Toka aingia hadi anatoka idadi ya mizigo inayopitia bandari ya Dar es salaam ni ile ile container 400,000 kwa mwaka, wakati Bandari ya Mombasa katika kipindi hicho hicho imeongeza idadi maradufu. Kasi ya utoaji mizigo,urasimu na ukiritimba bandarini umeendelea kubaki vilevile,ndio kisa cha jirani zetu Rwanda na Uganda kuamua kuingia kwenye coalition of the willing ya Wakenya ili watumie bandari ya Mombasa. Ni ukiritimba huo umewafanya waone bora waunge mkono mradi wa reli ya kutoka mombasa hadi Nairobi kwa ajili ya kubeba mizigo yao, angali wakijua ni umbari mrefu, na gharama za usafiri zitakuwa kubwa kuliko route ya Dar es salaam......lakini wapi....wakaona bora ya lawama kuliko fedheha ya kutumia bandari ya Dar es saalam.


Wakati waziri Nundu anaondoka, ilikuwepo mipango kamambe ya kuboresha gati no 1-7 na kujenga gati mpya 13 na 14, lakini Mwakyembe toka aingie mipango hiyo imebakia kwenye makaratasi na ahadi hewa za maneno. Wawekezaji wengi wamejitokeza kutaka kufanya miradi hiyo kwa ubia na Serikali, mwakyembe ameshindwa kusimamia hilo litokee..... Ni katika kipindi hicho hicho, wakenya wamepata wabia wa kujenga gati mpya katika bandari ya mombasa- tena wabia hao walishaomba kuingia ubia Dar es aalaam wakapigwa chenga. Ni Mwakyembe huyo huyo, aliyeunda Bodi ya watu wenye weledi, kisha akawafukuza ndani ya miezi sita kwakuwa hawakukubaliana na mawazo ya Menejimenti ambayo Mwakyembe aliiamini na kuitegemea. Ni Mwakyembe huyo huyo ambaye toka ameingia hadi sasa, ameshindwa kusimamia mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu wa Shirika nyeti la Taifa, yaani Mamlaka ya Bandari Tanzania. Muda wote huo nafasi hiyo inakaimiwa (acting)........hakuweza kumconfirm anayekaimu, na kama alidhani hana uwezo anayekaimu, hajaweza kuteua anayefaa.


bandari ya Tanga na Mtwara zimeendelea kuwa bandari njiti zisizokua katika kipindi chote cha Mwakyembe. Bandari ya Bagamoyo imeendelea kuwa njozi ya kufikirika chini ya Uongozi wa Mwakyembe.


kwenye usafiri wa Maziwa, nako hakuna cha kuonyesha cha maana, sana sana kabla hajaondoka meli iliyokuwa inategemewa kwenye ziwa Victoria imesimamishwa (baada ya kuwa neglected miaka mingi kufanyiwa matengenezo, ikiwemo miaka aliyokaa Mwakyembe wizara ya uchukuzi). Kwenye ziwa Nyasa na Tanganyika habari ni ile ile, mile zilizopo zina hali isiyo ya kuridhisha....pengine Mwakyembe angetembelea kule pia, nazo angezifungia.


Reli
kwenye sekta ya reli habari ni ile ile....no progress, mere empty words. Ujenzi wa Reli katika viwango vya kimataifa umebakia kuwa njozi. Kushindwa kwa Mwakyembe kutekeleza mipango madhubuti aliyoiweka kufufua reli ile, kumepelekea Rwanda, Burundi na Uganda (wateja wakubwa wa bandari ya Dsm na reli ya Kati) waachane na Tanzania na kukimbilia mradi wa reli ya Kenya.




kwa analysis hii, ni sahihi kabisa kusema kwamba Mwakyembe, alipwaya kwenye wizara ya Uchukuzi, pamoja na makeke yake yote. Tatizo lake la msingi ni micro-management ya mashirika yaliyo chini yake....


Ninaamini kule alikopelekwa atakuwa na value zaidi....kwani kule anapokwenda anatakiwa mtu mwenye uwezo wa kujieleza, kujenga hoja, na umakini wa kuangalia maslahi ya nchi hayachezewi na nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Bahati nzuri Mwakyembe ameshawahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki.....anaifahamu vizuri process yote ya kule......atatumia weledi wake, ujuzi wake na uzalendo wake vizuri zaidi kule......



Falsifying the truth!!!
 
Hivi JK unataka tukukumbuke kwa lipi?? Mnona kila kitu unafanya kwa mapenzo yako binafsi badala ya kuangalia wananchi wako??? .

Safari 500 za Ulaya na Marekani katika kipindi chake ya urahisi kututafutia wapiga kura wake chakula tusife njaa! Yaani kwa lugha nyepesi 'da Gama of the 21st Century':(
 
Wakiyembe hamna kitu yule yeye anapenda kufanya kaz na vyombo vya habar kama alikuwa na ninia ya kufufuwa reli nchin mbona aliwaacha menejiment ya tazara kuiuwa tazara
 
Mkuu pixel shida ya watu wa Mabunga Kisale mpaka Kafundo ni shida aswa hata zahanati kwa vijiji hivi hamna isipokuwa zahanati ya Ngamanga.

kazi kweli kweli.

Hilo mkuu nakubaliana na nyie,pianieni haki zenu mpaka mwisho,piganieni maendeleo ya kyela yenu.mimi napinga kutumia uwaziri ili kuipendelea kyela kwa meli kama alivyoandika mleta mada kabla hajafuta na kuandika upya.
 
Falsifying the truth!!!
Ngurubhe...... Huo ndio ukweli mchungu. Nilichofanya ni kuacha ushabiki na kuelezea FACTS na sio kutoa hoja kwa hisia.

wewe nenda kwenye kila fact...niambie wapi ni uwongo....
..Bath 13&14 zimejengwa? Zipo wapi?

Reli ya Kati ishajengwa? Ipo wapi? Na je ni uwongo kwamba Rwanda na Uganda sasa wameamua kuweka matumaini yaomkwenye reli ya Kenya badala ya Tanzania?

ATCL ishatoka ICU? Ipo wapi?

Meli za uhakika katika ziwa Victoria na Tanganyika zishapelekwa? Zipo wapi?

Mkurugenzi Mkuu wa Bandari keshateuliwa? Ameteuliwa lini? Ninajua aliyepo anakaimu

niambie huo ukweli uliokuwa faslified ni upi? Tusipende kusifia vitu hewa........
 
Inaniuma sanaa Mwakyembe kubadilishwa sasa usafiri wa Treni ndio mwisho wake na mabasi ni ghali sijui nitaweza
 
Asee,mwakyembe ni mbunge wangu na mbaya zaidi ni jirani yangu nyumba ya tatu toka kwao ikolo kwa mama yake njia ya kwenda ngonga,hii n kwa faida ya wadau humu kule hakana alichofanya,kna manomba ya maji kila baada ya nyumba kumi yalijengengwa na wananchi miaka thelathini iliyopita kwa hisani ya mfuko flan wa jamii ndo pekee ukija kyela tena ikolo utakuta bara bara ni mbovu za zaman sana tena kuelekea bandarini na njia ni kokoto kwa upandea wa njia ya kwao inayopita uani kwao yaani nyumba yao n.kama jeng la benjamin mkapa afu bar bar ni ile ya nje pale ila ni ya vumbi,maji hakna tena mabomba yameziba,umeme hakna,mashirika na vikundi vidogo vya uuzaji wa kokoa vmekufa na magodwn pia yamekua magofu ambayo yalkua n sehm ya uchumi wa watu wa kyela...kwa kweli niljarbu kwend kukutana na badhi ya wadau wa chama na weny viti wa vijiji asee ni tatzo kwao pamoja na kua team mwakyembe ila shida zile za kule zmewavaa japo kyela n wilaya yenye utajir mkubwa sana na rasilimali nyingi haiitaji jambo kubwa sanaaa kufanya maisha ya wanakyela ambao kwa ssa n mchanyiko wa makabila karbu yote na mchaga na mkinga na mmakonde akiweka makaz kwa ajili ya biashar kufanya kyela iwe juu na nzr.na iwe ni sehem inayochangia pato la taifa kwa kiwango cha juu..ssa kiongoz anajenga nyumban kwanz na nje pia ssa kwa kweli mr kule kaacha kama alivyokuta sana sana jiran yetu pale mr mwamunyange mkuu wa majeshi ndo kidogoo kafany kitu sio yye..Asanteni
 
Watu wengi wanamjua Mwakiembe wa magazetini na kwenye TV.

Mwakiembe ni bomu mno. Hata kwao kyela wamemkataa kwasababu ya usanii wake.
 
Jamaa haangalii ufanisi yeye anaangalia namna anavyoweza kuwafurahisha anaohisi ni watu wake,yaani eti wanapeana ulaji zamu kwa zamu:)!!!!,,,

Yaani hii nchi imegeuzwa kikampuni cha familia kadhaa tu na wanaitafuna kweli kweli. Mwakyembe amerudisha imani na nchi majirani wanaotumia bandari yetu baada ya kukata tamaa kutokana na kuchukua muda mrefu kutoa mizigo yao na mingine kupotea hovyohovyo na makusanyo yalikuwa kidogo sana na Mwakyembe kayapandisha Kwa sana. Jamaa kaleta treni Dar na limesaidia wananchi wengi. Leo kweli unamtoa Mwakyembe wizara ile? Rais hauko na nia njema na hii nchi na watanzania wengi wanaoteseka Kwa umaskini ili hali kuna watu wachache wamejilimbikizia mali kiasi kwamba hata hawajuwi wazifanyie nini.
 
Mashauri,
Mwakiembe kapata wapi pesa bilioni
moja ya kununua kiwanja Bahari beach?

Ikulu wanajua kila kitu na deals zake bandarini ndio maana wamemtoa,

Hata yeye anajua kwanini katolewa.
 
mwakyembe lait km angekuwa waziri mkuu ingetosh sana lkn kule EAST .A nikumpoteza tu na madawa ya kulevya yaweze kupita vizuri airport
 
Hata mimi nimejaribu kuliangalia hili,nimeona kama kuna kupotezeana vile!!!!

Hivi umtoe Mwakyembe wizara ya uchukuzi halafu umlete msanii wa bongo muvi Sitta!!?


Huku si kuwatania watanzania!!?

Hapa umenena huyu msanii awezi kwendana na wazee wa Bandari, yeye huyu bado ana ndoto za kugombea Urais hivyo muda wa kufuatilia mambo kwa umakini hakuna, juzi watu wamefanya pati wanadai Mwakyembe aliwabana mno hata fedha za kutambia mitaani ilipotea kabisa
 
Jamaa haangalii ufanisi yeye anaangalia namna anavyoweza kuwafurahisha anaohisi ni watu wake,yaani eti wanapeana ulaji zamu kwa zamu:)!!!!,,,

Kuna mtu mchangiaji amenifurahisha kidogo. Anadai siku jamaa atapoacha urahisi wake isherehekewe kitaifa. Mimi naongezea atafutiwe kiwanja lushoto harafu tumuuwekee geti pale mombo akae huko na fisadi mwenzie aliyemuacha astaafu salama pamoja na mabaya yote alotufanyia ya kuuza nchi.
 
Mashauri,
Mwakiembe kapata wapi pesa bilioni
moja ya kununua kiwanja Bahari beach?

Ikulu wanajua kila kitu na deals zake bandarini ndio maana wamemtoa,

Hata yeye anajua kwanini katolewa.

Hii ni mpya aisee?! Ni kweli haya? By the way ka deliver hata hivyo. Kuna wengine ni matapeli na wezi halafu na utendaji ni sifuri pia ni hasara juu ya hasara
 
Ngurubhe...... Huo ndio ukweli mchungu. Nilichofanya ni kuacha ushabiki na kuelezea FACTS na sio kutoa hoja kwa hisia.

wewe nenda kwenye kila fact...niambie wapi ni uwongo....
..Bath 13&14 zimejengwa? Zipo wapi?

Reli ya Kati ishajengwa? Ipo wapi? Na je ni uwongo kwamba Rwanda na Uganda sasa wameamua kuweka matumaini yaomkwenye reli ya Kenya badala ya Tanzania?

ATCL ishatoka ICU? Ipo wapi?

Meli za uhakika katika ziwa Victoria na Tanganyika zishapelekwa? Zipo wapi?

Mkurugenzi Mkuu wa Bandari keshateuliwa? Ameteuliwa lini? Ninajua aliyepo anakaimu

niambie huo ukweli uliokuwa faslified ni upi? Tusipende kusifia vitu hewa........

Mbona Dr Shukuru kawambwa aliitwa mzigo...!! kamng'ang'ania?? msitudanganye bana....kiongozi dhaifu tunamjua!
 
Back
Top Bottom