Kikwete unamuogopa Mwakyembe

Kikwete unamuogopa Mwakyembe

Watu wa kyela hawana utani,
Nakumbuka yaliyomkuta Mwakipesile miaka ile.

Hapana, mwakipesile alikuwa ameisha tumika sana, walau hata barabara kuu ili wekwa lami, umeme pia tulikuwa hatuujui mgao, pia miaka aliyotumika ilikuwa inamtosha kabisa, ila huyu hapana anautani na watu, wacha apunzike. pamoja na kuwakuna uwezekano mkubwa wa kuchaguliwa tena, na hivi ni waziri sijui.
 
Dr Harison Mwakyembe alikuwa ni Waziri wa uchukuzi Wizara ambayo imekuwa na matatizo makubwa sana kiutendaji.

Kuanzia Dr Mwakiyembe alipokabidhiwa Wizara hiyo amefanya mambo makubwa sana kuhakikisha Sekta ya uchukuzi inafanya vizuri.

Moja ya mambo ambayo ameyashughulikia kwa nguvu zote ni usafirishaji kwa njia ya Reli ambayo ndio sababu kubwa ya yeye kuondolewa.

Ikumbukwe kuwa Viongozi wengi ndio wenye Makampuni ya usafirishaji kwa njia ya Barabara na kitendo cha kufuafua usafiri wa Reli ni pigo kubwa kwa watu wenye malori.

Ikumbukwe kuwa Viongozi wengi wanamiliki Malori mamia kwa mamia na wao ndio wenye tenda ya kubeba mizigo kutoka Viwandani kusambaza mikoani na nje ya Nchi.

Kwa mfano kipindi cha nyuma Cement kutoka Tanga kuja Arusha ilikuwa inasafirishwa kwa njia ya Reli kwa bei nafuu. Lakini sasa hivi ukienda Railway Station utaona Magari ndio yanayo shusha mizigo pale badala ya Train.

Sasa inamaanisha kuwa spidi ya Mwakyembe kufufua Reli ingekuwa ni pigo kwa wasafirishaji wa Malori kwani Train inasafirisha Mizigo kwa bei rahisi sana.

Kuchaguliwa kwa Samwel Sitta ni kuharibu System yote ambayo Dr aliweka kuhakikisha Sekta ya usafirishaji inakua.

Kama Sitta alivyoharibu Mchakato wa Katiba ndivyo atakavyo haribu Wizara ya Uchukuzi na Watanzania tusitegemee jipya ktk Wizara ya Uchukuzi.

Kuondolewa kwa Makyembe ni kwa faida ya Vigogo na Familia zao.
 
Yaani: Wakati mwingine ukisikia mambo kama haya unatamani kuwararua mafisadi na washenzi wanaotudumaza kwa ulafi wao. Tumefanaya makosa makubwa sana kukubali kuongozwa na mijitu kama hiyo inayonunuliwa na wenye malori ili ijinufaishe yeneyewe! Sijui nani kailoga Tanzania? Alisha kufa?
 
wizara ya afrika mashariki chini ya sitta imepoa na kupoteza mashiko hyo JK ameona ni vyema apeleke Jembe mwakyembe

mpaka sasa sitta atakuwa na kazi rahisi uchukuzi
 
Wauza sembe wameiweka siri kali mfukoni pale air port sasa wanapita bila hofu yeyote.
 
Naamini kama Cementi ingesafirishwa kwa Treni hakika leo tungenunua cementi tshs 7000 kwa Mfuko. Tz ni Shidaaaaaaaaaaa.
 
ww ni miongoni mwa mawaziri wazuri kabisa, mpo wawili ww na yule mwingine, kitu ambacho sijaelewa ni kwa nini mkuu wa kaya amekutoa uchukuzi, lkn kwa wanao tazama kwa jicho la3 watakuwa wanafahamu, kuhoji hatuwezi dah! na hata tukijibiwa lazma itakuwa blah! blah! doh tufwire nyambara. ! nkamugwangu.
 
Siasa za Tz bwana

Jamani tusidanganyane sababu za uhamisho wa mwakyembe


Kilichofanyika (kumbadilishia portfolio) kimetafsiriwa na wengi kimakosa kwamba ametoswa wakati ukweli sio huo. Sanasana kilichotokea amehamishiwa kwenye wizara ambayo weledi wake, usomi wake na uzalendo wake utatumika kikamilifu na matunda makubwa zaidi kupatikana kwa nchi. Kwa maneno mengine kule aendako atamudu zaidi kulikohata kule atokako.


Na kweli kabisa tukitizama objectively, huku atokako Mhe Mwakyembe alipwaya. Tuache ushabiki- na kuwa move na television stunts za kufukuza wafanyakazi kwenye mikutano ya hadhara, kukamata wezi bandarini, kukamata wauza unga airport na kuchimba mikwara ya hapa na pale- kimsingi Mwakyembe hana accomplishment za msingi katika sekta ya uchukuzi nchini. Nitaelezea kwanini:


Sekta ya Anga
Mwakyembe ameingia madarakani, ATC ilikuwa na hali mbaya, leo anaondoka wizara ile ATC bado ikiwa taabani. Pamoja na jitihada za makampuni kadhaa ya nje kutaka kuingia Ubia na ATCL ikiwemo Turkish Airline, AVIC,Flydubai, Oman Air, Mwakyembe ameshindwa kuwezesha ubia mzuri kutokea ili Shirika hilo liondokane na laana ya kuwa shirika hoi na hatimaye lishindane na mashirika kama Fastjet, Rwandair, n.k- hapo Kenya Airways wala sina haja ya kujilinganisha nayo.


Sekta ya Bandari
kwenye sekta ya bandari Mwakyembe hakufanikiwa kuongeza ufanisi mkubwa uliotegemewa. Kikubwa alichoweza na hapo nampongeza ni kudhibiti wizi wa mizigo. Lakini mengine yote hakufankiwa. Toka aingia hadi anatoka idadi ya mizigo inayopitia bandari ya Dar es salaam ni ile ile container 400,000 kwa mwaka, wakati Bandari ya Mombasa katika kipindi hicho hicho imeongeza idadi maradufu. Kasi ya utoaji mizigo,urasimu na ukiritimba bandarini umeendelea kubaki vilevile,ndio kisa cha jirani zetu Rwanda na Uganda kuamua kuingia kwenye coalition of the willing ya Wakenya ili watumie bandari ya Mombasa. Ni ukiritimba huo umewafanya waone bora waunge mkono mradi wa reli ya kutoka mombasa hadi Nairobi kwa ajili ya kubeba mizigo yao, angali wakijua ni umbari mrefu, na gharama za usafiri zitakuwa kubwa kuliko route ya Dar es salaam......lakini wapi....wakaona bora ya lawama kuliko fedheha ya kutumia bandari ya Dar es saalam.


Wakati waziri Nundu anaondoka, ilikuwepo mipango kamambe ya kuboresha gati no 1-7 na kujenga gati mpya 13 na 14, lakini Mwakyembe toka aingie mipango hiyo imebakia kwenye makaratasi na ahadi hewa za maneno. Wawekezaji wengi wamejitokeza kutaka kufanya miradi hiyo kwa ubia na Serikali, mwakyembe ameshindwa kusimamia hilo litokee..... Ni katika kipindi hicho hicho, wakenya wamepata wabia wa kujenga gati mpya katika bandari ya mombasa- tena wabia hao walishaomba kuingia ubia Dar es aalaam wakapigwa chenga. Ni Mwakyembe huyo huyo, aliyeunda Bodi ya watu wenye weledi, kisha akawafukuza ndani ya miezi sita kwakuwa hawakukubaliana na mawazo ya Menejimenti ambayo Mwakyembe aliiamini na kuitegemea. Ni Mwakyembe huyo huyo ambaye toka ameingia hadi sasa, ameshindwa kusimamia mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu wa Shirika nyeti la Taifa, yaani Mamlaka ya Bandari Tanzania. Muda wote huo nafasi hiyo inakaimiwa (acting)........hakuweza kumconfirm anayekaimu, na kama alidhani hana uwezo anayekaimu, hajaweza kuteua anayefaa.


bandari ya Tanga na Mtwara zimeendelea kuwa bandari njiti zisizokua katika kipindi chote cha Mwakyembe. Bandari ya Bagamoyo imeendelea kuwa njozi ya kufikirika chini ya Uongozi wa Mwakyembe.


kwenye usafiri wa Maziwa, nako hakuna cha kuonyesha cha maana, sana sana kabla hajaondoka meli iliyokuwa inategemewa kwenye ziwa Victoria imesimamishwa (baada ya kuwa neglected miaka mingi kufanyiwa matengenezo, ikiwemo miaka aliyokaa Mwakyembe wizara ya uchukuzi). Kwenye ziwa Nyasa na Tanganyika habari ni ile ile, mile zilizopo zina hali isiyo ya kuridhisha....pengine Mwakyembe angetembelea kule pia, nazo angezifungia.


Reli
kwenye sekta ya reli habari ni ile ile....no progress, mere empty words. Ujenzi wa Reli katika viwango vya kimataifa umebakia kuwa njozi. Kushindwa kwa Mwakyembe kutekeleza mipango madhubuti aliyoiweka kufufua reli ile, kumepelekea Rwanda, Burundi na Uganda (wateja wakubwa wa bandari ya Dsm na reli ya Kati) waachane na Tanzania na kukimbilia mradi wa reli ya Kenya.




kwa analysis hii, ni sahihi kabisa kusema kwamba Mwakyembe, alipwaya kwenye wizara ya Uchukuzi, pamoja na makeke yake yote. Tatizo lake la msingi ni micro-management ya mashirika yaliyo chini yake....


Ninaamini kule alikopelekwa atakuwa na value zaidi....kwani kule anapokwenda anatakiwa mtu mwenye uwezo wa kujieleza, kujenga hoja, na umakini wa kuangalia maslahi ya nchi hayachezewi na nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Bahati nzuri Mwakyembe ameshawahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki.....anaifahamu vizuri process yote ya kule......atatumia weledi wake, ujuzi wake na uzalendo wake vizuri zaidi kule......


 
Hebu mpigie simu mwakiembe tusikie yeye binafsi anasemaje?
 
Hapo hakuna ukweli wa hivo !! labda asilimia nduchu sana %...lakini Ni waziri mzalendo....
 
Mabadiliko yoyote yanalengo la kuborehsa mada siyo mrefu mzee sitta ataanzia alipoishia mwakyembe na matunda yake yataonekana wenyewe mtashangaa sitta anajua kazi kweli.
 
Back
Top Bottom