Kikwete to USA (May 2009)

Wangesema tu kuwa yuko private visit na kuacha kutoa dana dana zisizo na mbele wala nyuma. Because in reality that is what it is.
 
Watanzania bwana, yaani huko San Francisco hakuna hata mtanzania moja aliyempokea kwa bango - naambiwa kwa vijembe huko ndiko kwenyewe. Kumbe pamoja na kukaa unyamwezini, akili za mbongo bado ni zile zile za uswahilini. Nilikuwa nasubiri kushuhudia anavyotupiwa mayai viza - ama ndo yale yale ya kujipitisha pitisha usisahaulike ?
 

Hakuna hayo wewe...Waafrika makunguru sana. Hapa penyewe tunapiga makelele lakini watu tukipata fursa ya kumwuliza maswali ana kwa ana tunakuwa na ile nidhamu ya woga. Sasa nani atathubutu kumshikia mabango na kuandamana kumpinga?
 
Mag3,
San Francisco alikutana na kundi la Watanzania 10. Sasa walichaguliwaje hiyo sijui. Hata ukiangalia maswali waliyouliza ilikuwa ni a very friendly audience.
 
Mag3,
San Francisco alikutana na kundi la Watanzania 10. Sasa walichaguliwaje hiyo sijui. Hata ukiangalia maswali waliyouliza ilikuwa ni a very friendly audience.

Lakini Jasusi mbona huyu Kikwete keshawahi kukutana na wabongo huko DC na sijui Nyu Yoki...na kilichotokea ni watu kujipendekeza pendekeza tu
 
Lakini Jasusi mbona huyu Kikwete keshawahi kukutana na wabongo huko DC na sijui Nyu Yoki...na kilichotokea ni watu kujipendekeza pendekeza tu
Nyani,'
Naona sasa kuna mtindo wa kuchagua nani aonane na muishimiwa. Hapa DC watu wake wamekataa asionane na Watanzania eti kwa sababu tuna matatizo ya uongozi katika Jumuiya ya Watanzania. Lakini mimi nadhani it goes deeper than that. Najua San Francisco there are more than 10 Tanzanians na hata pale Hotelini alipofikia kuna ukumbi mkubwa tu wa kuweza kuchukua 100 people. So why only 10?
 

Uongo! Daily News mnatoa 'facts' za uongo ili iweje? Kwani wale wa SA na Ethiopia aliyekutana nao London mnajifanya mmesahau?
 
Last edited:
Hakuna hayo wewe...Waafrika makunguru sana. Hapa penyewe tunapiga makelele lakini watu tukipata fursa ya kumwuliza maswali ana kwa ana tunakuwa na ile nidhamu ya woga. Sasa nani atathubutu kumshikia mabango na kuandamana kumpinga?

Mimi hapa NN. Bango langu litakuwa 'UTAWALA WAKO ZERO KABISA HAIJAPATA KUTOKEA. BORA MKOLONI'
 
President Kikwete and his delegation arrived here on Saturday, for a week-long official tour and is scheduled to visit President Obama at the White House on Friday.


Nchi hali ya uchumi mbaya, suala la mabomu kwake lilikuwa la siku moja tu, lakini USA ana wiki nzima ya kutumia kuchungulia watu wengine wakifanya kazi zao. Hivi hii ndio kazi ya raisi tena wakati mgumu kama huu?

Makubwa haya.
 

Jasusi si unajua tena, hizi sifa anazomwagiwa muungwana na hizi nchi wakati mwingine chanzo chake ni sisi wenyewe. Kama wabongo huku majuu wangeweza kumzomea ama basi kumtolea uvivu, safari za nje zingeweza kupungua. Nyumbani hatulii kwa kuogopa kero za wananchi au kupopolewa mawe, lakini huku yaonekana anapata ahueni - anaokutana nao hawampi kibano - badala yake wanarefusha shingo na wao waonekane.
 
Uongo! Daily News mnatoa 'facts' za uongo ili iweje? Kwani wale wa SA na Ethiopia aliyekutana nao London mnajifanya mmesahau?

I don't believe he had any official meetings with them in London. As i recall he only officially held meetings with Brown, Hu Jintao, and Medvedev.

Besides they might be talking about at the White House.
 

yaani nikisoma kipande hicho hapo juu namkumbuka Kikwete siku ile yule Dada wa CNN alipomuuliza maswali Kikwete....kwenye ule mkutano na IMF........YES JK IS A RESPECTED AND A GREAT THINKER.........hii imakaaje wadau
 
huyu raisi wetu mbona haeleweki jamani...hivi anakazi nyingi za kufanya nje kuliko ndani??? ni mbona akiwa hapa nyumbani huwa haitishi mikutano na watanzania na kulonga nao live kuhusu masuala ya nchi wale wa nje wanamchango gani mkubwa huku nyumbani??? au kuna lingine/??????
 
Steve D hongera kwa kazi nzuri mkuu. Mimi kinachonishangaza juu ya Jakaya ni kwamba he neither listens nor learns , kwasababu kama kweli angekuwa anasikiliza ushauri angetulia nyumbani na kufanya kazi badala ya kuzurula kama machinga! Anatutia aibu mbele ya macho ya International community; kwani kweli kama nia yake ilikuwa kuwaalika hao wenye makampuni ya komputa kuja kuwekeza mbona hakuongozana na waziri anaehusika na Teknologia!! Juu ya yote hayo makampuni aliyokwenda kuyatembelea Silicon Valley yote yameathirika na hii global financial meltdown kwahiyo emphasis yao kubwa kwa sasa ni kuimalisha makampuni hayo huko kwao kwanza; charity begins at home! Kwa vile muungwana amezoea kusafiri ndio maana hata akialikwa na NGO ya kiushikaji marekani jamaa anapanda pipa anaondoka hata kama kuna emergency ya watu kupigwa mabomu!! kweli nchi imepatikana!!
 
Hivi Obama amesafiri nje ya nchi yake mara ngapi na atasifiri mara ngapi mwaka huu?
 
Hivi Obama amesafiri nje ya nchi yake mara ngapi na atasifiri mara ngapi mwaka huu?
Companero,
Obama kishaenda Uingereza, Ufaransa,Uturuki, na nchi nyingine sikumbuki sawasawa, lakini hakuenda kukagua ofisi za IBM au Cisco. Pia Julai atakwenda Misri na Ghana. Kishaenda Mexico, Canada na South America kwenye mkutano wa mataifa ya bara la Marekani alipokutana na Chavez. Kama kuna safari nyingine sikumbuki atajazia Nyani Ngabu.
 
JK atuwambie kwenye bakuli letu la ombaomba zimejaa ngapi ?Na atuambie matumizi yake je na ametoa na nani hajatoa mchango ili tujue kama anaweza kupendwa kwa tabia hiyo ili 2010 tuone kama anafaa au tumpe mtu mwingine.
 

Kumbe naye kasafiri kote huko kujiwekeza within his 100 days in office!

Afrika inaabudu utatu wa Unsustainable Aid, Unequal Trade & Unending Debt!

Sasa Mkuu ameamua ku-focus kwenye utatu huo mwacheni asafiri!

Ikumbukwe alijitetea kuwa anaenda huko kuvutia tuliwe ili nasi tule!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…