Kikwete: Tatizo la maji Dar kubaki historia

Posa

Member
Nov 12, 2010
76
79
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema tatizo la maji mkoani Dar es Salaam litabaki kuwa historia kuanzia mwaka mmoja ujao, kwani mikakati kabambe imewekwa kwa ajili ya kuongeza vyanzo vya maji.

Vile vile, ameahidi kuzipandisha hadhi zahanati zote za jijini Dar es Salaam kuwa vituo vya afya na hospitali ya Amana kuwa ya rufaa.

Alitoa ahadi hizo jijini Dar es Salaam jana wakati wa mikutano yake ya kampeni katika maeneo ya Kiwalani, Kitunda na Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

Alisema chanzo cha maji hivi sasa Ruvu Juu kinatoa lita 60,000 kwa siku na Ruvu chini lita 90,000 kiasi ambacho hakitoshelezi mahitaji ya maji jijini Dar es Salaam.

Kikwete alisema mahitaji ya maji ni lita 360,000 kwa siku hali iliyosababishwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu kulinganisha na miaka ya nyuma.

Alisema kwa msaada wa watu wa Marekani, Serikali inaendelea kupanua Ruvu Chini ili iweze kuzalisha kiasi kikubwa cha maji.

Alisema wakati Serikali ikiendelea na mkakati wake wa kupanua vyanzo vya maji, chanzo kingine cha maji kimegundulika Kimbiji kutokana na utafiti uliofanywa na wataalamu wa Norway.

"Watu wa Norway waliniambia Kimbiji imejaa maji mimi nikawauliza hayo si mafuta jamani wakaniambia hapana ni maji, na wakanionyesha mchoro kweli ni mengi kama nusu ya yaliyoko Ziwa Victoria," alisema.

Alisema katika uzalishaji huo yatapatikana maji lita 260,000 kwa siku ambazo zikiunganishwa na zile zinazopatikana katika vyanzo vingine yatakuwa yanatosheleza mahitaji ya Dar es Salaam.

Aidha, alisema awali wataalam wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) na Dawasco, walimweleza kuwa mpango huo unaweza kukamilika ndani ya miaka mitatu.

"Waliponiambia kuwa mradi huo utakamilika ndani ya miaka mitatu, nikasema hapana lazima tuangalie namna ya kuukamilisha mapema, nikasema visima apewe mkandarasi mwingine, ujenzi wa matenki mkandarasi mwingine na usambazaji wa mabomba makubwa ya kuleta maji Dar es Salaam, apewe mkandarasi mwingine na nina uhakika tutakamilisha mapema," alisema Kikwete.

Alisema mtandao wa zamani wa mabomba ambao umechakaa unaondolewa na kuwekwa mpya kazi hiyo inafanywa kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China.

Kuhusu barabara, alisema Serikali itaendelea kuongeza fedha katika mfuko wa barabara ili nyingi zijengwe kwa kiwango cha lami.

Alisema katika kuondoa msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, Serikali itazijenga barabara za pembezoni kwa kiwango cha lami ili watu wote wasilazimike kwenda mjini kwa kutumia barabara moja.

"Tunataka mtu akitoka Morogoro anakuja huku asilazimike kwenda hadi Buguruni, akifika Kimara kule anakunja kulia anakuja huku kwa kutumia barabara nyingine, na yule aliyeko Tegeta akitaka kwenda Morogoro asilazimike kwenda hadi Ubungo apitie kule kule," alisema Kikwete.

Kuhusu barabara ya Mombasa Kivule, alisema kinachosubiriwa ni watu waliojenga kando kando ya barabara hiyo walipwe fidia na kisha ijengwe kwani fedha za ujenzi zipo.

Aidha, alisema serikali itaendelea kuiongezea uwezo Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) ili viweze kukopa zaidi kwenye taasisi za fedha na kukopesha wanachama wake wafanye biashara na kuondokana na umaskini.

Rais Kikwete aliitumia mikutano hiyo kujibu kauli zilizotolewa na wanasiasa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, dhidi yake.

Kikwete alisema kuwa mashambulizi ya Chadema dhidi yake ni dalili za hofu ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.


Chanzo: NIPASHE

Tupime, tujadili kuna muelekeo wa hayo yaliyoahidiwa?
 
¡°Waliponiambia kuwa mradi huo utakamilika ndani ya miaka mitatu, nikasema ha pana lazima tuangalie namna ya kuukamilisha mapema, nikasema visima apewe mkandarasi mwingine, ujenzi wa matenki mkandarasi mwingine na usambazaji wa mabomba makubwa ya kuleta maji Dar es Salaam, apewe mkandarasi mwingine na nina uhakika tutakamilisha mapema,¡±
...ila hii ni kama tutapata msaada kwa 'wakubwa' kama daudi na wenzake...
 
mambo mazuri hayataki haraka trust jk! Litakuwa kweli historia ....

"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯
 
Jk tumekuchoka na ahadi zako hewa, unafikiri nani atakuamini kwa ahadi hizo. We maliza muda wako tu utoke hapo soko la samaki.
 
Hata akipewa miaka 10 mingine zaidi JK huyu ninayemfahamu hawezi kamwe kutimiza japo mojawapo ya ahadi hizo. Kibaya zaidi ni Wadanganyika wanavyodanganyika kirahisi. Ni aibu watu wazima tena wenye familia zao kukubali kudanganywa kiasi hicho, na bado wakiendelea kuimba na kwaya yao ya kina komba "nambari wani ni sisiem, au amechukua ameweka waaa"
 
Nilikuwa nadhani kasema jana kumbe mambo ya ahadi za uchaguzi!! Kutekeleza ahadi ni mchakato. Tungemuuliza Mwandosya yuko kwenye hatua gani ya mchakato wa kutekeleza hizo ahadi za rais.
 
siasa za jk hizo, siasa za ''nimeongea na Obama sasa hivi, amesema atatupa hela ya kununua vyandarua zaidi'

hovyo kabisa!!!
 
Aidha, alisema awali wataalam wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) na Dawasco, walimweleza kuwa mpango huo unaweza kukamilika ndani ya miaka mitatu, sasa ni.

“Waliponiambia kuwa mradi huo utakamilika ndani ya miaka mitatu, nikasema hapana lazima tuangalie namna ya kuukamilisha mapema.

Japo utekelezaji ni mchakato. Sasa hivi ni zaidi ya mwaka umepita na kama watalaam walichukua ushauri wake basi hatuna zaidi ya miaka miwili ya utekelezaji, je kuna dalili
 
mambo mazuri hayataki haraka trust jk! Litakuwa kweli historia ...."ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯
Hata kukatika kwa umeme aliahidi itakuwa historia toka mwaka 2005
 
Mkuu,
Ahadi za huyu bwana wala hata usihangaike nazo, ni kuachana nazo tu!!
Katuahidi mengi sana ambayo mengine ukijiuliza utaumwa sana kichwa bure mtu wangu!!
 
Too bad that all the people who really know how to run the country are busy driving taxi cabs or cutting hair. As a result those who do not even possess a wee amount of leadership experience oftenly become the MPs and heads of states. Making things awful is their invariable predisposition to pledge on unfulfilled promises and their inclination to exploit the public's desperations for their own advantage. JK, during past presidential campaigns, did commit himself to erecting fly-over roads at areas notorious for traffic jam while he privately knew that his promise might be far from incarnation.
 
"Watu wa Norway waliniambia Kimbiji imejaa maji mimi nikawauliza hayo si mafuta jamani wakaniambia hapana ni maji, na wakanionyesha mchoro kweli ni mengi kama nusu ya yaliyoko Ziwa Victoria," alisema.

"Waliponiambia kuwa mradi huo utakamilika ndani ya miaka mitatu, nikasema hapana lazima tuangalie namna ya kuukamilisha mapema, nikasema visima apewe mkandarasi mwingine, ujenzi wa matenki mkandarasi mwingine na usambazaji wa mabomba makubwa ya kuleta maji Dar es Salaam, apewe mkandarasi mwingine na nina uhakika tutakamilisha mapema," alisema Kikwete.

Kikwete alisema kuwa mashambulizi ya Chadema dhidi yake ni dalili za hofu ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Yani nimecheka mpaka mbavu zinauma, dahh waswahili kweli tuna kazi..
 
Kaaazi kweli kweli, hii furahidai imekuwa nzuri sana baada ya kusoma hii thread. Kazi kwao waliompa kura zao kwa kutegemea kupata maji wakati wanajua jamaa ni mswahili halisi.
 
Back
Top Bottom